Hamisi Taletale na PhD ya USD 2,500

Hamisi Taletale na PhD ya USD 2,500

Watanzania tunahusudu sana hizi labels haijalishi tuwe tumesoma au vinginevyo. Profesa ukisahau kumuita hivyo unaweza kujikuta pabaya. Hata nnje ya chuo ni prof. Kaburini ni prof. Dr. nae ni dr usisahau. Vyuo vyetu aibu kabisa vinashindana kugawa degree za heshima kila raisi wanampa halafu fikiria cha ziada kilichofanywa na mtunukiwa ni kipi. Unaona epa, escrow etc.
Ukienda afya kila anae vaa koti jeupe ni dokta. Ugonjwa ukaenea sasa tuna Eng. Masiya, CPA Fedha etc. Tumegundua uwepo wa phd mchongo za kununua za vyuo visivyo eleweka, waheshimiwa ndio kimbilio lao. Kwa ujinga huu nani atasimamia elimu yetu? Hivi unapo mpa raisi phd au drsc baada ya kukulia kiti kwa mwaka na nusu tu unapeleka ujumbe gani? Tuko serious kweli? Kiufupi tunatukuza sana titles na tuko tayari kuzipata kwa njia yeyote hata kujipachika au kununua. Prof. Dr. Masiya
 
Back
Top Bottom