Hamtaki kujiingiza kwenye Siasa basi acheni waliojiingiza huko wale na Watoto wao

Hamtaki kujiingiza kwenye Siasa basi acheni waliojiingiza huko wale na Watoto wao

Kipato Mkuu Kama hakitoshi kua-Afford tunafanyaje?


Wewe ni mwanafalsafa andika mbinu mbadala

Mbinu zipo nyingi Sana
Ila mbinu za kitaifa ni hiyo ya kuleta maisha magumu Kwa nchi ili kuamsha akili zao

Katika individual level,
Mbinu ni kuhifadhi chakula kingi na Kupunguza bajeti zisizo za lazima.

Kutumia like kinachosumbua wengine kujikusanyia faida.
Mfano; watu wanashindwa ya Ajira.
Wewe usitafute Ajira Ila wape wewe Ajira Kwa level yako.
Watu wanatafuta chakula, wape wewe chakula, Kwa level yako. Yaani wauzie.

Usiwe sehemu ya kundi kubwa, yaani sehemu ya wahitaji Bali jitahidi uwe sehemu ya kutafuta Suluhu la waliowengi.

Watu wanamtafuta Mungu au Mganga, waonyeshe Mungu alipo au kuwa mganga au waonyeshe mganga. Piga Pesa.

Usiwe sehemu ya watafutaji, kuwa sehemu ya kile kinachotafutwa.
Hiyo ndio mbinu popote uwapo.
Usijesema sikukuambia.

Usiwe sehemu ya Wanaolalamika, kuwa sehemu ya walalamikiwa.
 
Sijapotosha kitu hapo MKUU.

Ukiona nchi Fulani kuna kundi Fulani linakula zaidi ya kundi jingine lazima ujiulize swali Kwa nini iwe hivyo.
Ninachoandika ni kile nilichokifanyia tathmini na haya ninayoandika ni matokeo tuu ya kile nilichokiona.

Nataka nikuambie, nchi hii na zingine za Afrika haziendelei Kwa sababu kuna kutegeana miongoni mwa watu katika kuikomboa Nchi.

Haiwezekani wategaji walingane Sawa na waliokuwa mstari wa mbele Hilo haliwezekaniki.

Hata Waisrael waliokuwa wanakula Mema ya nchi ni WALAWI kutokana na kuwa Waliokuwa Fronti kukomboa Waisrael kutoka Misri utumwani ni Musa na Haruni ambao ni kabila la Lawi.

Kama watu wanataka wale Mema ya nchi lazima wawe mstari wa mbele kuikomboa nchi.
Kwa Mali zao
Kwa jasho Lao
Kwa damu zao
Kwa akili Yao
Kwa karama zao
Kwa vipaji vyao.

Haiwezekani wengine wakiendelea kukomboa nchi wakiwa mstari wa mbele alafu kuna wengine wanakuwa nyumanyuma kanakwamba sio kundi moja linaloelekea sehemu moja.
Wanakuwa sehemu ya kutoa lawama na changamoto za ndani ya nchi.
Nimekuelewa sana. Wakati Mbowe yuko rumande kwenye kesi ya ugaidi, wana CDM walipata forum kubwa sana ya kuongea. Freeman Mbowe aliotoka na kwenda Ikulu wakanuna mpaka leo.

Ukiwaambia basi na nyinyi mlianzishe vuguvugu la mikutano kama Mbowe hawataki
 
HAMTAKI KUJIINGIZA KWENYE SIASA BASI ACHENI WALIOJIINGIZA WALE WAO NA WATOTO WAO

Na, Robert Heriel

Waacheni warithishane madaraka, waacheni wapeane vyeo. Mlitaka wafanyaje? Wao ni wanasiasa na watawala mlitaka wawape watoto wao nini kama sio mambo hayo.

Haiwezekani watu wahangaike na siasa kutwa kuchwa, miaka nenda Rudi ninyi mnawatazama tuu. Wengine Baba zao wamekufa, wengine wamefanywa vilema, wengine walionja joto la jiwe, alafu wakifanikiwa na kuanza Kula matunda Yao mnaanza kupiga makelele, come on motherfantashiru. Tuweni serious kidogo.

Hivi Kwa mfano mtu Kama Tundu Lisu, au kina mbowe, au kina Mdude Chadema na kambi Yao. Wachukue nchi alafu wakianza Kula matunda ya jasho lao na kuwarithisha watoto wao Madaraka au vyeo watokee watu wanapiga kelele kuwa wanajipendelea. Mlitaka wafanyaje?

Wakati wakipigana mliwaachia au mlikuwa nyumanyuma Kwa Hofu au wengine hamkuwa upande wao. Leo wamepata mnajifaraguza Kama ajuza asiye na tumaini. Pumbavu!

