Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

samahani swali langu liko nje ya mada kidogo. nauliza je, ni wewe mzee mohamed said ndiye uliyetunga kitabu cha NYOTA YA REHEMA?
 
Hapo ndio utaona tofauti ya kiongozi na mtawala mungu amuweke mahala pema peponi yy pamoja wazee wetu wengine mshume kiante mwijuma kambi hamza mwapachu juma mzee jumbe ally kirro mama daisy bibi titi mohamed said tewa nk
 
Ni muhimu sana kuzihifadhi historia za watu mbali mbali walio na umuhimu katika historia ya Tanzania. Na moja ya hayo ni mchango mkubwa anaoufanya mzee Mohammed Said kwa utafiti mbali mbali ikiwa na pamoja na kukaa na kuzungumza na wazee walio kuepo wakati huo na kurekodi maelezo yao ambayo vinginevyo yatapotea pindi hawa wazee watakapo fariki.

Mambo na matukio mengi muhimu ya kihistoria hayaku haririwa ipasavyo kwa sababu mbali mbali zikiwamo za kisiasa.
 

Kwezisho umenishangaza, tatizo naona lipo kwenye story za mitaani ambazo msingi wake sio mzuri sababu hizo unazo taka kuamini hazina proof yoyote. Mwenzio kufanya utafiti na kakujibu swali lililoulizwa wewe hutaki kuamini! sema unachoamini ulekebishwe Mkuu! Kumbuka wazee wetu waliopigania uhuru wengi hawakuwa na uchu wa madaraka. Kiu yao Kubwa ilikuwa ni kumuondoa mkoloni! Hivyo madaraka baada ya uhuru kwao haikuwa ishu sana kama unavyoshangaa Abdul Sykes kutokuwa kwenye safu ya uongozi. Kwake yawezekana haikuwa ishu ilimladi mkoloni kuondoka basi. Tuheshimu tafiti tusipende Kuongea pasipo kutafiti
 
Daaa kwahiyo Nyerere aliibuka Kuwa mwenyekiti wa TANU kama JPM alivyo ibuka kugombea na kuwa Rais wa JMT yaani hawakuwa walengwa ...
Kajembejr,
Mwalimu Nyerere
hakuibuka.

Mwalimu Nyerere tayari katika maisha yake toka udogo alionyesha
uwezo wa akili ambao haukuwa wa kawaida.

Hamza Mwapachu ambae walikuwa wote Tabora School na Makerere
alikuwa anaujua vyema uwezo wa Nyerere na ndiyo sababu alimuomba
Abdul amchukue Nyerere katika TAA kwenye safu ya uongozi hapo HQ
New Street.
 
Mkuu samahani sana, swali lilikuwa hivi:
Kwanini Abdul hakupewa cheo kikubwa serikalini
Nawe wasema hivi:
Uncle Jei Jei, mie naheshimu sana tafiti za kihistoria nawe pia umeniongezea kitu kwa kusema kiu kubwa ya wazee wetu ilikuwa ni kumuondoa mkoloni. Ila kidogo naomba kutofautiana nawe kwamba, watu waliojumuika na Julius Nyerere baada ya kuikomboa Tanganyika walikuwa na "uchu wa madaraka".
Hili neno uchu wa madaraka linanipa ukakasi na kunikwaza na hata mtafiti wetu Mzee Mohamed Said hapendi kulitumia katika hoja zake. Mzee wetu, Mohamed Said ni gwiji na hazina yetu hilo sote tunaliafiki.
Mimi nilitaka kufahamu kwa nini Abdulwahid Sykes na kizazi chake hawakutaka kujumuika na Julius Nyerere kama ilivyo kwa Mwapachu na familia yake? Je kuna kitu cha ziada au kina Sykes walikuwa na kiu ya kumuondoa mkoloni kisha hawakutaka kulijenga taifa walililolipigania? Yawezekana zipo sababu nyingine za ziada, hebu tujaribu kumdadisi na kumfikirisha Mzee Mohamed Said aendelee na utafiti wake ili aje atujuze.
 
Kwezisho,
Unasema yawezekana zipo sababu nyingine zaidi.
Ndiyo inawezekana zikawepo sababu nyingine zaidi.

Mimi nimejitahidi kujibu kadri ya uwezo na ufahamu wangu.

Na ni vizuri katika utafiti wowote ikaachwa nafasi ya mtafiti
mwingine kueleza yale ambayo mtafiti wa mwanzo labda kwa
sababu za kibinadamu zimempita.

Wenye taarifa zaidi ya historia ya kipindi kile wanaweza na wao
wakajazia pale ambapo mimi nimeishia.

Huenda kwa majibu ya wengine ikawa hiyo kiu ikakatika.

Kuhusu shida uinayo kuhusu jibu langu wala hapana haja ya wewe
kupata hiyo shida.

Nichukulie mimi kama mtu wa kawaida mwenye kikomo cha uwezo
na kwa ajili hii ipo nafasi kubwa sana ya kukosea.

Umetumia neno ''kususa'' na ''kukataa.''

Katika utafiti wangu sikukumbana na hali yoyote iliyoonyesha kuwa
Abdul ''alisusa'' au ''kukataa.''

Abdul kama walivyokuwa wenzake wengine katika wale wafadhili
wakubwa wa TANU waliendelea kukisaidia chama hadi uhuru 1961.

Hilo swali la kwa nini Nyerere hakupenda kuwatumia akina Sykes
kama alivyowatumia akina Mwapachu hili swali lako halijakaa vyema.

