Hamza Johari: Kikatiba, nafasi ya Nchimbi ilikoma baada ya kuvuliwa uanachama CCM

Hakuna kipengele kwenye katiba kinachosema mtu atakoma kua makamu siku ambayo atasitishiwa uwanachama wake.Hizi tafsiri nyingine ambazo haziko direct ni utashi wa mtu na kulingana na maamuzi anayo yatetea.Ningekuwa mtu wa mwisho kuamini AG huyu angeweza kuiongoza serikali vizuri
 
Huyo mwanasheria aanze kugawa urithi kwa watoto!!

wazalendo wasioonekana watamla kichwa,katiba mama ni nguzo kuu kabla ya chama!!

Mi sijui,lakini kwa hiki kinachotamkwa ni rasmi walionyuma ya nchimbi walicheza karata zao vema!

Hapa wame create mgogoro wa kimedani,yaani kikatiba Bado nchimbi ni makam wa Rais sasa ikitokea kabla ya tarehe tajwa akatangaza kubadili maamuzi kuwa amefikiriaaaa sana ameona asijiuzulu Hadi katiba mpya ipatikane chama kitafanyaje!!?

Yaani Hadi tarehe 4 September,nchimbi akibatilisha uamuzi akasema wazee wa chama wamemshauri taifa Bado linamhitaji akabatilisha kwa barua itakuaje kikatiba!!?

Nawaza sana,
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoa ufafanuzi kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais​

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ametoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu lini nafasi ya Makamu wa Rais inakuwa wazi, akisema tarehe rasmi ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais ni Septemba 4, 2026, kwa mujibu wa Ibara ya 149(2) ya Katiba, baada ya Rais kukubali tarehe hiyo. Amesema kwa maana hiyo, aliyekuwa Makamu wa Rais ataendelea kuwepo madarakani hadi Septemba 4, 2026, huku akieleza kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala hilo.

Johari amesema Ibara ya 50(4) inaweka utaratibu wa kujaza nafasi ya Makamu wa Rais endapo nafasi hiyo iko wazi kutokana na kifo au kujiuzulu. Hata hivyo, amesema katika kutafsiri Katiba, vifungu vyake vinapaswa kusomwa kwa pamoja kwa kuzingatia Doctrine of Harmonious Construction, yaani msingi wa kutafsiri vifungu kwa namna inayoviweka katika uwiano. Amesema kwa msingi huo, suala la nafasi ya Makamu wa Rais haliwezi kuangaliwa kwa Ibara ya 50(4) pekee.

Ameeleza kuwa ili kubaini sifa za mtu anayestahili kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ni muhimu pia kuangalia Ibara ya 47(4), inayosema mtu hatateuliwa kugombea au kushika nafasi hiyo bila kuwa na sifa zinazotakiwa. Johari amesema hivyo anapingana na tafsiri kwamba Ibara hiyo inahusu kipindi cha kugombea pekee, akisisitiza kuwa kifungu hicho kimetaja wazi pia suala la kushika nafasi ya Makamu wa Rais.

Johari ameongeza kuwa Ibara ya 47(4) inaweka sifa za mtu anayestahili kuteuliwa kugombea au kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ikiwemo kuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano, kuwa na umri wa miaka 40, kuwa mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa na kuwa na sifa za kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Amesema mtu akipoteza sifa hizo, ikiwemo uraia wa Tanzania, suala hilo linaweza kuathiri nafasi yake.

Soma kuhusu > Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Amesema kiti cha Makamu wa Rais kinaweza kuwa wazi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo muda wa madaraka kumalizika, kifo, kuapishwa kuwa Rais, kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, kuondolewa madarakani au kuacha kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba. Johari amesema kipengele hicho cha mwisho kinabeba mazingira mengine yanayoweza kumfanya mtu kushindwa kuendelea na nafasi hiyo.

Kwa upande mwingine, amesema kipengele cha Ibara ya 47(4) kinapaswa kusomwa pamoja na Ibara ya 50(4), akieleza kuwa mtu akipoteza sifa za kushika nafasi ya Makamu wa Rais, kiti hicho kinaweza kuwa wazi. Johari amesema kuvuliwa uanachama wa chama cha siasa ni miongoni mwa mazingira yanayoweza kuathiri sifa hizo, na kwamba vifungu hivyo vinapaswa kutafsiriwa kwa pamoja.

Ametolea mfano uteuzi wa aliyekuwa Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango, akisema mwaka 2021 Rais Samia Suluhu Hassan aliwasilisha jina lake Bungeni kwa mujibu wa Ibara hiyo hiyo ya 50(4), licha ya mazingira hayo kutotajwa moja kwa moja katika kifungu hicho. Amesema Bunge lilimthibitisha Mpango Machi 30, 2021, na siku iliyofuata, Machi 31, 2021, akaapishwa na Jaji Mkuu.

Waambieni sisi tunachotaka sasa ni Katiba Mpya. Huo upumbavu wa taifa kuwa na mungumtu hatuutaki.
 
Zanzibar sio nchi nyingine
 
Huyo mwanasheria aanze kugawa urithi kwa watoto!!

wazalendo wasioonekana watamla kichwa,katiba mama ni nguzo kuu kabla ya chama!!

Mi sijui,lakini kwa hiki kinachotamkwa ni rasmi walionyuma ya nchimbi walicheza karata zao vema!

