Kwezisho,
Utawatafutia wapi?
Mjadala mpana wa nini na utaufanya na nani ilhali akina Hawa
biti Maftah, Titi Mohamed, Sharifa biti Mzee, Tatu biti
Mzee, Dharura biti Abdulrahman, Halima Selengia, Lucy
Lameck na wengineo kutaja majina machache weshatangulia mbele
ya haki?
Msome Susan Geiger: ''TANU Women.''
Kafanya utafiti huo huna haja ya kuurudia.
Nguruvi3,Hapana chuki ipo kubwa na ya dhahiri.
Tumelumbana sana na huyu mzee na tunamjua vema
Lengo lake ni fitna kati ya jamii, na ili afanikiwe lazima awe na daraja.
Nyerere ni daraja tu ili akamilishe azma yake. Hutamsikia akimsifia hata siku moja kila asiku anatafuta namna ya kumdhalilisha , kashfu, tukukana n.k.
Baada ya hapo daraja linakuwa tayari, anapita kuelekea kule anakotaka
Tunakataa mambo mengi si historia kama ilivyo. Kwanza, lazima tukiri Nyerere ni sehemu muhimu sana ya Historia ya Tanganyika.
kumbuka, kuna sehemu muhimu na sehemu kubwa ni vitu tofauti kabisa.
Na kwamba kumdhalilisha ni kukosa adabu kwa kiwango cha maana
Pili, uhuru wa nchi ilikuwa jukumu la pamoja.
Bila coalition ya Watanganyika pengine tusingefika hapa katika muda huu tunaoongea.
Tatu, tunaheshimu michango ya watu wote, hii habari ya familia tukufu ya Sykes, ni kutaka kuchagua watu muhimu na watu hafifu. Si kweli, kila mtu alikuwa na mchango wake
Kolorama,Maalim Mohamed Said assalam alaykum. Nimekusoma kwa muda mrefu sana kupitia jukwaa hili. Sina budi kukushukuru kwa niliyojifunza kutoka kwako. Nimesoma somo la historia hadi kidato cha sita. Lazima tukubali historia yetu inamapungufu makubwa sana. Hayo nisingeyajua kupitia historia rasmi pasi kukusoma wewe. Mungu akujalie umri mrefu na afya njema.
Magari7,Mzee mohamed said :
Nimekua nafuatilia huu mjadala tokea awali, na nadhani mzee umeona comment zangu kwenye page za kwanza kwanza kabisa!
Mimi ni kijana,
Napia ni Mkristo, lakini nimevutiwa mno na namna ya uandishi wako tokea mwanzo, sijaona udini wala Chuki wala maneno ya kashfa ambayo umeyatoa dhidi yetu wa Kikristo. Kila upande umeupa Heshima!
Ahsante sana.
Nimejifunza, kuamua 'Kuelewa' mtu asipoamua kuelewa basi kamwe hawezi kukubali 'kuelewa' asipoamua kujifunza, kamwe hawezi 'Kujifunza'
Mimi nadhani umeongea kwa upana sana, tulio amua kujifunza na kuelewa , tumekuelewa mzee na kujifunza!
Kazi nzuri mzee said!
Nguruvi3,Mohamed katika bandiko umewataja wote na hakuna ushahidi waliacha maandiko.
Kutaka kukwepa ukweli unasema Matola hakuandika kuhusu maisha yake.
Well, kama hakuandika ungemtaja ingetosha. Kilichofanya ukamkwepa ni ukweli kuwa yeye ni Mwanzilishi wa AA kama Mwenyekiti.
Hapa kuna jambo jingine, kwamba licha ya kutojulikana elimu yake ilimsaidia kushawishi townsman kama Kelist kuunda chama
Na hilo linaonekana alipopewa uenyekiti na Townsman kuwa katibu
Inashangaza mchango wa Matola unafutwa kwa hadithi za 1933 baada ya kifo chake ili kuhakikisha Klesit na Familia tukufu inaendelea kusifiwa!
Kuhusu Imani, inategemea nani ameandika na kwa lengo gani.
