Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Nyerere alifanikiwa kuwafukuza wakoloni, hakuna asiyefahamu msimamo wa Nyerere dhidi ya mataifa ya Ulaya na Marekani na hata kwa baadhi ya Mataifa au Viongozi wa Afrika walioonyesha kutumiwa na hao wamagharibi. Alionekana hadharani akiwapinga waziwazi, hivi kwa akili yako unadhani leo akitokea "KANJANJA" mmoja anayetaka kumshusha hadhi Nyerere wataacha kumuunga mkono!? Hivi unadhani wataacha kumpigia nyimbo za pongezi! Wao wenyewe hawampendi kwa sababu alikuwa mwiba kwao hadi mauti yanamkuta! Hivyo mialiko hiyo inawezekana kabisa na nidhihaka kwako kwa kutotaka kuthamini mtu aliyewatoa jasho! Hivi kwa akili yako, hao kina Sykes unaowatukuza walishindwa nini kwenda wao kama wao huko kwa Malkia!? Hivi ni akili nzuri kweli kutaka kuwaweka mizani Sawa na Kambarage!? Wao walishindwa nini hata kumbembeleza ajiunge nao!? Nani anafahamika kimataifa!? Wataachaje kukualika wakati unajaribu kumshasha mtu ambao wao wenyewe wanatamani hata asitamkwe kwa sababu aliwawekea kauzibe!? Ukombozi wa Tanganyika ulianza siku mkoloni alipoingia Tanganyika na wala haukuasisiwa na hao kina Sykes unaotaka tuwaabudu!! Nani asiyefahamu kuwa kina Bwana Heri walinyongwa sababu ya kudai uhuru!? Nani asiyefahamu Kuwa kina Chief Mirambo, Mkwawa wote hao hawakumtaka mkoloni!? Hao kina Sykes ni kina nani hasa hadi unatulazimisha kwa nguvu zote tuwaabudu!? Hivi, hujui kuwa mtoto anaweza kuwa maarufu kuliko baba!? Hujui kuwa mtoto anaweza kupata mafanikio makubwa kuliko baba!? Obama ni Rais wa Marekani, historia itamkumbuka yeye au baba yake!? Hitler aliusumbua huu ulimwengu miaka ya 1939 - 1945, historia inamkumbuka baba yake au yeye!? Wewe unataka tumshushe hadhi Nyerere eti pazia limeshushwa, tumlaumu baba yako aliyejinyima ukapata hiyo elimu unayotaka kuitumia vibaya au tukulaumu wewe!? Nyerere alikibeba Chama baada ya kuingia hivyo lazima historia itamkumbuka tu! Hao kina Sykes ni kama WAZAZI wanaofurahia matunda yaliyo letwa na kijana Nyerere waliyemkaribisha chamani kama baba anavyojivunia mafanikio ya mwanae!!

Uncle Jei Jei:
Tatizo Nyerere si muislam kwa dini wala mmanyema kwa kabila.
Na kibaya zaidi, baba wa mwandishi huyu, aliwahi kuwekwa rumande na serikali ya Nyerere baada ya kuleta chokochoko za kidini zilizoanzishwa na AMNUT.
 
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.
 
Reading between lines, dhamira yako ya kumdharaulisha Nyerere bado inaendelea.
Nyerere "alimtiaje" ndani chief David Kidaha?
Je ni sahihi kuandika historia ya sasa kuhusu Sheik Ponda kuwa alipigwa risasi na Kikwete, kwa vile tu tukio lilitokea wakati utawala wa Kikwete?
Mkuu lengo ni hilo , kwanza kumdhalilisha Nyerere halafu kujenga hoja.

Unaweza kumsoma akisema '...Nyerere si muhimu tena' hilo tu linaonyesha nia aliyo nayo ya kutaka kumuonyesha Nyerere hana kitu

Na katika kushadidia hilo, bandiko la Uncle Jei Jei alitoa hoja kuwa wanahistoria wa kawaida ni rahisi kuwasahau 'initiator' wa harakati za uhuru''

Mohamed Said akasema si kweli na hakuna ushahidi wa kisomi, akimaanisha si kweli kuwa historia ina favor Nyerere kwa nyadhifa alizoshika licha ya ukweli kuwa wapo waliopigania na kuandaa mazingira mapema kabla yake

Tunaweza kuona mifano michache ya kushadidi hoja ya Uncle Jei jei na mantiki yake
1. Utasikia Abdul Sykes ndiye alifanya ABCD katika harakati za uhuru.