Kama unataka Madaraka au utawala ingia kwenye Siasa. Utakula vya Siasani, utawapa watoto matunda ya Siasa.
Lakini kama utajiingiza kwenye biashara utakula vya kwenye biashara na kuwarithisha watoto wako mambo ya biashara.

Kuna watu wanapenda vitu vya burebure.
Wengine watoe jasho alafu Yao Yale tuu. Upuuzi tuu!

Wana-CCM wataendelea kurithishana matunda ya Siasa Kwa sababu ndio haki Yao. Hakuna haja ya kulaumiana hapa.

Wakati unawaza Kwa nini viongozi wa nchi wanarithishana Madaraka na utawala jiulize Baba yako alikuwa anafanya nini hapo Kabla, isijekuwa Baba au Babu yako ndio Wale wenzao walipokuwa wakiitisha maandamano kupigania maslahi ya nchi au chama cha Siasa wao walikuwa nyumanyuma kama Mfuko wa suruali ya kabwela.
Jiulize hao Watoto wa viongozi wanaopewa vyeo na kurithishwa Madaraka Baba au Babu zao walifanya nini.

Hata hao CHADEMA au ACT au chama chochote kitakachoanzishwa watakaopigania Dola wakafanikiwa kupata hiyo Dola elewa watakaokula Mema ya nchi ni Wale wa Kule juu tuu.

Alafu mwisho ujiulize wewe unayohaki hiyo Kwa misingi ipi?
Umefanya nini upewe Cheo au Madaraka.
Sio utake kuvuna mahali usipopanda.

Kwenye Siasa kuna mambo hatari mno.
Kuna kupoteza maisha,
Kuna kujeruhiwa na kufanywa kilema,
Kuna kuwekwa Jela,
Kuna kufilisiwa,
Kuna kuvurugiwa familia,
Kuna kubakwa
Kuna kuharibiwa jina,
Sasa wewe upewe Cheo au Madaraka bila kutoa kafara fulani, uliona wapi mambo Kama hayo ndugu yangu.

Hata Daudi kabla hajawa Mfalme Ali-risk maisha yake Kwa Goliath, yaani ilikuwa Do or Die. Yaani pata potea.
Daudi alishanusurika mara kadhaa kuuawa na Mfalme Sauli, unafikiri Mpaka Daudi anakuwa Mfalme alipewa burebure kama pesa ahongwavyo Demu.
Hivyo Suleiman kurithishwa ufalme ni kutokana na jasho la Baba yake Daudi,

Ninachotaka kusema ni kuwa, hakuna mambo ya burebure hapa, Kama ulitaka mambo ya burebure muombe Mungu uzaliwe wakati mwingine mwanamke, tena hata ungezaliwa mwanamke lazima kuna mambo ulipie ndipo uyapate.

Wanasiasa, viongozi wa nchi, watawala endeleeni kula nchi kadiri muwezavyo, rithishane peaneni vyeo na Madaraka muwezavyo Hilo ndio Fungu Lenu. Msione haya Kwa kufanya hivyo. Ni Haki yenu. Hiyo ni halali yenu.
Kama kuna mtu anaona sio halali basi aingie kwenye Ligi au ringi na ninyi akishinda Fresh asiposhinda basi aache lawama.

Kila kazi inanamna yake ya kuifanya. Hivyo ndivyo hata kwenye Siasa zina namna yake.

Katika ngazi ya familia, unakuta Kijana wakati ana- hustle kutafuta maisha mazuri ndugu na marafiki wanakuwa mbali naye. Lakini akishapata tuu kelele ndio zinaanza,
Ooh! Anatumia pesa vibaya,
Anavaa nguo za gharama alafu hasaidii ndugu zake,
Ananunua magari na majumba makubwa wakati ndugu zake ni choka mbaya,
Anasomesha watoto wake shule za gharama ilhali watoto wa ndugu zake wanashindwa kulipa Ada za Shule za bei nafuu.
Oooh! Anampendelea mkewe alafu site ndugu zake ametusahau.
Hivi hiyo ni Akili Kweli. Acheni uzombi!

Ukitaka kitu kizuri fanya mwenyewe, kitafute mwenyewe sio usubiri wengine wakutafutie au wakutanyie. Huo ni upuuzi.

Au unakuta mtu kuanzisha Kampuni yake anaajiri ndugu zake au kabila lake alafu unasikia wapuuzi wanapiga kelele oooh! Wanaukabila, oooh! Wanaubaguzi! Oooh! Hivi ninyi Mbuzi meee mtakuwa na akili Lini?
Kwa nini nanyi msianzishe Kampuni au biashara zenu ili mfanye kama mnavyopenda?
Mnachojua ni kupangia watu chakufanya huku mkishindwa kujipangia wenyewe chakufanya. Acheni upuuzi.

Yaani mtu aache kuajiri ndugu yake akuajiri wewe ili asionekane ati ni mkabila au mbaguzi, labda awe hamnazo. Mambo ya hivyo wanafanyaga watu wajinga wasiojielewa, wanaopenda sifa za kijinga.

Ninachotaka kusema ni kuwa; Kula mtu awajibike Kwa kile anachokitaka katika maisha yake. Ukiona changamoto pambana sio uanze kulalamika
Kanuni kuu inasema; Usitamani Mali ya jirani yako.
Kumaanisha usiwe na kijicho, wivu mbaya.
Kama wanarithishana nawe fanya kazi upate cha kurithisha watoto wako. Hakuna atakayekuonea wivu.

Kama unapenda Madaraka au utawala kanuni za kiulimwengu zipo wazi Kabisa. Weka mikakati, pambana kufa na kupona upate hayo Madaraka.
Sio umuombe mwenye Madaraka au utawala akupe Madaraka au utawala wake. Tumia hata akili, Hilo Jambo haliwezekaniki.
Usituletee mambo ya umama hapa.
Na lazima ujue kuwa kwenye mapambano yoyote hasa ya Kisiasa lolote linaweza kutokea. Hivyo ujipange haswa sio ujipange kulialia kama Mbuzi Bali jipange haswa

Taikon nimemaliza mwenye swali anaweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sindano ya moto hii.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nimekuelewa sana. Wakati Mbowe yuko rumande kwenye kesi ya ugaidi, wana CDM walipata forum kubwa sana ya kuongea. Freeman Mbowe aliotoka na kwenda Ikulu wakanuna mpaka leo.

Ukiwaambia basi na nyinyi mlianzishe vuguvugu la mikutano kama Mbowe hawataki

Thubutu!
 
Hata kama tutajiingiza wote huko, bado wataendelea kula wao na watoto wao, kwani hata sasa sio wote wanaokula kwasababu wako kwenye siasa.

Halafu mifano uliyoitoa haiendani na mada yako, kampuni inaweza kuwa ni mali binafsi ya mtu, lakini chama cha siasa, ni cha wote, japo kwenye kula ndio wanakula wachache.
Na ukijiingiza huko na wakakuona wewe ni tishio kwa nafasi zao ujue utapigwa rungu la utosi kimya kimya !! Kwanza wote hawa tunaowaona wanarithishana hawajawahi kupata suluba zozote zile kwenye siasa zaidi ya kubebwa bebwa tu !! Wote wenye kupata suluba au wengi wao huishia kapuni ! Mfano bibi titi na akina Sykes na wengine wengi tu ! Akina Mtikila akina Lisu akina lipumba akina Maalim Seif na wengine wengi tu!! Niambie hao ambao wanakula na kurithishana walizipata suluba wapi na kwa namna gani. !!
 
Well said mkuu ROBERT HERIEL

Lakini hii makala yako kitaalamu tunaweza kuiita Involuntary Autosuggestion

Why?
Because it seems to me like a silent fear thought emotionalized and subjectified.

Your fear is taken as a request, then proceed to manifested and brings them into your experience.

What do you experience up to now?

Just relax and close your eyes. Now open your eyes.

Kwa maana nyingine ulichokiandika inaonekana ni kiasi gani umetawaliwa na kitu kingine ambacho kitaalamu tunaweza kukiita suggestive amnesia

Why?

Because it's within your psychological circle and you can't take it out of it.

The real cause of all this is negative and destructive thinking.

You're the only thinker in your own universe, but don't forget that we live in different universe.

Don't you know?
People programmed their mind to engineer their own living and death.

Copy that?

If the mind can be programmed to engineer death, it also be programmed to enhance life.

What do I mean?

I mean in this life we have physical survival which has only 3 components:

#1. Air
#2. Water
#3. Food

A person can go without air for only moments.

A person can go without water for a few days.

A person can go without food for a month or so.

Do you wonder why all this and where does it come from?

If starving person is given choice on three things, food, water and sex, what do you thing he will choose first?

A starving person will opt for food and water before sex, do you know why?

Disregarding genetics, at birth you were similar to any other newborn in your ability to perceive and respond to reality and in capability to develop your God-given ability.

You still ask why?

The quality of your life is your own making and nobody else.

You can help stabilize, advise and direct younger generation.

You can give the benefits of your knowledge, your experience and your wisdom.

We live in accordance to our survival in area of life in descending order of the following:

#1. Spiritual (love) survival
#2. Identify/Analytics/Mind survival
#3. Physical survival
#4. Territorial survival
#5. Sexual survival

Think good and good will follow.

Fikiria tena mkuu, yoyote anaweza akawa yeyote na anaweza akakaa popote kwenye nyadhifa yoyote haijarishi amekuliwa wapi au ametokea wapi, it doesn't matter how and where.

Niweke kalamu chini... Nitarudia
 
Back
Top Bottom