MS sipendi kujua jibu la kivukoni, tofauti na wasomaji wako watiifu mimi natumia ubongo kuchambua pumba na mchele.
Nilishachambua pumba za kivukoni na mchele na sasa ninaendelea kwingine
Ni kweli nitaonekana kichekesho sana na wala sitakuwa wa kwanza.
Ninafahamu kichekesho changu ni challenge na hilo halinitii wasi wasi kabisa.
Hakuna niliposema Nyerere alitakiwa kuonekana katika historia ya miaka 1800 hata 1929.
Cecil Matola anaanzisha AA Nyerere ana miaka 7, vipi angeonekana katika historia?
Wakuonekana hapo japo kwa kutajwa ni Cecil Matoala.
Kwa makusudi kabisa nafasi yake inazibwa na Kleist Sykes!!
Nikasema hivi mwaka 1948 Nyerere alihudhuria mkutano mkuu, sikusema 1848
Kuhusu Daisy, ni vema aandike historia ya babu yake na babu zake.
Hata hivyo, nature inatushawishi kutumia akili zetu maana kuna conflict of interest.
Unategemea Daisy aseme lolote jema kuhusu Nyerere aliyemweka Abdul Sykes bench!
Kuhusu picha, sijui zinaeleza nini mkuu. Je, hizo zinaeleza kuhusu katiba iliyoandikwa na Abdul Sykes ambayo umeshindwa kuiwasilisha hapa? Kama picha ndiyo katiba hewalaa
Pili, nimekuuliza kama Nyerere hakufanya transformation ya TAA kwenda TANU, nitajie mkutano au mkusanyiko mmoja tu uliowahi kufanyika kwa jina la TANU kabla ya hapo
Sidhani kama picha zinajibu hoja hizi
MS una wasomaji na wafuasi wengi wanaosoma historia yako kwa mafanikio makubwa
Kuna kundi dogo sana la vichekesho nikiwemo linasoma historia yako kwa ufahamu , kuhoji na kwa weledi.
Hili kundi ni muhimu sana kwako na lisome ukiendelea kucheka na vichekesho lakini lisome ukipata muda usilidharau
Nguruvi3,
Mkuu Nguruvi heshima yako. Kwa uzoefu wangu wa jukwaa hili japo nilikuwa nasoma kama mgeni ila nimekusoma siku nyingi sana. Nakupongeza sana kwa kutoa challenge kwa maalim Mohamed Said ila lazima tukubaliane kuwa historia yetu inamapungufu makubwa na pengine niseme hayajatokea kwa bahati mbaya. Historia inakuwaga na chimbuko ili upate mtiliriko mzuri ila mengi hayajasemwa kwenye historia rasmi na ndo maana maalim yeye kajaribu kuleta yale anayojua, kama Taifa lazima tukubali kuandika historia yetu kwa usahihi kwa manufaa mapana ya jamii yetu.
Kolorama,
Umesema kweli kufutwa kwa majina katika historia ya TANU na
uhuru wa Tanganyika hakukuwa kwa bahati mbaya.
Lile jopo la waandishi wa Chuo Cha Kivukoni walikuwa wanafata
maelekezo waliyopewa vipi waandike historia ile.
Swali la kwanza la kuuliza ni nani huyu aliyetoa maelekezo ya vipi
historia ya TANU iandikwe?
Bila shaka atakuwa kiongozi mwenye nguvu sana ndani na nje ya
chama.
Katika jopo lile nilikuja kujuana na wajumbe wawili na wote makada.
Dr. Mayanja Kiwanuka na
Hassan Upeka.
Hassan
Upeka ni marehemu.
Huyu ni mtu wa Dar es Salaam na ni mtumishi wa kwanza kuajiriwa
na TANU 1956 alipomaliza darasa la 10 Tabora School.
Upeka alikuwa kachero wa TANU kastaafu miaka ya 1980 akiwa katika
kazi hiyo.
