Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ofisi ya Kata ya Mpera yawatoza Tsh 2000 Vijana wanaotuma barua za maombi ya kazi za ukusanyaji wa Anuani za Makazi

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ofisi ya Kata ya Mpera yawatoza Tsh 2000 Vijana wanaotuma barua za maombi ya kazi za ukusanyaji wa Anuani za Makazi

Na nyie jifunzeni kuheshimu muda wa watu.

Hivi unafikiri kazi ya WEO Ni kukaa tu ofisini kusubiri watu walete barua zao ugonge mihuri?

Watu kama nyie ningekiwa Mimi, Wala hata nisingepitisha barua yako.
Sio kazi yake kivipi mkuu, si ndio maana tumeambiwa tupeleke huko? Wana majukumu mengi ndio ila na hilo ni mojawapo
 
Nyie ndo Huwa hamjielewi hivi nani anatakiwa ajue Hali halisi kati ya anayetafuta ajira na aliye ndani ya ajira? Mwenye ajira si ndo anatakiwa amhurumie ambae Hana maana uhalisia wa maisha unamuumiza Sana asie kua nacho.

Wala hii sio ishu ya ubush lawyer kutambua haki zako na mipaka ya kazi ya mtu mwingine sio ubush lawyer ni jukumu lako na ni haki yako zinduka ndugu
ivi hujawahi pata huduma serikali za mitaa ee kabla, au hata kwa mjumbe
kwa mjumbe tu kwenyewe kuweka sahihi yake inabidi uache 1000

documentation yoyote ile inayohitaji notarization ya serikali ndogo (ya mtaa) siyo bure
 
Sio kazi yake kivipi mkuu, si ndio maana tumeambiwa tupeleke huko? Wana majukumu mengi ndio ila na hilo ni mojawapo
Mmeambiwa mmepeleke huko lakini hshaurutishwi kumpitishia barua mtu yeyote.

Maana yake, unapitishq baraua kwake ili kuthibitisha kama kweli wewe Ni mkazi wa kata hiyo.

Sasa akisema hakujui kama Ni mkazi wa kata hiyo unafanyaje ?
 
Kiongozi wa serikali ya mtaa hawezi kumjua kila mtu kwenye mtaa wake hata itokee nini hasa kwa hapa mjini, ndio maana wengine ili kujiridhisha wanakutaka ulete utambulisho kutoka kwa mjumbe wako.
 
ivi hujawahi pata huduma serikali za mitaa ee kabla, au hata kwa mjumbe
kwa mjumbe tu kwenyewe kuweka sahihi yake inabidi uache 1000

documentation yoyote ile inayohitaji notarization ya serikali ndogo (ya mtaa) siyo bure
Mfano, Wenyeviti serikali za Mitaa hawana mishahara.

Hivi anadhani wanafaidikaje ?
 
ivi hujawahi pata huduma serikali za mitaa ee kabla, au hata kwa mjumbe
kwa mjumbe tu kwenyewe kuweka sahihi yake inabidi uache 1000

documentation yoyote ile inayohitaji notarization ya serikali ndogo (ya mtaa) siyo bure
Kwa sheria ipi? Mbona sehemu nyingine wanapitisha bure ina maana hawalijui hilo?
 
Sio kazi yake kivipi mkuu, si ndio maana tumeambiwa tupeleke huko? Wana majukumu mengi ndio ila na hilo ni mojawapo
Hivi mfano, unauza Kiwanja au nyumba yako, shuhuda wa kwanza mwenyekiti serikali ya mtaa.

Je, utalipa au Ni sehemu ya majukumu yake ?
 
Hivi mfano, unauza Kiwanja au nyumba yako, shuhuda wa kwanza mwenyekiti serikali ya mtaa.

Je, utalipa au Ni sehemu ya majukumu yake ?
Nikifika huko kwenye kununua na kuuza mashamba nitajua kwa sasa hivi niache kwanza.
 
Kiongozi wa serikali ya mtaa hawezi kumjua kila mtu kwenye mtaa wake hata itokee nini hasa kwa hapa mjini, ndio maana wengine ili kujiridhisha wanakutaka ulete utambulisho kutoka kwa mjumbe wako.
Na mjumbe wako hachukui hata 100 ?

Haya tuambie yeye analipwa na Nani?
 
Walipokuwa wanagombea hawakujua kuwa hakuna mishahara? Tena wanarogana hadi kurogana kwenye hizo nafasi...ili wakale kwa urefu wa kamba zao
Ubishi up na utabisha mpaka ugale gale chini.

Lakini mwisho wa siku , wewe ndio UTAKAYEPOTEZA.
 
Ubishi up na utabisha mpaka ugale gale chini.

Lakini mwisho wa siku , wewe ndio UTAKAYEPOTEZA.
Rushwa rushwa rushwa...rushwa ni adui wa haki. Tunabariki rushwa ndogo ndogo ila zikifika huko juu tunaanza kulalama....
 
Mimi sehemu zote nilizopita sikudaiwa hata 100
Of course, siyo kila mtu anataka pesa.

Mimi naishi Mombasa Ukonga, ila kwa Hulu barua zote ili upitishiwe lazima utoe chochote.

Lakini Kuna siku nimewahi kupeleka barua yangu serikali za Mitaa, Kinondoni hawakudai pesa yoyote ILA tu unatakiwa uwe na barua ya Mjumbe. Sasa hiyu Mjumbe ndio alitaka 3,000.
 
Naona mnanishambulia tu kumbe mimi ndo nipo nyuma ya wakati Ina maana Siku hizi hata kazi za serikali mpaka utoe kitu kidogo? Haya mambo tulizoea huko kwenye sekta binafsi sio serikalini
Kwani wewe ndio umeanza kufanya kazi na watumishi wa serikali hivi karibuni..mbona hii ndio maisha yetu...hatutoi rushwa ila tunaharakisha huduma.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi sidhani kama hizo Ni RUSHWA. Labda uziite TIP za lazima.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] kama ni tip haikupaswa kuwa lazima. Tena inatakiwa utoe mwenyewe au uombwe baada ya huduma ili hata kama huna huduma upate
 
Habari za wakati huu wana jamvi,

Billa kupoteza wakati Kuna kitu jana nimekishuhudia nikabaki kinywa wazi. Kuhusu hizi nafasi ambazo serikali imekuwa ikitangaza hivi karibuni Katika halmashauri na wilaya mbali mbali nchini kuhusu kazi ya kukusanya na kuweka vibao vya ANWANI ZA MAKAZI.

Jambo la kusikitisha nililoliona Katika halmashauri ya manispaa ya Tabora ofisi ya kata ya Mpera ni kwamba watu wakipeleka barua zao Ili zisainiwe na watendaji wa kata na mtaa baada ya kusainiwa wanaambiwa watoe shilingi elfu 2000/=.

Kijana mmoja akajaribu kuhoji "mbona kwenye maelekezo ya tangazo hakuna mahali tumeambiwa tulipe hio elfu 2000/=?"

Akaambiwa "hayo ndo maelekezo tuliyopewa" na akaoneshwa orodha ya waliotoa hio pesa idadi ni kubwa kidogo.

Basi yule kijana akamwambia "mimi sina hio pesa maana sikuona maelekezo yake"

Akaambiwa "wewe una kiasi gani hapo ulipo Ili tukusaidie?"

Yule kija akawajibu "Sina kiasi chochote,"

Akaambiwa "haya kama huna basi katoe hio barua yako copy ulete copy ya hio barua."

Nikabaki najiuliza.

1. Ina maana serikali imetoa maelekezo watu walipie pesa kuomba hizo nafasi?

2. Je, waliotoa pesa hizo pesa zinapelekwa wapi?

3. Je, ambao hawajatoa pesa kama huyo kijana atakuwa na ukakika wakupata hio kazi hata kama anakidhi vigezo?

4. Inawezekana waliotoa pesa ndo wakapewa priority kuliko ambao hawajatoa?

5. Ikiwa ajira hii ya siku chache hivi mtu analipishwa je zile kazi za muda mrefu huwa watu wanatozwa kiasi gan?

Maswali ni mengi itoshe kusema inasikitisha sana.

Wasalaam
Haya yasipokemewa mapema tutaangamia
 
Back
Top Bottom