Hamza Johari: Kikatiba, nafasi ya Nchimbi ilikoma baada ya kuvuliwa uanachama CCM

Hamza Johari: Kikatiba, nafasi ya Nchimbi ilikoma baada ya kuvuliwa uanachama CCM

81704793-415A-4959-BF80-8DE839474BEC.jpeg

Nchi mnaiendesha kama wauza machungwa …. Matakooo yenu
 
sijaelewa kwa hiyo tusema labda raisi samia akivuliwa uanachama leo hii na uraisi wake unakoma? sidhani nielewavyo hiyo ni katiba ya south afrika ndiyo iko hivyo lkn wao hawachagui mtu bali wanachagua chama i.e siku ya uchaguzi hakuna jina la mtu bali chama halafu chama ndiyo kinachagua mtu kuwa raisi hivyo chama kinaweza pia kumuondoa raisi na kuweka mwingine hata katikati ya muhula kabla ya uchaguzi kuu na bila ya haja ya kuitisha uchaguzi lkn tanzagiza hatuchagui chama bali mtu.

mimi siyo mwanasheria lkn sidhani kama ni sahihi kumfuta uanachama na umakamu unakoma kwani makamu ni raisi in waiting hivyo kwa logic yangu hawezi kufukuzwa tu kienyeji, so raisi samia akifa sasa hivi au akapata tatizo kubwa la kushindwa kuendelea kuwa raisi kwa mfano nani atakuwa raisi? ...
 
Kwani ameapishwa?
Na mbona niliona sehemu tena imeandikwa
Angefutwa uanachama kabla ya kujiudhulu, ndio angepoteza sifa za kuwa Makamu, ila Yeye aliwawahi, akajiuzulu kabla hajafutwa,,, hivyo ni makamu hadi tar 4 kama alivyoandika kwenye barua.
Kwa maelezo ya AG leo bungeni baada ya kufukuzwa uanachama ndio kilikuwa kikoma cha umakamu wa Rais wa Nchimbi. Hiyo ndiyo CCM.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoa ufafanuzi kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais​

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ametoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu lini nafasi ya Makamu wa Rais inakuwa wazi, akisema tarehe rasmi ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais ni Septemba 4, 2026, kwa mujibu wa Ibara ya 149(2) ya Katiba, baada ya Rais kukubali tarehe hiyo. Amesema kwa maana hiyo, aliyekuwa Makamu wa Rais ataendelea kuwepo madarakani hadi Septemba 4, 2026, huku akieleza kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala hilo.

Johari amesema Ibara ya 50(4) inaweka utaratibu wa kujaza nafasi ya Makamu wa Rais endapo nafasi hiyo iko wazi kutokana na kifo au kujiuzulu. Hata hivyo, amesema katika kutafsiri Katiba, vifungu vyake vinapaswa kusomwa kwa pamoja kwa kuzingatia Doctrine of Harmonious Construction, yaani msingi wa kutafsiri vifungu kwa namna inayoviweka katika uwiano. Amesema kwa msingi huo, suala la nafasi ya Makamu wa Rais haliwezi kuangaliwa kwa Ibara ya 50(4) pekee.

Ameeleza kuwa ili kubaini sifa za mtu anayestahili kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ni muhimu pia kuangalia Ibara ya 47(4), inayosema mtu hatateuliwa kugombea au kushika nafasi hiyo bila kuwa na sifa zinazotakiwa. Johari amesema hivyo anapingana na tafsiri kwamba Ibara hiyo inahusu kipindi cha kugombea pekee, akisisitiza kuwa kifungu hicho kimetaja wazi pia suala la kushika nafasi ya Makamu wa Rais.

Johari ameongeza kuwa Ibara ya 47(4) inaweka sifa za mtu anayestahili kuteuliwa kugombea au kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ikiwemo kuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano, kuwa na umri wa miaka 40, kuwa mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa na kuwa na sifa za kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Amesema mtu akipoteza sifa hizo, ikiwemo uraia wa Tanzania, suala hilo linaweza kuathiri nafasi yake.

Soma kuhusu > Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Amesema kiti cha Makamu wa Rais kinaweza kuwa wazi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo muda wa madaraka kumalizika, kifo, kuapishwa kuwa Rais, kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, kuondolewa madarakani au kuacha kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba. Johari amesema kipengele hicho cha mwisho kinabeba mazingira mengine yanayoweza kumfanya mtu kushindwa kuendelea na nafasi hiyo.

