Hamza Johari: Kikatiba, nafasi ya Nchimbi ilikoma baada ya kuvuliwa uanachama CCM

Rais hawezi kuongoza bila kuwa na chama kwa katiba hii.
 
Mkuu, Katiba imebakwa mchana kweupe. Sifa za kuchaguliwa/kuteuliwa na sababu za kuachia kiti ni mambo mawili tofauti hayapaswi kuchanganywa. Angalia upande wa speaker.
Spika wa bunge sio lazima awe na chama au mbunge.
 
 

Attachments

  • 675c679920d4d64c27f242780da68a29.webp
    261.3 KB · Views: 10
Rais hawezi kuongoza bila kuwa na chama kwa katiba hii.

sidhani kama ni kweli, raisi wa tanzagiza ana room ya kufanya mengi, uraisi kwa katiba ya tanzagiza kama ilivyo uko juu ya chama, kuna jambo ambalo binasi naliona ni muhimu labda klk yote, uraisi wa tanzagiza kikatiba unakoma pale raisi mwingine anapoapishwa, that tells everything, maana yake ni kwamba kwa maoni yangu tanzagiza kwa hali ya kawaida kikatiba haiwezi kuwa bila ya raisi na ndiyo mana kuna makamu wa raisi kazi yake kuu ni kusubiri uraisi tu mpaka mwisho wa muhula ni kama hadithi za utotoni za fisi na mkono wa mtu unaoninginia sijui kama uliwahi kuzisikia, again mimi siyo mwanasheria na inawezakana naandika bullshit tu ...
 
Nakumbuka kuna wabunge walifukuzwa kwenye chama chao lakini tuliambiwa kuwa kufukuzwa uanachama hakumaanishi kufukuzwa ubunge. Hakuna aliyesema kuwa walikosa sifa ya kuwa wabunge pale waliponyang'anywa uanachama wa chama chao.

Amandla...
 
Vipi kuhusu ubunge wa wale wabunge 19 wa CDM maarufu kama COVID-19 pale walipovuliwa uanachama!?

Mwanasheria Mkuu mbona hakutoka hadharani na kufafanua kuhusu nafasi zao za ubunge kuwa zimekoma mara tu baada ya kuvuliwa uanachama na vikao halali vya chama chao!?

Utawala wa Marais wa awamu ya 5 na 6 utakuja kukumbukwa kwa maamuzi yao ya kiutawala. Na hasa hii ya sasa ambayo ni "replica" ya Mfalme Mangungo wa Msovero.

Bila hatua kuchukuliwa kwa haraka, mpaka ifikapo 2030 tutakuwa tumechoka mno. Yaani Vice President anavuliwa uanachama kwa kuunga mkono mabadiliko ya katiba kuukuu ya 1977!
 
Rais akitimuliwa uanachama urais wake unakoma na makamu wa Rais anachukua nchi. Katiba hii hairuhusu rais asiye na chama kuongoza nchi.
 
Spika wa bunge sio lazima awe na chama au mbunge.
Spika na Naibu wa Spika
84(1) Kutakuwa na Spika wa Bunge ambaye atachaguliwa na Wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au mwenye sifa za kuwa Mbunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.

84(7) Spika atakoma kuwa Spika na ataacha kiti cha Spika litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) iwapo mtu huyo alichaguliwa kutoka miongoni mwa Wabunge, basi ikiwa atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote ambayo haihusiki na kuvunjwa Bunge; au
(b) ikiwa kutatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Spika lingemfanya mtu huyo asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi wa Spika; Sifa mojawapo ya kuwa mbunge lazima uwe na chama.

Sifa ya kuwa Mbunge lazima uwe na chama, so automatically huwezi kuwa au kubaki kwenye nafasi ya spika bila kuwa na chama.
 
Mwijaku aligombania uspika bila kuwa mbunge.
 
Mwanasheria Mkuu ndio Anaitwa Hamza Imagine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…