Hayo yanayosemwa ameyafanya miaka ya 1948. Tukirudi nyuma , kuna mtu asiyetajwa ambaye kwa mujibu wa uncle jei jei ndiye 'initiator' wa harakati za karibuni (1900)

Huyu ni mwalimu Ceci Matola, mwenyekiti wa kwanza wa AA akiwa na katibu wake Sykes
Vipi Abdul Sykes anaweza kuwa nyota kuliko Cecil Matola?
Na kwanini Nyerere asiye nyota kuliko Abdul Sykes?

Pili, leo tunazungumzia Nelson Mandela wa ANC. Chama hicho kilianzishwa miaka 1915 na akina Dube na Plaatje. Kilibadilika na kuwa ANC mwaka 1923 Mandela akiwa mtoto wa miaka si michache sana.

Nyota ya Mandela iling'aa wakati wa Umkhonto Weswize kama ilivyokuwa kwa Abdul

Nani anawajua akina Govan Mbeki, Oliver Tambo au Ahmed Kathrada Zaidi ya Mandela?

Tatu, India anajulikana Gandhi. Huyu alifanya shughuli zake kule Afrika kusini hata Mandela hajazaliwa ingawa si mwanzilishi wa harakati za uhuru wa India.

Leo nani anajua mwanaharakati mwingine Zaidi ya Gandhi?

Kwa mifano hiyo ni wazi kuwa historia yetu itamtaja Nyerere kama ilivyowataja akina Mandela, Gandhi n.k. Iweje basi wawepo wenye vinyongo dhidi ya Nyerere kuwa superior kwa Abdul Sykes na si Cecil Matola?

Historia haitungwi au kurithishwa,inajieleza. Katika kujieleza huko kuna ''spikes'' mbazo hutokea bila kuandaliwa.

Kujaribu kuzifuta ni ku disturb equilibrium ya equation na hapo ndipo kunazuka tatizo.

Tatizo ni kama hili alilolileta Mohamed la kuweka Nyerere na Abdul katika mizani ili kumdharaulisha Nyerere kwa kauli kama 'pazia la show yake limeshushwa'

well, tunamwangalia Abdul Sykes na kugundua mengine , kwa mfano

1. Tunajua Sykes wote hawaku modernize siasa katika kiwango cha Nyerere

Tumesema Nyerere kaandika katiba ya chama cha siasa ya kwanza.
Goli linahamishwa alikopi kutoka kwa Nkrumah. Tukiangalia Zaidi, Sykes wote hakuna aliyewahi kuandika au kukopi mwongozo wa chama. MS kashindwa kuleta ushahidi

2. Tunaambiwa TANU ilianza Burma. Tumeomba ushahidi mmoja tu wa mkusanyiko uliowahi kutumia jina la TANU kabla Nyerere haja rasmisha chama kuwa TANU. Hakuna

Kuwa na jina mfukoni na kulitumia jina practically ni vitu tofauti. Hawakubali

Lakini pia MS anakwepa ukweli kuwa Abdul hakuwepo katika uongozi baada ya uhuru

Kilichomtimua Sheikh Amir ni harakati za misikitini dhidi ya Nyerere.
Hizi ziliungwa mkono na wengine. Baada ya chaguzi za chama wapo waliopoteza umaarufu. Hawa wakahamisha harakati za ukombozi wa nchi kuwa za kidini

Wakitaka kumuondoa Nyerere kupitia siasa za misikitini, na kama mtawala Nyerere hakukubali hilo. Unaweza kumsoma MS anaposema waislam ndio wamepigania uhuru wa chi hii. Hapa kuna reservations ambazo huziweka wazi katika nyuzi nyingine

MS anaposema Nyerere kamtimua sheikh Amir, lengo ni kuonyesha alivyowachukia waislam. Hatoi sababu akijua zitapingana na dhana ya uhuru. Ni katika kumdhalilisha

Na ukimsoma MS hatumii neno serikali, anatumia Nyerere. Mbele ya safari kwa akina Mwinyi na Kassim Juma, Kikwete na Ponda, hatumii majina anatumia serikali

Unaweza kuona jinsi anavyojitahidi kumjengea mazingira ya chuki Mwalimu.

Ndiyo maana anafikia mahali pa kusema ' Nyerere hana umuhimu tena na pazia la show yake limeshushwa''
 
Porojo ndeeeeeefu isiyo na kichwa wala miguu.