Sitegemei Daisy aongee jambo zuri kuhusu Nyerere hata siku moja kama ambavyo Mohamed Said na Faiza wangefanya
Harakati za uhuru zinachukuliwa kama za Pwani, ukweli ni kuwa zilisambaa kwingineko
Na hapa tunajifunza jambo jingine, kwamba harakati hizo zilibebwa kwa msingi wa dini na hivyo kukwama kwa miaka 29 chini ya Familia tukufu ya Sykes.
Hakukuwa na broad coalition dhidi ya Mkoloni na hivyo kukatokea mgawanyiko
Miaka ya 1950 Nyerere alikuja na idea mpya. Kubadili TAA kuwa TANU ililenga kuleta broad coalition na inclusion ya different sect of society.
Ilimchkua miaka chini ya 10 kufikia lengo la uhuru.
Mafanikio yake yamejengwa katika elimu, exposure and leadership
Kwavile alikuwa educated na exposure of modern politics aliweza kumbwaga Abdul Sykes katika uchaguzi na kuendelea na transformation za chama kama kuandika katiba
Kuandika katiba ilikuwa ni kuachana na mass movement na kufanya politics kama sehemu ya institution.
Hilo ndilo likawaleta Watanganyika wa dini, kabila , Imani mbali mbali kama kitu kimoja chini ya institution ya TANU ambayo before yeye haikuwepo!
Kutokana na frustrations za kupoteza uongozi na kuona the future ilianza kutoweka, Abdul Sykes akaamua kurudia wazee ili kupata kuungwa mkono.
Ndipo alipomtumia Sheikh Amir kuanza kujenga umaarufu na movement nyingine dhidi ya Nyerere. Hili kalisema MS katika Makala zake alipomnukuu kiongozi mmoja akisema '...mnampa huyu mtu chama mnamjua?"'
MS kaendelea kutueleza '...Sheikh alitoka na kuwaangalia waliokuwa wanamzomea, akasema ipo siku mtanikumbuka''
MS anaonyesha katika maandishi yake Abdul was real frustrated, the last card he could play ni misikitini akimtumia sheikh Amir.
Nyerere hakuvumilia, akamuondoa Amir haraka iwezekanavyo akiwaangalia akina Abdul kwa jicho la karibu. Mtawala yoyote duniani angefanya hivyo.
Bila waislamu tusingepata uhuruNdugu zetu waislamu mlifanya juhudi kubwa Tanganyika kupata uhuru.
Mwandwanga,Bila waislamu tusingepata uhuru
Wanajamvi, kuna wale wambao hawakuwahi kumsikia au kumwelewa Mohamed.
Nguruvi3,Wanajamvi, kuna wale wambao hawakuwahi kumsikia au kumwelewa Mohamed.
Tafadhali sikiliza sauti hiyo kisha utafakari
Katika dakika 11 hadi 14 MS anasema Abdul Sykes alimwingiza Nyerere katika chama 1952 na kumpa uongozi 1953. Akasema wakati huo hakuna aliyemjua Nyerere au kumsikia
Tukirudi nyuma Nyerere alikuwa mwanafunzi Makerere na zipo harakati na mwasiliano aliyofanya kuhusu chama cha wanafunzi wa Tanganyika. Haya kayasema Mohamed katika maandiko yake
Nyerere alikuwa katibu wa Chama akiwa Tabora. Na Tabora ilikuwa moja ya matawi makubwa ya chama. Nyerere alihudhuria mkutano mkuu 1948 akakutana na viongozi wa makao makuu
Katika kufifisha historia, MS anasema Nyerere kaanza siasa na Abdul Sykes 1952
Fikiria hapo
Pili, katika dakika 51 kuendelea, MS anasema baada ya kukabidhiwa chama na Abdul Sykes, chama kiilikufa kwasababu hakuna aliyemjua Nyerere.
Well, ni Nyerere aliyemshinda Abdul katika uchaguzi. Sasa alishindaje bila kujulikana linabaki kuwa swali.
