Hamtaki kujiingiza kwenye Siasa basi acheni waliojiingiza huko wale na Watoto wao

Umeongea Ukweli siasa Ni hatari sana

Acha Ccm na CHADEMA wale mema yao

Mfano lissu wanae wote wanasoma Marekani

Mbowe ndo hak
 
Kweli kabisa kuna familia hazikosagi kwenye teuzi au ajira sehemu nyeti mfano kama familia ya Nyerere, Karume, Mwinyi, Mkapa, Jakaya, Magufuli, Mama Samia, Mrema, Sumaye, Sokoine, Lowasa, Makamba, Mnauye, Kinana, Kingunge n.k.
Tupambane aisee
 
Mwl Nyerere alionyesha wazi kutopenda Mambo za kurithisha wanafamia wake Leo tunaona akina madaraka Ni Watu wa kawaida Kabisa
unadhani mwalimu asingeweza kuiweka nchi hii mfukoni mwake na kizazi chake kitawale Hadi Leo Kama sio dhana ya democracy ili mtawala mwalimu ni nini?

Unataka kusema hakuna watoto au wajukuu wa Nyerere kwenye system?

Nyerere hakupigania demokrasia ya nchi isipokuwa alipigania Uhuru wa nchi hii. Tofautisha hayo mambo mawili Mkuu.

Nyerere na demokrasia ni vitu viwili tofauti Kabisa. Yaani kuhusu mambo ya demokrasia huwezi mtaja The Legend Julius Nyerere.
Mission yake haikuwa hiyo. Na alikuwa na sababu ya muhimu kutoishabikia demokrasia.
 
Viongozi wengi wa Sasa wamejawa na ubinafsi wa familia Zao
Refer familia ya mwl.Nyerere faninisha na sasa

Hakuna Binadamu asiye mbinafsi Mkuu😂😂
Wewe ndio unataka kuleta jambo jipya.
Ubinadamu ni Ubinafsi.

Unapigania maisha yako,
Unapigania Mkeo na watoto wako,
Unapigania nchi yako.
Huo ndio ubinafsi wenyewe.
 
Kweli kabisa kuna familia hazikosagi kwenye teuzi au ajira sehemu nyeti mfano kama familia ya Nyerere, Karume, Mwinyi, Mkapa, Jakaya, Magufuli, Mama Samia, Mrema, Sumaye, Sokoine, Lowasa, Makamba, Mnauye, Kinana, Kingunge n.k.
Tupambane aisee

Kila mtu apambane na upande wake.
Mbona kuna sekta nyingi,
Kuna muziki,
Mpira,
Dini,
Biashara
Kilimo
Uvuvi
Uwakala n.k

Kila mtu anajenga misingi Kwa kile anachokifanya.
Tatizo linakuja pale mtu mmoja anapotaka kubomoa msingi wa mtu mwingine aliouunda Kwa miaka nenda Rudi unategemea nini kitatokea.

Muangalie Diamond Platinum alafu aje mtu atake kumuangusha unategemea nini hapo Mkuu?
 
"No sweet without sweat" ,"Asiye fanyakazi asile"Bible

Siku zote waoga hubaki duniani kuonesha makaburi ya mashujaa huimba sifa tele kwa watu walio jitoa kwa jasho na damu kupigania vitu muhimu,sababu ya uoga wao hushindwa hata kupigania haki zao wenyewe bali hutegemea mtu,watu au kundi fulani lifanye hivyo kwa niaba yao huu Ni ujinga uliona wapi mtu ana vuna sehemu ambayo haja panda ? Kanuni ya msingi ni Ile Ile "utakula uliko peleka mboga" hukujitoa kupigania Jambo kaa kimya ukiona walio jitoa wanakula jasho la sadaka zao.

Watu wanajitoa kupigana lengo kuu ni kutafuta nguvu sababu kuu ni moja nguvu ndio haki maana mwenye nguvu ndio anaye amua kipi ni haki na kipi sio haki hivyo aliye jitoa lazima ajipe haki yake Kwanza yeye kwa sadaka zake.

Umeelezea vizuri Sana Kwa ufupi.
 
Unataka kusema hakuna watoto au wajukuu wa Nyerere kwenye system?

Nyerere hakupigania demokrasia ya nchi isipokuwa alipigania Uhuru wa nchi hii. Tofautisha hayo mambo mawili Mkuu.

Nyerere na demokrasia ni vitu viwili tofauti Kabisa. Yaani kuhusu mambo ya demokrasia huwezi mtaja The Legend Julius Nyerere.
Mission yake haikuwa hiyo. Na alikuwa na sababu ya muhimu kutoishabikia demokrasia.
Lkn ndiye mtu kinara kukubali multi party system na Hiyo Ni principe ya democracy ingawa ilikataliwa lkn aliikubali ianzishwe huyo ndiye Mwl. Nyerere
ukubali tu kuwa uanzishwaji wa democracy kwetu ni upuuzi marakumi kingship ingeendelea kuliko haya mazingaombwe
 
Hakuna Binadamu asiye mbinafsi Mkuu😂😂
Wewe ndio unataka kuleta jambo jipya.
Ubinadamu ni Ubinafsi.