Hakuna kijana wa Dar es Salaam wa umri wangu aliyekuwa hamjui kaka
Upeka kwani akiogopewa kwa ile kazi yake.
Lakini hakupata kumnyayanyasa mtu yoyote kwa wadhifa wake ila nasikia
mara moja moja alikuwa akipita Mnazi Mmoja kuwatisha wauza bangi na
kuwaambia atawaletea polisi ikiwa wataendelea na kazi hiyo.
Vinginevyo alikuwa mtu mtaratibu na mkimya sana.
Labda ni kutokana na mafunzo ya kazi yake.
Upeka akinijua kama bwana mdogo tu lakini alipostaafu tukawa karibu sana.
Wakti huo mimi nishafanya mhadhara wangu wa kwanza Mnazi Mmoja na
kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru nikidai wazee wetu
wapewe heshima wanayostahili.
Cassette za mhadhara huu ziliuzwa kama maandazi ya moto.
Kila kibanda cha kuuza inawekwa na watu wamejazana wananisikiliza.
Kipindi hiki nishaandika ile makala ambayo gazeti zima lilikusanywa na
kutolewa katika mzunguko kwa sababu nilimtaja
Abdul Sykes kuwa muasisi
wa TANU.
Hili lilikuwa Africa Events likichapwa London.
Makala zangu kuanzia 1990 zikawa maarufu na zikivutia wasomaji wengi.
Africa Events na New African yote magazeti ya London yakinichapa.
Katika hali hii siku moja
Upeka aliniomba nende tukae faragha ofisini kwake.
Ofisi yake ilikuwa Mtaa wa Mvita, Karikaoo.
Upeka alinifungulia kifua chake kuhusu tatizo alilokutananalo wakati wa
kuandika historia ya TANU.
Akanieleza pia jinsi alivyomsaidia
John Iliffe wakati ule mwalimu wa historia
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kupata nyaraka za TAA na TANU zilizokuwa
TANU Office, Lumumba Street.
Akanieleza pia kuhusu ''notes,'' za
Abdul Sykes alizoandika katika mazungumzo
na yeye kuhusu historia ya TANU.
Upeka akanambia kuwa ''notes,'' hizi zilikataliwa na jopo.
Jopo liliamua kuandika historia ya TANU bila kumtaja
Abdul Sykes.
Nilimuomba ruhusu nitumie mazungumzo yetu katika kitabu cha
Abdul Sykes
na nitaje jina lake.
Upeka alinikubalia.
Upeka tulibaki marafiki hadi alipofariki mwaka wa 2010.
Sasa tuje kwa
Dr. Mayanja Kiwanuka.
Yeye ndiye aliyeandika barua ya kunitisha (
Africa Events, May, 1988, barua
ya
Dr K. Mayanja Kiwanuka) baada ya Africa Events kuchapa ile makala
yangu, ''In Praise of Ancestors,'' (
Africa Events, London, March/April, 1988,
September, 1988) ambayo kwa mara ya kwanza wasomaji walisoma kuwa
Abdul Sykes ndiye muasisi wa TANU.
Haya ni baada ya toleo zima la Africa Events kuondolewa katika mzunguko
kama nilivyodokeza hapo juu.
Nguruvi3,
Ndiyo nakuambia huna moja unalojua katika historia hii.
Yapo makubwa niliyozungumza na marehemu
Hassan Upeka.
Yeye alikuwa anajua kuwapo kwa historia ya TANU katika nyaraka za TANU
iliyoandikwa na
Abdul Sykes na
Dr. Wilbard Klerruu mara tu baada ya
uhuru.
Je, ungependa kujua nini kilitokea kwa mswada huu?
Kipi walikiona kimepungua au kimezidi katika mswada ule kiasi hadi leo si tu
haujachapwa lakini inaelekea umefichwa au kuchomwa moto?
Tusimame hapa.
Nakuwekeeni hapo chini picha ya maziko ya
Upeka nyumbani kwake
Mwananyamala: