Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Kiukweli ndo maana Safari za misafara sizitaki, ukiongozana na mtu anapepea nawe utatamani kupepea
Sahihi Mkuu, yaani unakaa unasema hivi kwanini nisifike walau speed 160km/hr ukifika speed hiyo unasema kwanini nisimalize kabisa dashboard 😜

Kuja kutahamaki watu wanaimba parapanda italia 😭
 
Tatizo sio mwendo kasi bali mwendo kasi kwenye nchi gani na barabara gani.Nchi zetu miundombinu bado ni changamoto,unakuta barabara ni highway ila ina viraka na mashimo kama chandarua uku watumiaji wengine wa barabara nao wamejiachia bila kujali chochote.
Bongo kama huna chuma kizito barabarani achana na spidi, spidi ni yawatu wazito wenye vyuma vizito
 
Aliyekuwa Dereva na mmiliki wa gari ndogo, Hamis Chaurembo (27) maarufu kama SIMBA ambaye amefariki baada ya kupata ajali mbaya huko Kibondo Kigoma amezikwa jana.

Ila kuna cha kujifunza hapa kutokana na maneno ya baadhi ya marafiki zake.

"Baadhi ya A.K.A alizopambwa nazo ni pamoja na 'Mwendo wa rocket', ndege ya ardhini, Hamisi on fire' Titanic icon' Sukari ya Warembo'

"Alikuwa akitumia dk 20 hadi 25 kutoka Kibondo hadi Kakonko, watu walimpenda kwasababu ya ucheshi wake, alikuwa hana baya yeye anawasha gari hata kama amepata abiria mmoja.

"Ahadi aliyojiahidi imetimia, katika kauli zake aliwahi kusema

"Siku nikipata ajali ni lazima niondoke na abiria wote".
Madereva wa Probox akili zao zinafurahisha sana. Tazama huyu anavyoendesha

View: https://youtu.be/Kp-IqS9N1AI?si=RJ2O3TMRBgw3xaFR
 
Kibondo - Kakonko kuna kilometers 43. Kwa probox ikitembea kwa kilometers 100 kwa saa constantly, itatumia dakika 25 plus au minus.
Kabla ya kuweka lami barabara hiyo bado iliruhusu vijana wa probox kuchezea kwenye mia na zaidi. Hivi imewekwa lami tutegemee vilio zaidi hasa Hiace na Probox za Kibondo - Kasulu.
 
Sio kweli…kutoka Kigoma mjini Kibondo unafika around saa 5 na Kakonko around 6 na nusu mchana ukiwa unaelekea Mwanza kwa basi
Ukitokea kigoma au kasulu unaingia kakonko kwanza ndio kibondo ukiwa unaelekea mwanza
 
Sio kweli…kutoka Kigoma mjini Kibondo unafika around saa 5 na Kakonko around 6 na nusu mchana ukiwa unaelekea Mwanza kwa basi
Ukitokea kigoma au kasulu unaingia kakonko kwanza ndio kibondo ukiwa unaelekea mwanz
 
Aiseee Khamis alikuwa shemeji angu duuuuh kiukweli tulikuwa tukimwambia sana juu ya mwendo ona sasa dada angu kabaki mjane ila yote kwa yote marehemu hasemwi vibaya.
 
Probox inabeba watu wangapi kwani???? Duu yani hao wote 8 walikiwa kwenye probox
Nane mbona wachache jomba? ... Siku moja nimeshuhudia watu wanapangwa, wanne mbele akiwemo dereva. Katikati wanne na nyuma kwenye boot wanne pamoja na mizigo. Na bado dereva alitaka kuongeza ... Nikashuka na kuchukua boda boda Kakonko - Kibondo kwa 20,000/=
 
Back
Top Bottom