Jee, umewahi kumsikia Mafongo? Nnajuwa la Mshume Kiyate (my hero) limekuwa gumu sana kwako kulimeza, sasa shushia na Mafongo.
 
Umekazana kutapika "kumtusi Nyerere" lakini mpaka sasa hujaweka nukuu hata moja ya kuonesha hilo. Unabwabwaja na kuhororoja bila mpango wakati Alama Mohamed Said anakupa vitu kimpangilio na "citations" na mapicha juu.

Wacha kupinga hewa, njoo na vitu "solid", unajizidishia maradhi bure bilash.

Sasa Kati yako na uliyemjibu nani anabwabwaja!? Hivi mbona una mtetea sana huyu mzee aliyeamua kuwapotosha!? Kwanini usijisimamie mwenyewe!? Huyu mzee sio kwamba hajafanya research, amefanya lakini anatumia research zake upside down kuwapotosha watu kama nyie. Kifupi anaandika historia kwa mtazamo wa kidini japo hamtaki kukubali. Mbona amekaza na kina Abdul Sykes wakati cabinet ilikuwa na watu wengi!? Kama hao kina Sykes walikuwa na uwezo walishindwa nini kupata uhuru miaka ya 1950 kabla ya ujio wa Nyerere. Barcelona inawachezaji wengi anayevuma ni Messi, Madrid inawachezaji wengi kinara wao ni Ronaldo, mtake msitake Nyerere is a hero, na hakuna washindi wa kwanza wawili hata wakilingana marks mwenye alfabert ya mwanzo ndio ataanza kutamkwa. Hakuna namna ya kuwatamka wote kwa sekunde moja hata maumbile yanakataa!!
 
Nnaona unabwabwaja na kuhororoja bila mpango na kutowa shutuma bila ya kuwa na yakini.

Jee, umekisoma kitabu cha Maisha na Nyakati za Abdul Wahid Sykes, kilichoandikwa na Alama Mohamed Said?
 
Mkuu lengo ni hilo , kwanza kumdhalilisha Nyerere halafu kujenga hoja.

Unaweza kumsoma akisema '...Nyerere si muhimu tena' hilo tu linaonyesha nia aliyo nayo ya kutaka kumuonyesha Nyerere hana kitu

Na katika kushadidia hilo, bandiko la Uncle Jei Jei alitoa hoja kuwa wanahistoria wa kawaida ni rahisi kuwasahau 'initiator' wa harakati za uhuru''

Mohamed Said akasema si kweli na hakuna ushahidi wa kisomi, akimaanisha si kweli kuwa historia ina favor Nyerere kwa nyadhifa alizoshika licha ya ukweli kuwa wapo waliopigania na kuandaa mazingira mapema kabla yake

Tunaweza kuona mifano michache ya kushadidi hoja ya Uncle Jei jei na mantiki yake
1. Utasikia Abdul Sykes ndiye alifanya ABCD katika harakati za uhuru.

Hayo yanayosemwa ameyafanya miaka ya 1948. Tukirudi nyuma , kuna mtu asiyetajwa ambaye kwa mujibu wa uncle jei jei ndiye 'initiator' wa harakati za karibuni (1900)

Huyu ni mwalimu Ceci Matola, mwenyekiti wa kwanza wa AA akiwa na katibu wake Sykes
Vipi Abdul Sykes anaweza kuwa nyota kuliko Cecil Matola?
Na kwanini Nyerere asiye nyota kuliko Abdul Sykes?

Pili, leo tunazungumzia Nelson Mandela wa ANC. Chama hicho kilianzishwa miaka 1915 na akina Dube na Plaatje. Kilibadilika na kuwa ANC mwaka 1923 Mandela akiwa mtoto wa miaka si michache sana.

Nyota ya Mandela iling'aa wakati wa Umkhonto Weswize kama ilivyokuwa kwa Abdul

Nani anawajua akina Govan Mbeki, Oliver Tambo au Ahmed Kathrada Zaidi ya Mandela?

Tatu, India anajulikana Gandhi. Huyu alifanya shughuli zake kule Afrika kusini hata Mandela hajazaliwa ingawa si mwanzilishi wa harakati za uhuru wa India.

Leo nani anajua mwanaharakati mwingine Zaidi ya Gandhi?

Kwa mifano hiyo ni wazi kuwa historia yetu itamtaja Nyerere kama ilivyowataja akina Mandela, Gandhi n.k. Iweje basi wawepo wenye vinyongo dhidi ya Nyerere kuwa superior kwa Abdul Sykes na si Cecil Matola?

