Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 3,135
- 3,392
Nyerere alifanikiwa kuwafukuza wakoloni, hakuna asiyefahamu msimamo wa Nyerere dhidi ya mataifa ya Ulaya na Marekani na hata kwa baadhi ya Mataifa au Viongozi wa Afrika walioonyesha kutumiwa na hao wamagharibi. Alionekana hadharani akiwapinga waziwazi, hivi kwa akili yako unadhani leo akitokea "KANJANJA" mmoja anayetaka kumshusha hadhi Nyerere wataacha kumuunga mkono!? Hivi unadhani wataacha kumpigia nyimbo za pongezi! Wao wenyewe hawampendi kwa sababu alikuwa mwiba kwao hadi mauti yanamkuta! Hivyo mialiko hiyo inawezekana kabisa na nidhihaka kwako kwa kutotaka kuthamini mtu aliyewatoa jasho! Hivi kwa akili yako, hao kina Sykes unaowatukuza walishindwa nini kwenda wao kama wao huko kwa Malkia!? Hivi ni akili nzuri kweli kutaka kuwaweka mizani Sawa na Kambarage!? Wao walishindwa nini hata kumbembeleza ajiunge nao!? Nani anafahamika kimataifa!? Wataachaje kukualika wakati unajaribu kumshasha mtu ambao wao wenyewe wanatamani hata asitamkwe kwa sababu aliwawekea kauzibe!? Ukombozi wa Tanganyika ulianza siku mkoloni alipoingia Tanganyika na wala haukuasisiwa na hao kina Sykes unaotaka tuwaabudu!! Nani asiyefahamu kuwa kina Bwana Heri walinyongwa sababu ya kudai uhuru!? Nani asiyefahamu Kuwa kina Chief Mirambo, Mkwawa wote hao hawakumtaka mkoloni!? Hao kina Sykes ni kina nani hasa hadi unatulazimisha kwa nguvu zote tuwaabudu!? Hivi, hujui kuwa mtoto anaweza kuwa maarufu kuliko baba!? Hujui kuwa mtoto anaweza kupata mafanikio makubwa kuliko baba!? Obama ni Rais wa Marekani, historia itamkumbuka yeye au baba yake!? Hitler aliusumbua huu ulimwengu miaka ya 1939 - 1945, historia inamkumbuka baba yake au yeye!? Wewe unataka tumshushe hadhi Nyerere eti pazia limeshushwa, tumlaumu baba yako aliyejinyima ukapata hiyo elimu unayotaka kuitumia vibaya au tukulaumu wewe!? Nyerere alikibeba Chama baada ya kuingia hivyo lazima historia itamkumbuka tu! Hao kina Sykes ni kama WAZAZI wanaofurahia matunda yaliyo letwa na kijana Nyerere waliyemkaribisha chamani kama baba anavyojivunia mafanikio ya mwanae!!
Uncle Jei Jei:
Tatizo Nyerere si muislam kwa dini wala mmanyema kwa kabila.
Na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa na AMNUT.