Unapigania maisha yako,
Unapigania Mkeo na watoto wako,
Unapigania nchi yako.
Huo ndio ubinafsi wenyewe.
Ubinafsi nao una viwango
Una level ukizidi Sana unabidilika jina
 
Lkn ndiye mtu kinara kukubali multi party system na Hiyo Ni principe ya democracy ingawa ilikataliwa lkn aliikubali ianzishwe huyo ndiye Mwl. Nyerere
ukubali tu kuwa uanzishwaji wa democracy kwetu ni upuuzi marakumi kingship ingeendelea kuliko haya mazingaombwe

Maji yalikuwa kidevuni.
Mtu ametoka madarakani ndio awe kinara?
 
Taikon toa suluhisho la Kupata nafuu ya maisha vitu vimepanda Sana bei
 
HAMTAKI KUJIINGIZA KWENYE SIASA BASI ACHENI WALIOJIINGIZA WALE WAO NA WATOTO WAO

Na, Robert Heriel

Waacheni warithishane madaraka, waacheni wapeane vyeo. Mlitaka wafanyaje? Wao ni wanasiasa na watawala mlitaka wawape watoto wao nini kama sio mambo hayo.

Haiwezekani watu wahangaike na siasa kutwa kuchwa, miaka nenda Rudi ninyi mnawatazama tuu. Wengine Baba zao wamekufa, wengine wamefanywa vilema, wengine walionja joto la jiwe, alafu wakifanikiwa na kuanza Kula matunda Yao mnaanza kupiga makelele, come on motherfantashiru. Tuweni serious kidogo.

Hivi Kwa mfano mtu Kama Tundu Lisu, au kina mbowe, au kina Mdude Chadema na kambi Yao. Wachukue nchi alafu wakianza Kula matunda ya jasho lao na kuwarithisha watoto wao Madaraka au vyeo watokee watu wanapiga kelele kuwa wanajipendelea. Mlitaka wafanyaje?

Wakati wakipigana mliwaachia au mlikuwa nyumanyuma Kwa Hofu au wengine hamkuwa upande wao. Leo wamepata mnajifaraguza Kama ajuza asiye na tumaini. Pumbavu!

Kama unataka Madaraka au utawala ingia kwenye Siasa. Utakula vya Siasani, utawapa watoto matunda ya Siasa.
Lakini kama utajiingiza kwenye biashara utakula vya kwenye biashara na kuwarithisha watoto wako mambo ya biashara.

Kuna watu wanapenda vitu vya burebure.
Wengine watoe jasho alafu Yao Yale tuu. Upuuzi tuu!

Wana-CCM wataendelea kurithishana matunda ya Siasa Kwa sababu ndio haki Yao. Hakuna haja ya kulaumiana hapa.

Wakati unawaza Kwa nini viongozi wa nchi wanarithishana Madaraka na utawala jiulize Baba yako alikuwa anafanya nini hapo Kabla, isijekuwa Baba au Babu yako ndio Wale wenzao walipokuwa wakiitisha maandamano kupigania maslahi ya nchi au chama cha Siasa wao walikuwa nyumanyuma kama Mfuko wa suruali ya kabwela.
Jiulize hao Watoto wa viongozi wanaopewa vyeo na kurithishwa Madaraka Baba au Babu zao walifanya nini.

Hata hao CHADEMA au ACT au chama chochote kitakachoanzishwa watakaopigania Dola wakafanikiwa kupata hiyo Dola elewa watakaokula Mema ya nchi ni Wale wa Kule juu tuu.

Alafu mwisho ujiulize wewe unayohaki hiyo Kwa misingi ipi?
Umefanya nini upewe Cheo au Madaraka.
Sio utake kuvuna mahali usipopanda.

Kwenye Siasa kuna mambo hatari mno.
Kuna kupoteza maisha,
Kuna kujeruhiwa na kufanywa kilema,
Kuna kuwekwa Jela,
Kuna kufilisiwa,
Kuna kuvurugiwa familia,
Kuna kubakwa
Kuna kuharibiwa jina,
Sasa wewe upewe Cheo au Madaraka bila kutoa kafara fulani, uliona wapi mambo Kama hayo ndugu yangu.

Hata Daudi kabla hajawa Mfalme Ali-risk maisha yake Kwa Goliath, yaani ilikuwa Do or Die. Yaani pata potea.
Daudi alishanusurika mara kadhaa kuuawa na Mfalme Sauli, unafikiri Mpaka Daudi anakuwa Mfalme alipewa burebure kama pesa ahongwavyo Demu.
Hivyo Suleiman kurithishwa ufalme ni kutokana na jasho la Baba yake Daudi,

Ninachotaka kusema ni kuwa, hakuna mambo ya burebure hapa, Kama ulitaka mambo ya burebure muombe Mungu uzaliwe wakati mwingine mwanamke, tena hata ungezaliwa mwanamke lazima kuna mambo ulipie ndipo uyapate.

