Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imetoa ufafanuzi kuhusu uchakavu wa madarasa ya Shule ya Msingi Kibisi iliyopo Kata ya Kyimo kwa kueleza kuwa kuna kiasi cha Tsh. Milioni 10 kimetengwa kwaajili ya maboresho.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mwananchi kuhoji kupitia JamiiForums.com kuwa “Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe hii Shule ya Msingi KIBISI mmeamua kuipotezea?” ambapo alieleza taasisi hiyo inakabiliwa na hali mbaya ya miundombinu, huku madarasa wanayosomea watoto yakiwa yamechakaa kwa kiwango kikubwa.
Hoja ya awali ~Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe hii Shule ya Msingi KIBISI mmeamua kuipotezea?
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Rungwe, Noah Kibona ameeleza kuwa Halamshauri imetenga Tsh. Milioni 10 kukamilisha maboresho ya madarasa hayo mawili ambayo yapo kwenye hali ya uchakavu kwa kuwa tayari maboresho yalishafanyika kwenye chumba kingine cha darasa pamoja na ofisi ya Walimu.
Ameongeza kuwa maboresho hayo yalifanyika katika Mwaka wa Fedha 2024/25, hivyo mwishoni mwa mwezi juu Juni au mwezi ujao Julai 2026 mchakato wa maboresho utaanza katika vyumba viwili vilivyoelezwa na Mdau.
Amesema “Hatua zinaendelea kwa ajili ya upatikanaji wa kibali cha kubomoa majengo chakavu hatua itakayosaidia Wanafunzi kusoma katika mazingira tulivu.”
Majengo ambayo yameshaboreshwa 👇🏽