Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #461
Wembeee,Mi sio kinda wa mtu yyte yule sababu natumia akili kuhoji sio kama nyie kila neno mnapanua mdomo na kumeza paspo kuchagua zipi pumba hupi mchele mwisho wa siku mnameza sumu paspo kuhoji
Ingekuwa mimi naandika maneno mabaya uliyoyaita ''sumu,''
unadhani ningepata heshima ya kualikwa kuzungumza kwingi
katika makongamano na mikutano ya kimataifa?
Ingekuwa wewe hodari wa wa kuchambua ungeliamini kwa
miaka hiyo yote historia rasmi inayotambuliwa nchi nzima?
Je, ulimjua Abdul Sykes kabla ya leo?
Nimeuliza swali hapa leo siku ya tatu nyote meogopa kujibu.
Nimesema baada ya magazeti ya TANU kupiga kimya kuhusu
taazia ya Abdul Sykes, Brendon Grimshaw mhariri wa
Tanganyika Standard alimuadikia Abdul taazia na ikachapwa.
Nimekuulizeni mngependa kujua Grimshaw alisema maneno
gani kuhusu Abdul?
Kama wewe hodari wa kuchambua iweje hadi leo hujajiuliza
kwa nini wazalendo wengi walifutwa katika historia ya TANU
na uhuru?
Nauliza tena.
Mngependa kujua alichoandika Grimshaw kuhusu Abdul Sykes?