Hamisi Shaban Taletale aka Babu Tale, fanya hima ujenge kwenu hii nyumba ni aibu kuu

Hamisi Shaban Taletale aka Babu Tale, fanya hima ujenge kwenu hii nyumba ni aibu kuu

Nimekuelewa, ila kwa mtu ambaye ana uwezo wake mzuri kwanini ushindwe kujenga mjini na kijijini?

Hii ndo sababu inasababisha maendeleo pia yasienee kijijini maana watu hawaoneshi kujali umuhimu wa walipozaliwa

wengi mnaojenga kijijini, mnajenga ku maintain status ni kama pride Fulani, wala hakuna linguine linalowasukuma kufanya hivyo.. which is sad... pride wengine sio tu pride hawana bali pia sio priority....

Maendeleo kijijini tafuta kwa nini hamna.
 
Hakuna kitu kibaya kama msiba,maana msiba huwezi kumzuia mtu kuhudhuria tatizo ni pale kwenu hukupaendeleza then ikatokea ni lazima umati ukusanyike pale iwe ni wewe binafsi au vyovyote vile.

Kijijini nakotokea yupo brother mmoja aliondoka kutafuta maisha amehangaika sana nyota ikaenda kung'aa akiwa Msumbiji kwenye madini,jamaa mitandaoni anarusha picha yupo anakula maisha (though mazingira ya starehe kule hayakuwa makali sana but anavyojiweka kwa mjanja anamstukia huyu kashatusua),mara apige picha $ kazigandamiza na pistol,mara ana-drive Hummer haikuwa act ni maisha asili aliyokuwa anaishi.

Mwaka juzi jamaa akadondoka ghafla akafariki kumleta home haikuwa shida kutokana na connection aliyokuwa amejitengenezea jamaa akafikishwa kijijini,mila za kwetu huwezi kuzikwa nje ya sehemu uliyopewa na baba yako iwe ulijenga au hukujenga,zilikuja gari za maana Vogue,Hummer zilikuwa kama nne zime-park chini ya miembe hizo Land Cruisers zilikuwa kama Bajaj zinavyopaki hovyo pale Kariakoo,ila jamaa ilifyekwa majani sehemu itakayotumika kumzika akawekwa watu wakaamsha.kuendeleza makwetu kuna umuhimu mkubwa sana hata kama siyo kwa sababu nilizoorodhesha hapo juu ila ni kujitayarishia sehemu nzuri ya kupumzikia ukiwa bored kule ulipo.

Home nilijengaga nyumba ya kawaida ile ya ujana but nataka nikainue nyengine nzuri Mungu akinipa umri mrefu sitaki kuishi humu mijini maisha yangu yote ila nitakuwa miezi nane kijijini miezi minne mjini,mtu huwezi kufanya hivi kama kwenu hujajenga hata hao wasioenda kwao miaka na miaka kwao hawajajenga so aibu wanaiona pale wamekaa town miaka miwili au mitatu kisha wanarudi kijiji wanaenda tena kupishana na mama zao kwenye corridor za nyumba walizokulia huku bukta zimewatuna kwa mbele.
 
Ndio akili zenu za kimbumbumbu nilizosema. Mawazo yote kwenye nyumba kama vile mmekuwa kobe. Kobe ndiye lazima awe na nyumba ili mwili usiishiwe maji. Wewe binadamu unayezikwa na sanduku tu na shuka moja, utashupalia nyumba kiasi hicho cha nini?

Hata kusoma Kiswahili haujui. Nimeandika mtu ana nyumba nzuri, anakaa nyumba ya kupanga nzuri kwenye eneo zuri la mji (Dar - Masaki, Oysterbay nk). Halafu unaniponda huku unarudia kile kile nichokisema. Una akili kweli? Siyo ujinga huo. Halafu wajinga wenzio wamesoma halafu wakakupa "Thanks"!
Sasa una hela alafu unaishi kwenye nyumba isiyoendana na hela uliyonayo hiyo ni akili ujenge au upangishe inatakiwa ukae kwenye nyumba nzuri
 
wengi mnaojenga kijijini,mnajenga ku maintain status ni kama pride Fulani,wala hakuna linguine linalowasukuma kufanya hivyo..which is sad...pride wengine sio tu pride hawana bali pia sio priority....

Maendeleo kijijini tafuta kwa nini hamna.
Siyo sahihi,hatujengi kulinda au kujitafutia hadhi ila pale ni nyumbani nimezaliwa nimekulia pale lazima nitatakiwa kupatembelea mara kwa mara sasa nitalala wapi nikiwa pale?au nikitaka kupumzika nikapumzike wapi?...hotel?

Afadhali post imetumwa na mwanamke angekuwa mwanaume ningemtukana.
 
Aibu kwa kweli halafu huwa wanajiita matajiri,hata kuweka curtains tu kumemshinda ?Kashindwa kuendeleza kwao ndo huyu anataka ubunge ????Au anataka ubunge ili anufaike ?Aibu hii.Maisha ya social media bwana........
Ukweli unauma
Huu ndio uhalisia
Wa aina hii wengiii
 
Sisi tusio na nyumba Bongo tuna tabu sana. Wengine hawana nyumba lakini wana pesa benki. Wana gari nzuri na nyumba nzuri ya kupanga maeneo mazuri ya mji. Kwani kuna tatizo gani? Mbona watu ambao hajasoma huwa wanashabikia nyumba hivi? Tangu niko mdogo kijijini, wasomi walipokuwa wanatangulia mbele ya haki na kuja kuzikwa kijijini, mbumbumbu wa kijijini walikuwa wanawaongea vibaya sana eti kwa sababu hawakujenga nyumba kwao! Nimeishi nje kwenye nchi zilizoendelea, ambako watu wana pesa za kutupa, wala watu hawashobokei nyumba kiasi hiki. Watu wanaweka mapesa benki. Wakitangulia, wanaacha pesa kwa familia.
Preach it....
 
Siyo sahihi,hatujengi kulinda au kujitafutia hadhi ila pale ni nyumbani nimezaliwa nimekulia pale lazima nitatakiwa kupatembelea mara kwa mara sasa nitalala wapi nikiwa pale?au nikitaka kupumzika nikapumzike wapi?...hotel?

Afadhali post imetumwa na mwanamke angekuwa mwanaume ningemtukana.

mnhhhh umezaliwa, umekulia pale..leo hujui pa kupumzikia?? khaa
 
Back
Top Bottom