Hamisa Mobeto ana mchango gani kwenye sekta ya madini? Wizara ya Madini mjitafakari sana kuelekea TMIC2024

Hamisa Mobeto ana mchango gani kwenye sekta ya madini? Wizara ya Madini mjitafakari sana kuelekea TMIC2024

Bosi wewe hujaelewa, yaani hivi vitu hata wewe unaweza jiweka yaani iko hivi kukiwa na tukio siku hizi imekuwa mtindo mtu kujitangaza kwa kuambatanisha na tukio, mfano kama wakuu wa taasisi walipoalikwa Arusha kila mmoja alikuwa anajiandika nitakuwepo, hivyo usimshambulie Hamisa
Hii mbona hajajitangaza hilo tangazo liko moja kwa moja kwenye page ya wizara husika
 
Huvaa hereni ,ni madini hayo. Ni mdau wa madini KWA namna hiyo.

Wanauchumi wana chingereza chao wanaita final consumer.


Ila kiukweli amesaidia kuupa promo huo mkutano
Wee jamaa nina uhakika ni bright sana... Kiufupi we jamaa kichwani una kitu tena sio kidogo

Umejibu simple and clear
 
Nimeona Wizara ya Madini wameandaa mkutano wa TANZANIA MINING AND INVESTMENT CONFERENCE 2024 (TMIC2024)

Wameuita USIKU WA MADINI utakuwa 20th Nov 2024 Mlimani City Mall, DSM

Hamisa naye atakuwepo, nimeshangaa sana. Hivi kweli Wizara imekosa wachimbaji wakubwa wa kati na wadogo ili waje kutoa hamasa kwenye mkutano huo!

Kuna wanawake wengi tu wanafanya kazi kule migodini ambao walitakiwa kupewa kipaumbele.

Wapo wadada na akina mama wanaowekeza kwenye madini na wanayapambania mnakuja kubeba waigizaji?

Ajabu wametuletea Hamisa acha tuone hayo madini atakayotoa.

Na ikumbukwe huu ni mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini.

Nikiwa kama mdau wa hii sekta hili jambo limenishangaza sana.

View attachment 3155006

Hili taifa linaendeshwa kishikaji sana
Kwa Wenyeji wa jiji hiyo wala sio story labda kama wewe mgeni wa juji
 
Back
Top Bottom