Sasa,mfano ukirudia maandishi yako,mbinu ya HAMAS kutumia kushinda vita na Israel iko wapi?
Kingine unaposema kwamba Israel alifanya kitendo cha uungwana kuwataka watu wahame. Unadhani kuacha kila kitu na kuondoka ni rahisi kama unavyofikilia? Haya,waote wana magari ya kusafilia? Siku moja iliyotolewa,wote walikuwa na nauli za kutumia?
Mkuu,ukimbizi usikie tu kwa watu usiombe ukukute,we chukulia poa tu.
Kikubwa iwe HAMAS au Israel wote wauaji tu.
Kama Israel angekuwa na akili,angewasaka wahusika kuliko kuua bila kuchagua. Kuuawa kwa aliyehusika na mauwaji kusingekuwa na tabu.
Kwani Israel ikishinda,wa Palestina wanaenda wapi? Na HAMAS ikishinda,wayahudi wataenda wapi? Wote si wakazi wa eneo hilo! Kikubwa wangekaa meza moja na kugawa ardhi kwa nchi mbili na zikaktambulika kimataifa. Full stop