FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,567
- 4,683
Mimi nadhani tusubiri tumsikie mtuhumiwa akisema ya upande wake, siku zote msema pweke mshindi.Kipi hasa cha maana alichokanusha?! Kwamba hana tatizo na Zari, au?!
Kuna vitu vingine unaweza kutumia common sense ukaamini alichosema muhusika na hata kama ni cha uongo hakiwezi kuwa mbali sana na ukweli.
Kwa mfano, Diamond anafahamika sana kwa kujua ku-care! Kwahiyo hata kama hakuwa akimpatia 70K daily, still I believe alikuwa anampatia kiasi.
Hata kama hakulipa 7M kwa ajili ya operation still I believe kuna kiasi alilipa!!
Kwamba child support analipa 200K ni jambo ambalo siwezi kuwa na shaka nalo hata kidogo kwa sababu hata sisi maskini hatuwezi kushindwa kutoa kiasi kama hicho in favor of child support!
Na inawezekana kabisa hata hiyo gari alimnunulia!!!
Lakini tukitumia utetezi wa Diamond kuhusu Zari! Swali je, unataka kusema kabla ya interview ile Zari alishamwaga manyanga rasmi? I don't think so!
Kama sio, kwanini Zari alitoka povu?!
Hapo ndipo unapokuja ku-make sense utetezi wa Diamond kwamba ingawaje alishaongea na Zari, lakini hakuwahi kumwambia gharama anazotoa kwa Hamisa!
Katika hali ya kawaida, hakuna mwanaume anayehudumia nje halafu akamwambia ukweli mwanamke wake wa ndani kwamba anatoa kiasi kadhaa wa kadhaa kwa mchepuko; HAKUNA!
Na kama hakuna, basi pia kuna kila dalilia gharama zile alizotaja Diamond bila kujali kama ni za kweli au si za kweli; kwa mara ya kwanza Zari ndo alizisikia pale!!!
Sasa katika mazingira kama hayo utashangaa Zari kuja juu?! Hivi hawa wanawake si huwa wanawafanya waume zao wawe wanatoa misaada kwa ndugu wa damu kwa kujificha kabisa! Na kama mwanaume mwenyewe hajiamini, anamwambia kabisa ndugu yake kwamba "hii pesa niliyokupa shemeji/wifi yako asijue!"
Sasa ikiwa kwa ndugu tu wanawake huwa na mtimanyongo; what anaposikia zinatoka za kutosha kwenda kwa mchepuko?!
Mondi alisema amesha settle hiyo ishu na Zari na wapo cool, ila Zari si amekanusha.