Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Mi sio kinda wa mtu yyte yule sababu natumia akili kuhoji sio kama nyie kila neno mnapanua mdomo na kumeza paspo kuchagua zipi pumba hupi mchele mwisho wa siku mnameza sumu paspo kuhoji
Wembeee,
Ingekuwa mimi naandika maneno mabaya uliyoyaita ''sumu,''
unadhani ningepata heshima ya kualikwa kuzungumza kwingi
katika makongamano na mikutano ya kimataifa?

Ingekuwa wewe hodari wa wa kuchambua ungeliamini kwa
miaka hiyo yote historia rasmi inayotambuliwa nchi nzima?

Je, ulimjua Abdul Sykes kabla ya leo?
Nimeuliza swali hapa leo siku ya tatu nyote meogopa kujibu.

Nimesema baada ya magazeti ya TANU kupiga kimya kuhusu
taazia ya Abdul Sykes, Brendon Grimshaw mhariri wa
Tanganyika Standard alimuadikia Abdul taazia na ikachapwa.

Nimekuulizeni mngependa kujua Grimshaw alisema maneno
gani kuhusu Abdul?

Kama wewe hodari wa kuchambua iweje hadi leo hujajiuliza
kwa nini wazalendo wengi walifutwa katika historia ya TANU
na uhuru?

Nauliza tena.
Mngependa kujua alichoandika Grimshaw kuhusu Abdul Sykes?
 
Mudeer Ramadhan Kareem...

Tupo hapa tunafyonza ilm tartiiibuu kabisa...

Ima kwa niaba yetu na wengineo wenye uchu wa kutaka kujua wewe endelea tuh kumwaga nyukiii...

Tunajua hawapendi ukweli ukiwekwa lakin wavumilie tuuh ndivyo haqqi ilivyo.

Nan aliwajua hawa katika historia ya kupigania uhuru wa nchi hii?...

Iweje sasa historia yao ikiwekwa bayana wao washikwe na maumiv ya moyo...

Historia lazima iandikwe.
 
Shukrani Mzee wetu Mohameid Said, maana hata mkondo wa Marxism hawaamini historia ni Zao la mtu mmoja kama tulivyoaminishwa na Nyerere bali ni Jamii ya wengi.
Mwenyezi Mungu akupe umri mrefu zaidi kwa sie vijana wako tuendelee kukusoma kwa uzuri zaidi.
 
Stata Mzuka,
Allahuma Amin.
Tumshukuru Allah kwa kutuongoza kufikia haya yote.
 
Aksante kwa hayo Mach
Aksante kwa hayo machache...!
 
Maalim ms naomba usome bandiko langu vzr afu ntakua na maswali juu yako juu ya Nyerere

Mwaka 1949 alipata [[skolashipu[[ ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Uskoti, Ufalme wa Muungano, akapata M.A. ya historia na uchumi (alikuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanganyika).

Aliporejea kutoka masomoni, alifundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.

Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.

Mwaka 1954 alibadilisha jina la chama cha TAA kwenda chama cha Tanganyika African National Union (TANU), ambacho pia kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kikawa tayari chama cha siasa kinachoongoza nchini Tanganyika.

Uwezo wa Nyerere uliwashtua viongozi wa kikoloni akalazimika kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

Alijiuzulu ualimu na kuzunguka nchi nzima ya Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta umoja katika kupigania uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship Council na Fourth Committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York.

Uwezo wake wa kuongea na wa kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu.

Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo, Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960.
 
Aksante kwa hayo Mach

Aksante kwa hayo machache...!
Ndakilawe,
Iko siku nilialikwa chakula cha jioni Kilimakyaro Moshi.
Nilijikuta katika kundi la jamaa wengi wa Kichagga.

Niliwapa stori za Chief Marealle na Abdul Sykes.
Hawa jamaa walifurahi sana.
 
Huyo Said Mohamed na yeye anajulikana mpaka huko Hong Kong or AU?
 
Wembeee,
Wala sihitaji kusoma.

Hakuna kitu kuhusu Nyerere ambacho sikusoma wakati nafanya
utafiti.

Sehemu kubwa ya utafiti wangu nilifanya nikiwa mwanafunzi Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.

Maktaba ya Chuo Kikuu imejaa hazina kubwa kuhusu Nyerere.

Niliposoma mstari wa kwanza tu nishajua wapi ''passage,'' hiyo ilikotoka.
Nasubiri maswali.
 
Wembee,

Unajua hii kitu?

In other words, plagiarism is an act of fraud. It involves both stealing someone else's work and lying about it afterward.

Unaposema ni bandiko lako ni kuwadanganya wanaukumbi ni vyema ungesema umelipata wapi ili bandiko.

Ahsanta!
 
Ritz,
Tumchukulie hakukusudia kutenda hilo.
Huenda maana yake ni lake kwa kuwa kaliweka yeye.

Nasubiri maswali yake kuhusu Nyerere.
 
Nami nasubiri kujifunza ...!
 
Hiyo picha inaonyesha huo ukoo wa kina Sykes ulikuwa na fedha sana mwaka 1942 Ally amevaa suti na tai!

Na ni watunzaji wazuri wa nyaraka na picha.
Halafu huyo askari amevaa kofia upande duh!
 
Kaka,
Sote hapa ni wanafunzi tunajifunza kwa yeyote atakaekuja na jipya.
Nguruvi3,
Kuna mahali umesema kwa kejeli sana na hii ni bahati mbaya kwako, kuwa
Abdul siasa zake ziliishia Kariakoo.

Nilikupa jibu lakini bahati mbaya kwangu sikuweza kupata rejea kwa wakati
niziweke jamvini kwa manufaa yetu sote.

Nimeipata rejea moja na nakuwekea hapa usome ili uijue vyema historia ya
TANU:

TANGANYIKA POLITICAL INTELLIGENCE SUMMARY, MARCH 1952


A passenger reading Abdul Sykes book inside a boat traveling to Zanzibar
(Photo taken by Abdulwahid Sykes' grandson of Abdul Kleist Sykes)



"Tanganyika Political Intelligence
Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has
dispatched letters to all branches asking members for suggestions under
the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal
Commission..."

“...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as
reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up
country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the
Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then
visited Kampala alone.....on 8th March, a secret meeting was held, attended
by leading members of the Mwanza Branch...”

(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.)


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…