Lakini pia MS anatusaidia katika hoja zetu kuwa Nyerere hakulingana na Abdul na kuwaweka katika mizani ya kisiasa ni makosa. MS anamnukuu Abdul akisema '...Nyerere ni msomi ana degree ya uzamili(master) hivyo Abdul aliona vema ashike chama'
Kwanini tunaposema elimu ya Nyerere ilimpa competitive edge katika siasa tunaonekana wehu? Kwanini wakisema ni sawa,tukisema ni makosa'
Hoja nyingine ni ile ya hotuba ya 'moto wa Waislam ukiwaka' maneno mazito yalisemwa kumtisha Nyerere baada ya kusoma waraka ulioandaliwa na akina Sheikh Hassan Amir
Ni mtawala gani angevumillia kitisho hicho cha 'Sheikh Amir'
MS anatusaidia anaposema (dakika 51 kuwa mikutano ya sheikh ilikuwa usiku) kwa maana kuwa kulikuwa na harakati zilizoendelea kichini chini za kutaka kumg'oa kupitia misikitini
Hivyo kuondolewa kwa Sheikh Hassan Amir hakukuwa uonevu dhidi ya waislam kama anavyodai MS, bali ni misuguano ya kisiasa kati ya sheikh na kundi lake na Nyerere
Hili linatueleza jambo moja kwamba Sheikh alikuwa na watu wake nyuma.
Wengine walisusa serikali ya Nyerere baada ya sheikh kuondolewa na mmoja ni Abdul Sykes
Tuna ushahidi wa wazi kutoka kwa MS akimnukuu Abdul Sykes aliyekiri kuwa Nyerere alikuwa na uwezo wa elimu Zaidi yake. Leo MS anapowaweka katika mizani anatfuta nini?
Na mwisho msikilize MS akizungumzia Nyerere, chama na ukatoliki.
Kwa ufundi sana alikuwa ana link kati ya Nyerere mkatoliki na siasa za nchi.
Lile daraja linaanza kujengwa kuanzia hapo
MS sipendi kujua jibu la kivukoni, tofauti na wasomaji wako watiifu mimi natumia ubongo kuchambua pumba na mchele.Nguruvi3,
Mimi nakuhurumia sana tena sana kuwa hujui uwezo wako na hii
si hali nzuri.
Nimekuuliza na hukunijibu kwa kuwa uneingiwa na hofu ya jibu
langu.
Nakuuliza tena.
Je ungependa kujua jibu la jopo la waandishi wa historia ile ya
Chuo Cha Kivukoni walipopewa ''notes'' za Abdul Sykes kuhusu
historia ya TANU?
Daisy katika kuandika historia ya babu yake kaandika habari
kutoka 1894 - 1949 tena akitumia mswada wa alioandika Kleist.
Nyerere ataingia vipi katika historia hiyo iliyoandikwa na Kleist
kabla ya kifo chake 1949?
Ndipo ninapokuhurumia kuwa hujui ukomo wa uwezo wako na
sasa unakuwa kichekesho.
Hiyo ''idea,'' mpya unayozungumza ya 1950 haikuletwa na Nyerere
kwa kuwa 1950 hakuna aliyekuwa anamfahamu katika siasa za TAA
pale New Street.
Hiyo ''broad coalition'' unayoizungumza ilianza 1950 kupitia TAA
Political Subcommittee baada ya Abdul na Kyaruzi kuingia katika
uongozi.
Hakuwa Nyerere aliyeibadili TAA kuwa TANU.
Mchakato huu ulianza 1950 na katika watu waliokuwa na msaada
mkubwa katika hili ni Earle Seaton kuisaidia TAA kuandika katiba
ambayo Gavana Twining aliikataa
Nguruvi3,
Hayo mengine uliyoandika ni vichekesho vikubwa sitakujibu chochote
ila hili la Sheikh Hassan bin
Ahante nilidtegemea ungekanusha kauli zangu, midhali unakubaliana nazo, tusonge mbeleNguruvi3,
Huyo uliyemsikia ndiye mimi khasa.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Historia hii ilikuwa haifahamiki kwa wengi.
Nashukuru kuwa sasa imekuwa, ''documented,''
na itaishi kusomwa na watakaokuja baaada yetu.