Kwa upande mwingine, amesema kipengele cha Ibara ya 47(4) kinapaswa kusomwa pamoja na Ibara ya 50(4), akieleza kuwa mtu akipoteza sifa za kushika nafasi ya Makamu wa Rais, kiti hicho kinaweza kuwa wazi. Johari amesema kuvuliwa uanachama wa chama cha siasa ni miongoni mwa mazingira yanayoweza kuathiri sifa hizo, na kwamba vifungu hivyo vinapaswa kutafsiriwa kwa pamoja.

Ametolea mfano uteuzi wa aliyekuwa Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango, akisema mwaka 2021 Rais Samia Suluhu Hassan aliwasilisha jina lake Bungeni kwa mujibu wa Ibara hiyo hiyo ya 50(4), licha ya mazingira hayo kutotajwa moja kwa moja katika kifungu hicho. Amesema Bunge lilimthibitisha Mpango Machi 30, 2021, na siku iliyofuata, Machi 31, 2021, akaapishwa na Jaji Mkuu.

Siwezi kusoma uharo wa chawa..lakini asante kwa kiliweka hapa, we ue interest wasome
 
sijaelewa kwa hiyo tusema labda raisi samia akivuliwa uanachama leo hii na uraisi wake unakoma? sidhani nielewavyo hiyo ni katiba ya south afrika ndiyo iko hivyo lkn wao hawachagui mtu bali wanachagua chama i.e siku ya uchaguzi hakuna jina la mtu bali chama halafu chama ndiyo kinachagua mtu kuwa raisi hivyo chama kinaweza pia kumuondoa raisi na kuweka mwingine bila ya haja ya kuitisha uchaguzi lkn tanzagiza hatuchagui chama bali mtu, mimi siyo mwanasheria lkn sidhani kama ni sahihi kumfuta uanachama na umakamu unakoma kwani makamu ni raisi in waiting hivyo kwa logic yangu hawezi kufukuzwa tu kienyeji, so raisi samia akifa sasa hivi au akapata tatizo kubwa la kushinda kuendelea kuwa raisi kwa mfano nani atakuwa raisi? ...
Tanzania kwa katiba ya sasa huwezi kuwa Rais, Makamu wa Rais au mbunge bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.
 
Tanzania kwa katiba ya sasa huwezi kuwa Rais, Makamu wa Rais au mbunge bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

naelewa hilo lkn vipi kama hypothecally raisi samia akifukuzwa uanachana na ccm sasa hivi, uraisi wake unakoma pia? nielewavyo tanzagiza tunachagua mtu na siyo chama. kumbuka kama tungetenganisha kofia mbili i.e uwenyekiti wa chama na uraisi ina maana raisi anaweza kufukuzwa uanachama pia hata kwa hila tu halafu uraisi pia unakoma? ...
 
Akifukuzwa uanachama urais wake unakoma.
 
Akifukuzwa uanachama urais wake unakoma.

hapana, haukomi, uraisi wa tanzagiza ni zaidi ya chama, raisi anaweza hata kuongoza bila ya chama kwa decree tu mpaka labda atakajiunga na chama kingine au hata kuanzisha chake, lkn uraisi haukomi.

haya mambo sa waliyaona yote na ndiyo maana katiba yao baada ya apartheid waliondoa hilo, ni kwamba wao (sa) wanachagua chama halafu ndiyo kina jukumu la kuchagua raisi kama kikishinda uchaguzi na pia kinaweza kumuondoa raisi bila ya uchaguzi na kuweka mwingine , na ndiyo maana sa mkuu wa chama siyo raisi wanatenganisha, hivyo raisi akiharibu hana influence kwenye chama kwa maana bosi wa chama ni mwingine na hivyo wanaweza kumondoa muda wowote ule na kuweka mwingine bila ya uchaguzi ...
 
sijaelewa kwa hiyo tusema labda raisi samia akivuliwa uanachama leo hii na uraisi wake unakoma? sidhani nielewavyo hiyo ni katiba ya south afrika ndiyo iko hivyo lkn wao hawachagui mtu bali wanachagua chama i.e siku ya uchaguzi hakuna jina la mtu bali chama halafu chama ndiyo kinachagua mtu kuwa raisi hivyo chama kinaweza pia kumuondoa raisi na kuweka mwingine hata katikati ya muhula kabla ya uchaguzi kuu na bila ya haja ya kuitisha uchaguzi lkn tanzagiza hatuchagui chama bali mtu.

mimi siyo mwanasheria lkn sidhani kama ni sahihi kumfuta uanachama na umakamu unakoma kwani makamu ni raisi in waiting hivyo kwa logic yangu hawezi kufukuzwa tu kienyeji, so raisi samia akifa sasa hivi au akapata tatizo kubwa la kushindwa kuendelea kuwa raisi kwa mfano nani atakuwa raisi? ...
Inamaana toka juzi nchi haina Makamu wa Rais
Haya ni maajabu
 
Back
Top Bottom