Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Nguruvi3,
Nimekupa majibu.
 
ah!..........
 
Mkuu Nguruvi3 waswahili wanasema ukiwa mwongo basi usiwe msahaulifu.Ustaadhi Mohamed Said ni aina ya watu wenye vipaji vya utunzi na simulizi za hadith narudia tena hadith si kwa bahati mbaya la hasha vitabu vyake au majarida yake tayari yana conclusion anayoitaka yeye lau kama conclusion ikiwa tofauti basi ataiweka kando au ataidharau.

Ustaadhi Mohamed Said uandishi wake umejikita zaidi katika kuidhoufisha uhusiano baina ya Uislam na Ukristo.Anapenda sana kuonyesha picha kwamba waliopigania uhuru wa nchi yetu ni waIslam pekee yake.Nafasi za viongozi wa Kikristo enzi za utawala wa mkoloni anazififisha hadi unashangaa.Mfano Rais wa kwanza wa AA Cecil Matola laiti huyu mwanamama angekuwa si mgalatia sifa zake zingekuwa si haba katika majarida ya Ustaadhi Mohamed,utashangaa zaidi Rais hatajwi kwingi lakini Katibu kwakuwa alikuwa Ustaadhi mwenzake anamiminiwa sifa kibao.
 
Nguruvi3,
Nimekupa majibu.
 

Hizi nondo ni ngumu sana kujibiwa sana sana utaambiwa na wewe kaandike kitabu chako.
 
Ngongo,
Uwanja wa huu huru ikiwa na wewe unalo la kueleza ahlan wasaalan
andika tutasoma na ukiwa na picha zibandike tutaziangalia.

Hayo mengine nimeyasoma ni fikra zako na binadamu hatuwezi sote
tukawa na fikra sawa.
 
Mkuu mpungizie dozi mzee wetu ms sababu utamkimbiza bure kwenye mnakasha
 
maalim Mohammed anamwaga ukweli. watu hawataki....
Mkuu tusaidie kidogo, kati yake na Juma Mwapachu nani anasema ukweli? Wengine hatuna ufahamu

Pili, alisema Abdul kaandika katiba ya TAA, umeiona ile aliyoileta? Ndiyo katiba?

Tatu, kumwambia amwage ukweli, jina la TANU lilitumika wapi na lini kabala ya Nyerere hajaidhinisha?

Hatuna tatizo na historia kabisa, tuna tatizo na hesabu za historia yake zenye conclusion si kutokana na matukio bali hisia. Wengine wanaiita Histohisia

Lengo lake si kufuata mtiririko wa matukio, ni kumlenga mtu wake Nyerere ili abinafsishe historia ya nchi kwa familia tukufu.
Ndiyo maana akina Juma wanasema, a aa ! inatosha
 
maalim Mohammed anamwaga ukweli. watu hawataki....
Ukweli gani? acha kubwabwaja ovyo hapa tatzo mmezoea kudanganya sana sasa leo kiongozi Nguruvi3 anasahihisha urongo wenu mnabaki kubwabwaja na kutoa lugha za kukera
 
Hizi nondo ni ngumu sana kujibiwa sana sana utaambiwa na wewe kaandike kitabu chako.
Ngongo,
Kuna wakati nikiwaambia hivyo kwa kuwa nilidhani mna uwezo
wa kuandika kitabu.

Majibu natoa zaidi ya majibu.
Nakupeni majibu lakini si yale ambayo nyie mnapenda.

Pili katika majibu naangalia na wasomaji wengine na ili nisiwafunge
kila inapotokea nafasi nakuja taaifa mpya.

Hivi ndivyo ninavyoweza kuufanya uzi huu upendenze na watu wengi
wajazane kuja kutusikiliza.

Ungelijuaje kama magazeti ya TANU yalikwepa kuandika taazia ya Abdul
alipofariki mwaka wa 1968.