Hapa wame create mgogoro wa kimedani,yaani kikatiba Bado nchimbi ni makam wa Rais sasa ikitokea kabla ya tarehe tajwa akatangaza kubadili maamuzi kuwa amefikiriaaaa sana ameona asijiuzulu Hadi katiba mpya ipatikane chama kitafanyaje!!?

Yaani Hadi tarehe 4 September,nchimbi akibatilisha uamuzi akasema wazee wa chama wamemshauri taifa Bado linamhitaji akabatilisha kwa barua itakuaje kikatiba!!?

Nawaza sana,
🤣
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali atoa ufafanuzi kuhusu nafasi ya Makamu wa Rais​

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ametoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu lini nafasi ya Makamu wa Rais inakuwa wazi, akisema tarehe rasmi ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais ni Septemba 4, 2026, kwa mujibu wa Ibara ya 149(2) ya Katiba, baada ya Rais kukubali tarehe hiyo. Amesema kwa maana hiyo, aliyekuwa Makamu wa Rais ataendelea kuwepo madarakani hadi Septemba 4, 2026, huku akieleza kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala hilo.

Johari amesema Ibara ya 50(4) inaweka utaratibu wa kujaza nafasi ya Makamu wa Rais endapo nafasi hiyo iko wazi kutokana na kifo au kujiuzulu. Hata hivyo, amesema katika kutafsiri Katiba, vifungu vyake vinapaswa kusomwa kwa pamoja kwa kuzingatia Doctrine of Harmonious Construction, yaani msingi wa kutafsiri vifungu kwa namna inayoviweka katika uwiano. Amesema kwa msingi huo, suala la nafasi ya Makamu wa Rais haliwezi kuangaliwa kwa Ibara ya 50(4) pekee.

Ameeleza kuwa ili kubaini sifa za mtu anayestahili kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ni muhimu pia kuangalia Ibara ya 47(4), inayosema mtu hatateuliwa kugombea au kushika nafasi hiyo bila kuwa na sifa zinazotakiwa. Johari amesema hivyo anapingana na tafsiri kwamba Ibara hiyo inahusu kipindi cha kugombea pekee, akisisitiza kuwa kifungu hicho kimetaja wazi pia suala la kushika nafasi ya Makamu wa Rais.

Johari ameongeza kuwa Ibara ya 47(4) inaweka sifa za mtu anayestahili kuteuliwa kugombea au kushika nafasi ya Makamu wa Rais, ikiwemo kuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano, kuwa na umri wa miaka 40, kuwa mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa na kuwa na sifa za kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi. Amesema mtu akipoteza sifa hizo, ikiwemo uraia wa Tanzania, suala hilo linaweza kuathiri nafasi yake.

Soma kuhusu > Dkt. Emmannuel Nchimbi afukuzwa uanachama wa CCM

Amesema kiti cha Makamu wa Rais kinaweza kuwa wazi kwa sababu mbalimbali, ikiwemo muda wa madaraka kumalizika, kifo, kuapishwa kuwa Rais, kutiwa hatiani kwa kosa la jinai, kuondolewa madarakani au kuacha kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba. Johari amesema kipengele hicho cha mwisho kinabeba mazingira mengine yanayoweza kumfanya mtu kushindwa kuendelea na nafasi hiyo.

Kwa upande mwingine, amesema kipengele cha Ibara ya 47(4) kinapaswa kusomwa pamoja na Ibara ya 50(4), akieleza kuwa mtu akipoteza sifa za kushika nafasi ya Makamu wa Rais, kiti hicho kinaweza kuwa wazi. Johari amesema kuvuliwa uanachama wa chama cha siasa ni miongoni mwa mazingira yanayoweza kuathiri sifa hizo, na kwamba vifungu hivyo vinapaswa kutafsiriwa kwa pamoja.

Ametolea mfano uteuzi wa aliyekuwa Makamu wa Rais, Philip Isdor Mpango, akisema mwaka 2021 Rais Samia Suluhu Hassan aliwasilisha jina lake Bungeni kwa mujibu wa Ibara hiyo hiyo ya 50(4), licha ya mazingira hayo kutotajwa moja kwa moja katika kifungu hicho. Amesema Bunge lilimthibitisha Mpango Machi 30, 2021, na siku iliyofuata, Machi 31, 2021, akaapishwa na Jaji Mkuu.

Attachments

  • 6385809-231b80ee3851c7ae56d080ce6609546b.mp4
    11 MB
Tena kakaapa eti lazima kamlete Mange Kizimkazi..

Hawa vibaka wamemgeuza Mange mradi wao yaani wakijiskia wanataka pesa wanachota kwa kisingizio cha kuhakikisha kesi ya kumrudisha Mange Tanzania.

Wakifikiri USA na mifumo yake ya kisheria inafanana na banana republics.
Huyu jamaa aliposema anaangalia njia ya kumleta Mange ndiyo nilijua ni hawa hawa ''wasomi'' wa Samia. Nilimdharau sana sana. Mwanasheria mkuu unaacha ku-deal na issues za maana unakimbilia kuonyesha upumbavu wako namna hii.
 
Mkuu huyo Johari kwa wanaofahamu uwezo wake [ waliosoma na kufanya nae kazi] wanajua ni bomu.

Hapo kafika kwa kete ya uzanzibari wake na kuwa dalali kwenye lile dili la DP World

Tukiweka meritocracy hawezi hata kuwa mwanasheria wa kampuni .

Ila ticket ya uongozi zama za Kizimkazi ni uchawa ukijumlisha na uzanzibari ndio hilo bumunda watanganyika wanalo kama AG.
 
Back
Top Bottom