Hamisi Shaban Taletale aka Babu Tale, fanya hima ujenge kwenu hii nyumba ni aibu kuu

cha muhimu usingizi unapatikana🤣, urembo wa nyumba ni mbwembwe tu
 
Nyumbani ,ni Nyumbani ata kukiwa kuzuri au kubaya ...By ....Dr Remmy...R.I.P.
 
Ni ushauri mzuri lakini hebu nasi tujiangalie.. Je yale tunayowashauri wengine sisi tukoje nayo?
 
Sisi tusio na nyumba Bongo tuna tabu sana. Wengine hawana nyumba lakini wana pesa benki. Wana gari nzuri na nyumba nzuri ya kupanga maeneo mazuri ya mji. Kwani kuna tatizo gani? Mbona watu ambao hajasoma huwa wanashabikia nyumba hivi?

Tangu niko mdogo kijijini, wasomi walipokuwa wanatangulia mbele ya haki na kuja kuzikwa kijijini, mbumbumbu wa kijijini walikuwa wanawaongea vibaya sana eti kwa sababu hawakujenga nyumba kwao!

Nimeishi nje kwenye nchi zilizoendelea, ambako watu wana pesa za kutupa, wala watu hawashobokei nyumba kiasi hiki. Watu wanaweka mapesa benki. Wakitangulia, wanaacha pesa kwa familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…