Ungelijuaje kama magazeti ya Africa Events yalikusanywa yasisomwe kwa
kuandika kuwa Abdul Sykes ndiye aliyeasisi TANU.

Ungejuaje kuwa Hamza Mwapachu alitaka sana Nyerere aongoze harakati
za kudai uhuru na maneno haya anamweleza Abdul Sykes.

Upande mmoja huenda nyie hamridhiki na kalamu yangu lakini kuna watu
hawaishi kunipongeza kwa kuwapa elimu bila khiyana.

Maalim wangu wa madras Sheikh Haruna akisema,''Tunakufundisheni ilm
hii ili waja wa Allah wafaidike na nyinyi. Hatuwafundishi mkataabishe watu.''

Ndiyo maana mimi na nyinyi leo tunajadili na mimi najitahidi kuwapeni ilm
ambayo kabla hamkuwanayo.
 
Siyo ilm tu umesema tunasahihisha makosa ya kivukoni, tukakubaliana.

Unaporudia makosa ya kivukoni kwa mlango wa nyuma inatisha kuliko kivukoni.

Ushajua ni makosa halafu unatenda makosa, ina maana umedhamira si bahati mbaya

Lakini MS kwa wengine kusoma kama hadithi ni njema, kwa baadhi yetu tunasoma kama comprehension ili tuweze kuunganisha dots

Ndiyo maana tunakuuliza

Kati ya sauti yako katika radio na kauli ya Juma Mwapachu tunasimama wapi?

Nyerere alijulikana TAA au hakujulikana kama unavyosema?

Lakini pia umehamisha goli kwa Platan, tunasema hakiharibika kitu

Je, uongozi wa TAA haukumhusu Abdul Sykes?

Upo tayari kuomba radhi radio Nur kwa upotoshaji wako?

Upo tayari kutuomba radhi kwa ubabaishaji wa kutumia historia?

Hakuna either way, ni uombe radhi tu ndilo litanusuru heshima yako

Sauti ya Mohamed Said, na maneno ya Juma Mwapachu yanafuata
 
Hizi nondo ni ngumu sana kujibiwa sana sana utaambiwa na wewe kaandike kitabu chako.
Nshaambiwa twende mbele tuachane na hayo!

Kwamba twende tuu hata kama darsa ya Mudeer Mohamed ina tatiza.

Tunatakiwa tukae kitako na kushangilia tu! go mudeer go, hurreeee! bravo

Mtu anapokwenda kwenye radio kusema uongo, inahitaji tufikiri kidogo
 
Mzee wetu ms waweza jibu maswali ya Nguruvi3 kabla atujaendelea na mnakasha?
 
Hakika Faiza kichwa chako kimejaa pumba cz mkuu hapo juu kaomba msamaha lkn wwe jinsi ulivyokua punguani unamtaka aombe msahama tena Ficha uzembe wako

Soma alichokiomba msamaha kipi na alichozua kipi, ukiweza vinukuu vyote na ukishindwa uje useme nani ni punguani zaidi yako.
 
Nguruvi3,
Mgumu sana kuelewa.
Hiyo si katiba ya TAA.

Walichoandika TAA Political Subcommittee nakuwekea hapa ingawa
nilikupa rejea nikakwambia ukimsoma Listowel (1965), Pratt (1976)
utapata kila kitu.

Hawa ndiyo watu wa kwanza kuileta katiba ile hadharani.

Mimi nimekuja baadae (1998) lakini kwa staili nyingine ya kwenda
nyuma ya wale wajumbe na kueleza uhusiano wao na umma waliokuwa
wanauongoza.

Nimeeleza kwa nini Abdul Sykes alimtia Sheikh Hassan bin Amir katika
siasa za TAA.

Kwa nini alimtia na Said Chaurembo katika siasa za TAA.
Huyu alikuwa kaka yake Sheikh Abdallah Chaurembo.

(Sheikh Abdallah Chaurembo alikuja kuwa mtu muhimu sana katika siasa
baada ya uhuru kupatikana).