Halijakaa vyema swali lako kwa sababu sasa hapa unakuja kwa watoto
wa Hamza Mwapachu na watoto wa Abdul na Ally Sykes.

Swali hili lingemstahiki Mwalimu Nyerere mwenyewe kulijibu.
Mimi siwezi kumsemea.
 
Mzee wangu nashukuru sana kwa jibu lako. Na vyema tukawapa fursa watafiti wengine wakaendelea pale ukomo wetu ulipofikia. Ila kwa ufahamu wangu, unayo mahusiano mazuri sana na hii familia ya Sykes, sio vibaya kuwauliuza labda wanaweza kutufahamisha.
 
Kwezisho,
Baada ya ufafanuzi huu wako sasa nimekuelewa.
Labda nami nijibu swali lako kwa kukuuliza swali.

Naamini umesoma historia ya TANU na uhuru wa
Tanganyika kuna mahali popote ametajwa Abdul?

Unasema Abdul hakutaka kujumuika na Nyerere.

Kwa nini isiwe labda Nyerere hakupenda kujumuika
na Abdul?

Lakini katika kundi hilo hakuwa Abdul peke yake.

Alikuwapo Sheikh Hassan bin Amir vile vile ambae
pia alitoa mchango mkubwa wa kukiongoza chama
vizuri na kumpa ''support'' kubwa Nyerere kati ya
1954 - 1961.

Iweje Nyerere alikuwa kimya kuhusu watu hawa
kama vile hakupata kujuananao?

Sasa hapa msiniachie mimi nifikiri peke yangu sote
tupige kichwa kufikiri.
 
Alhabyb Mohammed Said naomba nikuite jina hili kuanzia Leo "gurudumu la tarekh" hakika ww ni gogo Al bahri mashallah
 
Mzee wangu nashukuru sana kwa jibu lako. Na vyema tukawapa fursa watafiti wengine wakaendelea pale ukomo wetu ulipofikia. Ila kwa ufahamu wangu, unayo mahusiano mazuri sana na hii familia ya Sykes, sio vibaya kuwauliuza labda wanaweza kutufahamisha.

Kwezisho,
Nasikitika kukufahamisha kuwa baada ya mimi kuandika
kitabu cha Abdul Sykes kumeingia ''disinterest'' kwa hii
historia ya Nyerere kwetu sote.

Nyerere amekuwa sasa si muhimu tena baada ya ukweli
kujulikana katika historia ya AA, TAA na TANU.

Na nadhani baada ya Abdul na Ally Sykes kupewa nishani
katika kumbukumbu ya miaka 50 wa uhuru wa Tanganyika
kutambua mchango wao katika kupambana wa ukoloni sasa
hakuna tena jipya.

Imekuwa kama vile katika ''show,'' pazia limeshushwa.
 
Nashukuru kwa kunielewa. Mimi ni msomaji wa historia na nimeisoma historia ya TANU na nimebahatika kuvisoma baadhi ya vitabu vya Nyerere. Ila hili suala linanitatiza sana na kwa bahati mbaya hakuna majibu. Wengi wanajiuliza na hawapati kiini cha kujitoa (kususa?) kwa familia ya Sykes baada ya kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika.
 
Alhabyb Mohammed Said naomba nikuite jina hili kuanzia Leo "gurudumu la tarekh" hakika ww ni gogo Al bahri mashallah
Alhabib Bafa,
Ngoka nikueleze kitu.
Wallahi nakuapia si kama mimi ni mjanja kushinda wengine.

Bahati iliyonikuta mimi ni kuwa nimezaliwa na watu hawa na
kwa wakati ule.

Haya yanatendeka yanatendwa na watu ambao wazee wangu
wakiwajua na mimi nikaja kuwana kwa macho yangu.

Na yapo yaliyokuwa yakizungumzwa mimi mdogo nayasikia
ingawa haikunipitikia kuwa nilikuwa nashuhudia kitu kikubwa
sana katika historia ya Tanganyika.

Mimi nina picha alinipiga Mzee Shebe mwaka wa 1952 au 1953.
Huyu Mzee Shebe akaja kuwa mpiga picha wa TANU na Nyerere
wakati wa kudai uhuru.



Siku mama yangu alipokuja kunambia historia ya picha ile nilishtuka.

Mzee Shebe
alinipiga picha ile katika studio yake iliyokuwa Mtaa wa
Livingstone na Kipata.

Alhabib,
Ahsante kwa kunitunuku jina.
 
Kwezisho,
Abdul Sykes hakupata kumsusa Nyerere hata siku moja.

Ikiwa umesoma kitabu changu utakuwa umesahau baadhi
ya vitu na hii ndiyo sababu unahangaishwa na hii ''kususa,''
au ungependa kuwa Abdul awe kasusa.

Mimi tabu mtu kunichokonoa.
Huwa siingii kwenye tundu nabaki mlangoni.

Rejea kwenye kitabu cha Abdul Sykes na soma Sehemu
ya Tatu ya Kitabu.

Uhuru ushapatikana 1961.
Palipitika majambo.

Soma kisha rejea katika mjadala.
Usiandikie mate na wino upo.
 
Ukiongelea tanu na taa..bila kumtaja abdul sykes ..ni sawq ni sawa na kuongelea mapinduzi bila kumtaja che guevara..

Pumzika kwa amani mzee wetu abdulwaheid sykes
Escotter,
Allahuma Amin.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…