Wanasiasa, viongozi wa nchi, watawala endeleeni kula nchi kadiri muwezavyo, rithishane peaneni vyeo na Madaraka muwezavyo Hilo ndio Fungu Lenu. Msione haya Kwa kufanya hivyo. Ni Haki yenu. Hiyo ni halali yenu.
Kama kuna mtu anaona sio halali basi aingie kwenye Ligi au ringi na ninyi akishinda Fresh asiposhinda basi aache lawama.

Kila kazi inanamna yake ya kuifanya. Hivyo ndivyo hata kwenye Siasa zina namna yake.

Katika ngazi ya familia, unakuta Kijana wakati ana- hustle kutafuta maisha mazuri ndugu na marafiki wanakuwa mbali naye. Lakini akishapata tuu kelele ndio zinaanza,
Ooh! Anatumia pesa vibaya,
Anavaa nguo za gharama alafu hasaidii ndugu zake,
Ananunua magari na majumba makubwa wakati ndugu zake ni choka mbaya,
Anasomesha watoto wake shule za gharama ilhali watoto wa ndugu zake wanashindwa kulipa Ada za Shule za bei nafuu.
Oooh! Anampendelea mkewe alafu site ndugu zake ametusahau.
Hivi hiyo ni Akili Kweli. Acheni uzombi!

Ukitaka kitu kizuri fanya mwenyewe, kitafute mwenyewe sio usubiri wengine wakutafutie au wakutanyie. Huo ni upuuzi.

Au unakuta mtu kuanzisha Kampuni yake anaajiri ndugu zake au kabila lake alafu unasikia wapuuzi wanapiga kelele oooh! Wanaukabila, oooh! Wanaubaguzi! Oooh! Hivi ninyi Mbuzi meee mtakuwa na akili Lini?
Kwa nini nanyi msianzishe Kampuni au biashara zenu ili mfanye kama mnavyopenda?
Mnachojua ni kupangia watu chakufanya huku mkishindwa kujipangia wenyewe chakufanya. Acheni upuuzi.

Yaani mtu aache kuajiri ndugu yake akuajiri wewe ili asionekane ati ni mkabila au mbaguzi, labda awe hamnazo. Mambo ya hivyo wanafanyaga watu wajinga wasiojielewa, wanaopenda sifa za kijinga.

Ninachotaka kusema ni kuwa; Kula mtu awajibike Kwa kile anachokitaka katika maisha yake. Ukiona changamoto pambana sio uanze kulalamika
Kanuni kuu inasema; Usitamani Mali ya jirani yako.
Kumaanisha usiwe na kijicho, wivu mbaya.
Kama wanarithishana nawe fanya kazi upate cha kurithisha watoto wako. Hakuna atakayekuonea wivu.

Kama unapenda Madaraka au utawala kanuni za kiulimwengu zipo wazi Kabisa. Weka mikakati, pambana kufa na kupona upate hayo Madaraka.
Sio umuombe mwenye Madaraka au utawala akupe Madaraka au utawala wake. Tumia hata akili, Hilo Jambo haliwezekaniki.
Usituletee mambo ya umama hapa.
Na lazima ujue kuwa kwenye mapambano yoyote hasa ya Kisiasa lolote linaweza kutokea. Hivyo ujipange haswa sio ujipange kulialia kama Mbuzi Bali jipange haswa

Taikon nimemaliza mwenye swali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
🤔🤔🤔 Mmmh mhhh
 
Sasa si ungeita kikao cha kisiasa utolee watu hii hotuba kuliko kutufokea humu?

Suluhu ni maisha yazidi kuwa magumu mara kumi ili akili za watu ziamke.
Hali hii ndio njia sahihi Kabisa ya kukomboa watu
Kipato Mkuu Kama hakitoshi kua-Afford tunafanyaje?

Wewe ni mwanafalsafa andika mbinu mbadala
 
Aliyetoa kingi ndiye hula kingi.
Hata kwenye uchumi iko hivyo.

Wenzako wawe Front watoe mpaka damu alafu mlingane?
Uzuri Ni kuwa katiba zipo Kuna muda wakitaka kupenyezana Ina kuwa ngumu angalia kule kwa M7 na mwanae wanavyohangaika
Katiba katiba katiba tutafute katiba
 
Kwa mfano huko Kwa mu7 hivi wanategemea nini kama sio familia ya mu7 na Wale wote waliomsaidia mu7 kuingia nadarakani Kula vyeo.

Katiba nayo kuipata sio lelemama😀😀
 
Tulijiingiza huko kwa moyo wa kizalendo wa kutumika.
Tukapigwa cha mbavu.
Sasa ni bora tu 'kupaki basi' kusubiri msimu wa mvua uanze nikalime maharage kwenye ka shamba alikoacha babu huko Karagwe!
Viongozi wa chama walituhamasisha, 'vijana mjitokeze kugombea'. Ukifika kule unakuta fomu inauzwa milioni moja. Gharama za kutoka mkoani kufuatilia fomu Tsh laki mbili.
Wewe mtt wa mkulima uchome mil 1.2 kirahisi hivi! Si bora ukanunue matofali!
 
Back
Top Bottom