Halotel acheni wizi

Halotel acheni wizi

Kuna mtindo wameanzisha halotel wa kuiba data hata kama umezima data.
Kwa Sasa ukiweka hata bundle la 1000 baada ya sekunde unakuta zimeisha na hapo hujadownload chochote.
Huu ni wizi na nadiriki kusema huu mtandao ni majambazi
Ukiweka salio 5000 kila siku wanakata fedha kidogokidogo
 
Karibu nikuunge bando za mwezi mkuu za data, usahau hayo maswahibu.
Issue siyo bundle, tunazungumzia tabia ya udokozi ya Halotel
Ukiweka salio la 5000 kesho asubuhi usilitumie, ikifika Monday hutakuwa na 5000 ila utakuta deductions
 
Issue siyo bundle, tunazungumzia tabia ya udokozi ya Halotel
Ukiweka salio la 5000 kesho asubuhi usilitumie, ikifika Monday hutakuwa na 5000 ila utakuta deductions
Bro kutunza pesa ni kazi, Halotel nao ni watu🤣
 
Issue siyo bundle, tunazungumzia tabia ya udokozi ya Halotel
Ukiweka salio la 5000 kesho asubuhi usilitumie, ikifika Monday hutakuwa na 5000 ila utakuta deductions
Personally haijawah kunikuta, ila kwa ushauri uwe unatumia halopesa zaidi kuhifadhi pesa kwakuwa kule hakuna muingiliano, pesa ikikaa kama vocha hupungua kwa sababu nyingi. mfn, utatuma message mfumo unakuwa huru kutumia salio lolote iwe vocha au bando lako la message, hivyo muingiliano km huo unaweza kupelekea salio kupungua.

Utajiuliza siku ambayo umejiunga DK za wiki na za saa 24.. wakati unapiga wanatumia za wiki zinakwisha unabaki na za siku, unajiuliza imekuwaje kumbe umeupa mfumo options kitu ambacho mwisho wake unabaki lawama kwa mteja.

Jitahidi Sana km huhitaji vocha kwa wakati huo usiiweke, badala yake pesa hiyo iweke Halopesa kwa matumiz ya wakati ujao.
 
Hawa halotel wana tabia ukiweka vocha ya buku basi kwenye harakati za kujiunga ,...unaambiwa salio halitoshi...ukiangalia salio unaambiwa Ni 900 dah washaniibia kwa staili hii mara nne ...ila ipo siku yao...
 
utatuma message mfumo unakuwa huru kutumia salio lolote iwe vocha au bando lako la message, hivyo muingiliano km huo unaweza kupelekea salio kupungua.
  1. Kila mwanzo wa mwezi naweka Tzs 15,000
  2. Najiunga kifurushi cha kupiga 4,500 mwezi
  3. Najiunga kifurushi cha sms mwezi
  4. Kinachobaki huwa ni akiba yangu in case vifurushi vimekwisha usiku au nikiwa sehemu isiyo na duka
  5. Hiyo akiba ndiyo wananiibia
 
Pole Sana mkuu, itabidi siku moja kama wateja lialia tuandae kikao cha wadau kujadili na namna Bora ya kuliwasilisha hili kwako. Linaonakena ni kilio cha wengi.
 
Kuna siku nami ilitokea hadi nikapiga simu huduma kwa wateja kukalamika.

Nilichojibiwa nadhani kilikuwa sahihi, nilielezwa kuwa, kuna baadhi ya application zikiwa wazi hugeuka viwavi wa kubungua data hata usipotumia.

Kama tatizo haujalitafutia ufumbuzi nieleze nikuelekeze namna ya kuzuia.
Mkuu Naomba nitajie mfano WA hizo application maana nisijekuwa nafukuza mwizi wakati mwizi mwenyewe nnaye mm
 
Mkuu Naomba nitajie mfano WA hizo application maana nisijekuwa nafukuza mwizi wakati mwizi mwenyewe nnaye mm
Ingia kwenye SETTING:>
Sim and network setting>
Data &security>
Data setting and data usage>
Network management>
App list.

Hizo Application list utakuta zipo wazi zikisubiria kutafuna data, ukizizima unakuwa umeukata mzizi wa fitina.

Sasa utakapohitaji kutumia data kwenye app ulizozizima, simu yako itakudai kuwasha app hiyo ndiyo iweze kufanya kazi.

Cha muhimu uielewe formula hii ya kuzima ama kuwasha hizo App list.
 
Kuna siku nlichukia nkatamani ata nikawashtaki.. Yani nlikuwa na salio sh 700 nkannua vocha ya 500 ili niunge bando la buku, nashangaa wanasema salio halitoshi kuja kucheki nkakuta ipo ile 500 nloweka muda huo na ile 700 washaruka nayo. Nkaona isiwe kesi nkannua tena vocha ya 500 ili niongezee naile ilobaki iwe 1000 ninnue kifurushi.. kuunga tena wanasema salio halitoshi..! Kucheki nakuta kuna 900 yan wameruka tena na sh 100.

Ikabidi ninnue tena vocha ya buku ndo nkaunga bando.

Yan nlikuwa na hasira ingekuwa kuna sehem yakwenda kushitaki ningeenda kuwashitaki wezi kabisa hawa..
 
Ingia kwenye SETTING:>
Sim and network setting>
Data &security>
Data setting and data usage>
Network management>
App list.

Hizo Application list utakuta zipo wazi zikisubiria kutafuna data, ukizizima unakuwa umeukata mzizi wa fitina.

Sasa utakapohitaji kutumia data kwenye app ulizozizima, simu yako itakudai kuwasha app hiyo ndiyo iweze kufanya kazi.

Cha muhimu uielewe formula hii ya kuzima ama kuwasha hizo App list.
Asante
 
Back
Top Bottom