Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoani Pwani imetoa ufafanuzi kuhusu hali ya Barabara kutoka Sheli hadi Mpigi na ile ya kuelekea Tankini na Muheza katika Kata ya Mailimoja kwa kusema kuwa ilipeleka kiasi cha Shilingi Milioni 420 kwa mgawo wa Shilingi Milioni 30 kwa kila kata.
Taarifa ya Manispaa hiyo imeeleza kuwa kata zilizopata fedha hizo ni 14 ambapo ni mapato yaliyotokana na makusanyo ya ndani.
Hoja ya awali ~ Halmashauri ya Kibaha hizo Tsh. 420M za kuboresha Barabara, zimetumika katika Barabara zipi?
Imeeleza kuwa kila kata kupitia Kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata kiliteua barabara ambazo ni kero na kufanyia marekebisho kutokana na kiasi hicho cha fedha.
Taarifa imeongeza kuwa kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 50 kupitia mapato ya ndani kwa kila kata kwa kata zote 14 kwa ajili ya maboresho ya barabara za mitaa.
Mbali na hapo imeelezwa kuwa Barabara hizo zipo chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na inachofanya Halmashauri ni kutoa fedha kwa ajili ya maboresho.