Tusubiri fikra za wengine wewe nishakusikia.
hiyo I'd yangu nani mwingine anayo? mimi nasifia kitu ninachoona cha haki na kwa taarifa yako sijawahi kuwa na I'd tofauti na hiiYan saizi unarudi n I'd ya pili kujisifia
Mkuu kwanza nikushukuru kwa kulileta hili jamvini. Wengi hawaelewi kwanini tunahoji, tuna challenge na kutoa maoni kuhusiana na maandiko ya MohamedMkuu Nguruvi heshima yako. Kwa uzoefu wangu wa jukwaa hili japo nilikuwa nasoma kama mgeni ila nimekusoma siku nyingi sana. Nakupongeza sana kwa kutoa challenge kwa maalim Mohamed Said ila lazima tukubaliane kuwa historia yetu inamapungufu makubwa na pengine niseme hayajatokea kwa bahati mbaya. Historia inakuwaga na chimbuko ili upate mtiliriko mzuri ila mengi hayajasemwa kwenye historia rasmi na ndo maana maalim yeye kajaribu kuleta yale anayojua, kama Taifa lazima tukubali kuandika historia yetu kwa usahihi kwa manufaa mapana ya jamii yetu.
Asante mkuu Nguruvi3 nimepata kujua rangi halisi ya mzee Ms nashukuru sanaAhante nilidtegemea ungekanusha kauli zangu, midhali unakubaliana nazo, tusonge mbele
Nguruvi3,MS sipendi kujua jibu la kivukoni, tofauti na wasomaji wako watiifu mimi natumia ubongo kuchambua pumba na mchele.
Nilishachambua pumba za kivukoni na mchele na sasa ninaendelea kwingine
Ni kweli nitaonekana kichekesho sana na wala sitakuwa wa kwanza.
Ninafahamu kichekesho changu ni challenge na hilo halinitii wasi wasi kabisa.
Hakuna niliposema Nyerere alitakiwa kuonekana katika historia ya miaka 1800 hata 1929.
Cecil Matola anaanzisha AA Nyerere ana miaka 7, vipi angeonekana katika historia?
Wakuonekana hapo japo kwa kutajwa ni Cecil Matoala.
Kwa makusudi kabisa nafasi yake inazibwa na Kleist Sykes!!
Nikasema hivi mwaka 1948 Nyerere alihudhuria mkutano mkuu, sikusema 1848
Kuhusu Daisy, ni vema aandike historia ya babu yake na babu zake.
Hata hivyo, nature inatushawishi kutumia akili zetu maana kuna conflict of interest.
Unategemea Daisy aseme lolote jema kuhusu Nyerere aliyemweka Abdul Sykes bench!
Kuhusu picha, sijui zinaeleza nini mkuu. Je, hizo zinaeleza kuhusu katiba iliyoandikwa na Abdul Sykes ambayo umeshindwa kuiwasilisha hapa? Kama picha ndiyo katiba hewalaa
Pili, nimekuuliza kama Nyerere hakufanya transformation ya TAA kwenda TANU, nitajie mkutano au mkusanyiko mmoja tu uliowahi kufanyika kwa jina la TANU kabla ya hapo
Sidhani kama picha zinajibu hoja hizi
MS una wasomaji na wafuasi wengi wanaosoma historia yako kwa mafanikio makubwa
Kuna kundi dogo sana la vichekesho nikiwemo linasoma historia yako kwa ufahamu , kuhoji na kwa weledi.
Hili kundi ni muhimu sana kwako na lisome ukiendelea kucheka na vichekesho lakini lisome ukipata muda usilidharau
Kolorama,Mkuu Nguruvi heshima yako. Kwa uzoefu wangu wa jukwaa hili japo nilikuwa nasoma kama mgeni ila nimekusoma siku nyingi sana. Nakupongeza sana kwa kutoa challenge kwa maalim Mohamed Said ila lazima tukubaliane kuwa historia yetu inamapungufu makubwa na pengine niseme hayajatokea kwa bahati mbaya. Historia inakuwaga na chimbuko ili upate mtiliriko mzuri ila mengi hayajasemwa kwenye historia rasmi na ndo maana maalim yeye kajaribu kuleta yale anayojua, kama Taifa lazima tukubali kuandika historia yetu kwa usahihi kwa manufaa mapana ya jamii yetu.
Ahante nilidtegemea ungekanusha kauli zangu, midhali unakubaliana nazo, tusonge mbele
Hahahahahaha na ya TANU imeanzia kumtaja Nyerere bila Abdulwahd SykesHapo kwa Cecil Matola naona kuna hoja ya msingi imeachwa... Historia inaanzia kwa katibu bila kumtaja Rais wa chama!?
Hahahahahaha na ya TANU imeanzia kumtaja Nyerere bila Abdulwahd Sykes