Hamis Kigwangalla inakuwaje unashindwa kudhibiti hasira zako? Ona sasa umepatwa na janga

Hamis Kigwangalla inakuwaje unashindwa kudhibiti hasira zako? Ona sasa umepatwa na janga

c&p....DR KIGWANGALA AMPIGA RISASI MFANYAKAZI WAKE NA KUMJERUHI VIBAYA SANA


Mh, Mbunge wa Nzega HAMIS KIGWANGALA Leo 23-5-2023 anatuhumiwa kumpiga Risasi na kumjeruhi Kijana Anayefahamika kwa jina la SAID OMARY ambaye ni mfanyakazi wake na kupelekea kumjeruhi vibaya sana Miguuni na sehemu Mbalimbali za mwili wake Katika eneo la NHUNGUMALWA Kwimba Eneo ambalo Mh Hamis Kigwangala amekodi kiwanda cha Pamba(Cotton Ginnery)
Chanzo cha mgogoro huo hadi kupelekea kupigwa Risasi na Mh Kigwangala ni kutokana na Bwana Said Omary kumdai malipo yake bwana Kigwangala baada ya kuona anadaiwa Mh Kigwangala alidai yeye ndiye anamdai Fedha milioni 28 Bwana Said kufuatia hilo Bwana Said Omary aliona ni kama Anataka kudhulumiwa ndipo ukatokea ubishani mkubwa uliopelekea Mh Kigwangala kufyatua Risasi Hewani na Moja kumpiga Miguuni na Sehemu Mbalimbali za Mwili Bwana Said Omary, Baada ya kutokea hilo Said alienda Polisi kuchukua Pf 3 na hatimaye Kutibiwa majeraha yake, Polisi kituo Kikuu Cha Ngudu Ililazimika kumweka Ndani Mh Hamis Kigwangala, Taarifa Zilizoifikia NGUDU ONLINE TV Zinasema kuwa jioni ya Leo Mh Kingwangala ametolewa kwa Dhamani kwa madai kuwa ANAWAHI Bungeni Dodoma, Na Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa Zipo jitihada kubwa za kulizima jambo hili kimya kimya na JESHI LA POLISI KUPITIA KIGOGO MMOJA ALIYEPO POLISI MKOA WA MWANZA Kwa kushirikiana na OC CID KWIMBA Anaonekana kuwa kwenye Mpango huu wa Kumaliza kesi hii Ili ionekane Kijana Huyu Hajapigwa Risasi na Mh Hamis Kigwangala Kwa kubadilisha maelezo yaliyopo Na KUMBADILISHIA KESI Said Omary Ili Kumlinda Mh Hamis Kigwangala , kitu ambacho kinaonesha Waziwazi Uvunjaji wa Sheria za nchi, Baadhi ya Viongozi Katika Wilaya ya Kwimba waliohojiwa na NGUDU ONLINE TV Wakiwemo Watetezi wa Haki za Binadamu kutoka Maeneo mbalimbali Ya Mkoa wa Mwanza Wameoneshwa kusikitishwa na Kitendo cha Polisi kumwachilia Mh Kigwangala kwa haraka haraka bila kufuata taratibu nyinginezo Na wamezidi kuhoji kwa nini Watuhumiwa wengine huchukua hadi Siku 5 wakiwa Rumande bila dhamana kwa kisingizio cha Upelelezi kwa Nini huyu Aachiliwe kwa muda mfupi kupita Kiasi? Aidha Watetezi wa Haki za Binadamu Wameahidi kuendelea kufuatilia kwa Karibu Kesi hii Hasa dalili za Kijana Said Omary Kubadilishiwa Kesi na Yeye kuwekwa ndani ili kumlinda Mh Hamis Kigwangala

NGUDU ONLINE TV Ilipompigia Simu Bwana Said Omary Alikiri kweli kutokea kwa tukio hilo na AMEMUOMBA Mh Rais Kumsaidia kupata haki Yake!
Sasa mnamuita huyu mhuni mheshiniwa? Acheni utani aisee! Mbunge gani mpuuzi hivi?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Moja kati ya maajabu ni huyu jamaa kuwa Mbunge. Mimi nilifikiri tunapaswa kutanguliza watu makini mbele. Bongo ni tofauti, watu wa hovyo ndio tumetanguliza mbele
Ilishanenwa hivyo katika Biblia

Mhubiri 10:5‭-‬7 SUV
Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
 
Yaani doc, nimesikitika sana, umeshindwaje kudhibiti hasira zako hadharani?

Kwanini uwe gumzo kwa migogoro na wafanyakazi wako, hasa kwenye kuwanyima haki zao?

Haya yetu macho
Yule ni mbumbumbu sana ndio maana mgomvi mgomvi tu,na anatumia vibaya sana mamlaka akiwa nayo,shortly ni takataka and highly pompious
 
Kwenye kuwa na Akili ( Intelligent ) nakubaliana nawe 100% kwani kuna mahala niliwahi Kukutana nae na nikaligundua hilo.

Psychiatrists wajaribu kukaa nae kwani nahisi kuna linalomsibu na halijatatuliwa lakini pia mlio nae karibu mwambieni aachane na kupenda mno Waganga wa Kienyeji na ajikite Kumuamini Mwenyezi Mungu ( Allah ) pekee.

Nimesikitika sana kama kafanya hili.
Ndiye yule aliwahi kuongea bungeni kuwa Tundu Lissu ni mgonjwa wa akili kwani yeye ni Daktaru na, aliwahi kuli attend file lake pale Muhimbili. Wakati dunia inajua kuwa hajawahi kuwa na leseni ya udaktari.
Jamaa ni muendelezo wa vichwa vya hovyo vimekua vikiubuliwa na familia ya JK
 
Mbaya sana ikifikia kwenye nchi kiongozi anafanya anavyotaka, haya mambo ndio tunamkumbuka magufuli aliweza kudhibiti
 
Back
Top Bottom