Ana kisa kikubwa sana.
Kwa nini alimleta Earle Seaton kama mshauri wa sheria katika TAA nk. nk.

Wewe umeshikilia kuwa ni katiba ya TAA na unarudia mara kadhaa huku ukidai
sijibu maswali yako.

Hii ilikuwa katiba ya Tanganyika chini ya Gavana Edward Twining katiba
ambayo Twining aliikataa.

Huyu gavana ndiye aliyeomba mapendekezo vipi nchi itawaliwe kutoka kwa
watawaliwa.

Document hili limepotea halipo kokote.
 
Nshaambiwa twende mbele tuachane na hayo!

Kwamba twende tuu hata kama darsa ya Mudeer Mohamed ina tatiza.

Tunatakiwa tukae kitako na kushangilia tu! go mudeer go, hurreeee! bravo

Mtu anapokwenda kwenye radio kusema uongo, inahitaji tufikiri kidogo
Nguruvi3,
Mimi si muongo.

Nimeiandika historia ya TANU kwa kadri Allah alivyoniwezesha
kiasi hata hao wahusika wenyewe waliokuwa TAA na TANU
wamenipongeza.

Prof. Haroub Othman hakuniita muongo yeye kataka kusikia
upande wa pili wanasemaje.
 
Mkuu mpungizie dozi mzee wetu ms sababu utamkimbiza bure kwenye mnakasha
Wembeee,
Mimi nikimbie kwa kipi kitakachonitisha hapa jamvini?
Hebu tufahamiane:

PUBLICATIONS/RESEARCH PAPERS/ARTICLES
1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.
2. The Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press 2006, Nairobi. (Children’s book).
3. Contributing author for an African anthology: The Mermaid of Msambweni and Other Stories, Oxford University Press 2007, Nairobi.
4. Contributing author Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press 2011, New York.
5. Uchaguzi wa Busara, Abantu Publications 2008, Dar es Salaam.
6. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London).
7. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London).
8. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
9. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
10. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
11. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
12. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
13. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
14. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA)Morogoro 11th April 2004).
15. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
16. Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma bin Khamis (1940 – 1994) and the Pork Riots of 1993. (Paper Presented at the Regional Conference on Islam in Eastern Africa: Islam Encounter with the Challenges of the 21st Century 1st - 3rd August 2006, Kenyatta University, and Nairobi.
17. Muslim Bible Scholars of Tanzania – The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (1918 – 2005) Paper Presented at the International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa Organised by The Organisation of Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA) The National AWQAF Foundation of South Africa (AWQAF SA 1 – 3 September 2006 University of Johannesburg. The paper was also presented at Islamic Propagation Centre International (IPCI) Durban.
18. Tanzania: A Nation Without Heroes Seminar Organised by IFRA French Institute for Research in Africa and BIEA British Institute in East Africa 23rd and 24th September 2013 at IFRA Nairobi.

19. Awards: Several Awards.
20.Board Member Radio Kheri
21. Visiting Scholar: (2011)
University of Iowa, Iowa City, USA
Northwestern University, Chicago, Illinois, USA
Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
 
maalim Mohammed anamwaga ukweli. watu hawataki....
Myoyambendi,
Allah ana njia zake za ajabu kabisa.

Leo hii mimi nimepata hadhira ya bure naisome nikiwa nimekaa
kitako nyumbani kwangu.

Hivi sasa achilia mbali wanaonisoma JF blog yangu inasomwa
kwingi duniani na watu wa kawaida na watafiti.

Napokea simu nyingi sana.
Historia hii imeathir watu wengi sana.

Lakini mengi nisingeweza kuandika kama si kuulizwa na watu kama
Nguruvi3 na Ngongo.

Kwangu mimi hawa watu ni muhimu sana na ndiyo maana nawaweka
katika blog yangu ili watafiti wawasome na wajue fikra za wale ambao
kwa miaka walikuwa wanasomeshwa historia rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…