bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bwana Hamphrey Pole Pole amevunja ukimya na kusema Katiba ni ya Wananchi na si ya wanasiasa. Hebu mwangalie alivyotamka mwenyewe,"" Katiba hii siyo ya wanasiasa ni ya wananchi wenyewe, lakini cha kushangaza hapa ni wanasiasa wanavyochukua nafasi kubwa ya kuuteka mchakato huu na hii yote wanataka wapate nafasi ya kulinda masilahi yao na kuendelea kututawala watakavyo, hivyo ndugu zangu wa Mbeya na Watanzania wote chukueni hatua." Asante Bwana Pole Pole kwa kutuelimisha kwa maana wengi tulipotoshwa na kuambi;wa kuwa Katiba ni ya fulani na fulani mara ni ya chama fulani. Sasa ninyi mlioshiriki kuitunga akiwemo comredi Mbatia mnapotwambia hivyo mnatusaidia sana katika kuelewa Katiba Inayopendekezwa. Endelea kutueleza na mengine zaidi.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi