Sisi tusio na nyumba Bongo tuna tabu sana. Wengine hawana nyumba lakini wana pesa benki. Wana gari nzuri na nyumba nzuri ya kupanga maeneo mazuri ya mji. Kwani kuna tatizo gani? Mbona watu ambao hajasoma huwa wanashabikia nyumba hivi? Tangu niko mdogo kijijini, wasomi walipokuwa wanatangulia mbele ya haki na kuja kuzikwa kijijini, mbumbumbu wa kijijini walikuwa wanawaongea vibaya sana eti kwa sababu hawakujenga nyumba kwao! Nimeishi nje kwenye nchi zilizoendelea, ambako watu wana pesa za kutupa, wala watu hawashobokei nyumba kiasi hiki. Watu wanaweka mapesa benki. Wakitangulia, wanaacha pesa kwa familia.