Hama hama ya viongozi wa CHADEMA inarudisha nyuma hamasa ya vijana kuupambania upinzani

Duuh kuna vijana mnapambania upinzani uchukue madaraka??!! What a joke?!!! Kuikwamua nchi hapa ilipo kwenda hatua bora zaidi hakuhitaji wanasia (upinzani/watawala) bali kunahitaji 'watu' wenye nia thabiti na mawazo huru nje ya misingi ya vyama, kama unategemea CHADEMA wakipewa nchi watafanya tofauti na wanayofanya CCM nakupa pole in advance
 
Deal done! Nadhani ndiyo ile pesa ya Abdul na Mom aliyosema TAL kwenye moja ya mikutano!
Anyway wakati anaondoka Sugu anaendelea kuwasha moto wa CHADEMA huko Nyanda za Kusini!
 
Wajiunge na CCM mara ngapi?
 
chadema watabaki tu G-Z wazee wote waende watakako
 

..Nini kinawafanya wahamie CCM?

..kwa maneno mengine wanashawishika na nini?

..tukiweza kukiondoa hicho wanachokifuata huko CCM tutakuwa tumemaliza upuuzi huu kwa kiwango kikubwa.
 
Kazi ya Chadema ni kuwasaidia CCM kutawala. YAANI namaanisha Chadema ni mpango wa kando wa CCM kuwadanganya wazungu.kuwa tuna mfumo wa Vyama vingi. Ni jiwe tu hakutaka kuendelea na huo mpango ili abane matumizi kwa maana ya kuwanyima ruzuku.
 
Upinzani ni Ideology mkuu sujui ni lini mtaelewa hili, Upinzani sio Political Party. Kama mnawaza hivyo mtachelewa sana kupara mabadiliko.
Wale machalii wanaompelekea moto Ruto hawana chama lakini wanafanya kazi iliyotukuka zaidi ya vyama vya siasa.
 
..Nini kinawafanya wahamie CCM?

..kwa maneno mengine wanashawishika na nini?

..tukiweza kukiondoa hicho wanachokifuata huko CCM tutakuwa tumemaliza upuuzi huu kwa kiwango kikubwa.
Huko wanatafuta vyeo, kitu ambacho hakiwezi kutibika chadema kwakuwa hawana serikali.
 
Acheni CCM waendelee kuwachukua akina Kitambi, Msigwa, Kitila,bado chadema na upinzani utaendelea kuwepo ni itikadi na falsafa na mindset- walianza akina Mtei,Shariff Hamad nk hawapo lakini upinzani unaendelea ....
 
Huko wanatafuta vyeo, kitu ambacho hakiwezi kutibika chadema kwakuwa hawana serikali.

..dawa ni kuinua mojawapo ya vyama vya upinzani ili wawe na nguvu zinazokaribiana na Ccm.
 
Siasa ni kazi na Ajira kama zingine kinachoangiwa ni maslahi tuu 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/C82M_OVMNFf/?igsh=MTRsMHY1ZDA5cWlnZw==
Dini pia ni mchongo wa.kupiga hela Kwa mbumbumbu
 
Kuna vitu vinasikitisha sana nchi hii.

Hakuna kitu kinakera kama ujinga huu wa kina Msigwa. Nimemdharau sana
Hata huyo ambae unamheshimu anaangalia maslahi,ni ujinga wako ndio unakusumbua.
 
..Nini kinawafanya wahamie CCM?

..kwa maneno mengine wanashawishika na nini?

..tukiweza kukiondoa hicho wanachokifuata huko CCM tutakuwa tumemaliza upuuzi huu kwa kiwango kikubwa.
Pesa na vyeo. Ndani ya cdm huwezi pata hivyo. Mnyika na Lema nao watafuata. Haswa Mnyika na Msigwa ni kama walichelewa kuhamia ccm, ila kwa nyakati tofauti walishafika bei kwenye utawala wa dhalimu magu.

Kwa bahati mbaya hawaiongezea ccm mvuto kwa kuhamia, bali wanawaongezea idadi ya viongozi wa upinzani waliohamia ccm. Nina hakika atapewa vipindi kwenye media mbalimbali ili aichafue cdm, kisha baada ya hapo atakaa kwa kutulia kusubiri alichoahidiwa na ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…