Historia haitungwi au kurithishwa,inajieleza. Katika kujieleza huko kuna ''spikes'' mbazo hutokea bila kuandaliwa.

Kujaribu kuzifuta ni ku disturb equilibrium ya equation na hapo ndipo kunazuka tatizo.

Tatizo ni kama hili alilolileta Mohamed la kuweka Nyerere na Abdul katika mizani ili kumdharaulisha Nyerere kwa kauli kama 'pazia la show yake limeshushwa'

well, tunamwangalia Abdul Sykes na kugundua mengine , kwa mfano

1. Tunajua Sykes wote hawaku modernize siasa katika kiwango cha Nyerere

Tumesema Nyerere kaandika katiba ya chama cha siasa ya kwanza.
Goli linahamishwa alikopi kutoka kwa Nkrumah. Tukiangalia Zaidi, Sykes wote hakuna aliyewahi kuandika au kukopi mwongozo wa chama. MS kashindwa kuleta ushahidi

2. Tunaambiwa TANU ilianza Burma. Tumeomba ushahidi mmoja tu wa mkusanyiko uliowahi kutumia jina la TANU kabla Nyerere haja rasmisha chama kuwa TANU. Hakuna

Kuwa na jina mfukoni na kulitumia jina practically ni vitu tofauti. Hawakubali

Lakini pia MS anakwepa ukweli kuwa Abdul hakuwepo katika uongozi baada ya uhuru

Kilichomtimua Sheikh Amir ni harakati za misikitini dhidi ya Nyerere.
Hizi ziliungwa mkono na wengine. Baada ya chaguzi za chama wapo waliopoteza umaarufu. Hawa wakahamisha harakati za ukombozi wa nchi kuwa za kidini

Wakitaka kumuondoa Nyerere kupitia siasa za misikitini, na kama mtawala Nyerere hakukubali hilo. Unaweza kumsoma MS anaposema waislam ndio wamepigania uhuru wa chi hii. Hapa kuna reservations ambazo huziweka wazi katika nyuzi nyingine

MS anaposema Nyerere kamtimua sheikh Amir, lengo ni kuonyesha alivyowachukia waislam. Hatoi sababu akijua zitapingana na dhana ya uhuru. Ni katika kumdhalilisha

Na ukimsoma MS hatumii neno serikali, anatumia Nyerere. Mbele ya safari kwa akina Mwinyi na Kassim Juma, Kikwete na Ponda, hatumii majina anatumia serikali

Unaweza kuona jinsi anavyojitahidi kumjengea mazingira ya chuki Mwalimu.

Ndiyo maana anafikia mahali pa kusema ' Nyerere hana umuhimu tena na pazia la show yake limeshushwa''
Nguruvi3,
Hakika historia ya Mwalimu Nyerere katika TANU kwangu mimi haina
umuhimu tena kwani nimeikamilisha.

Ukurasa huu nimeufunga.

Lakini hii haikondoa umuhimu wa Mwalimu Nyerere kama somo kwa baadhi
ya watafiti.

Kwa takriban miaka mitatu hivi Prof, Issa Shivji, Prof. Saida Haroub Othman
na Dr. Kamata wanaandika maisha ya Mwalimu Nyerere.

Nimefanyanao mazungumzo mara tatu na yamerekodiwa.
Nimekuwekea picha nikiwanao nyumbani kwangu.

Nimewakabidhi nyaraka tena kutoka katika mafaili ya Sykes pamoja na picha
ambazo mimi nyingine ni za Sykes na nyingine kutoka kwa watoto na wajukuu
wa wazalendo waliokuwa na Nyerere katika TANU.

Kwa watafiti wapya wao ndiyo kwanza wanapandisha pazia.

Mimi langu nilipandisha zaidi ya miaka ya 30 iliyopita na kwa hakika historia hii
ndiyo iliyonifanya nifahamike kwani nilikuwa nimekuja na kitu kipya katika historia
ya Tanganyika.

Kulikuwa na watu wengi hawakupatapo kusikia katika historia ya TANU majina
niliyokujanayo.

Mfano ni kama Idd Faizi Mafongo huyu alikuwa mwanachama kadi yake no. 25.

Idd Faiz ndiye aliyeratibu safari ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 na alikuwa
mweka hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Tanganyika
Muslim Assocation).

Nilipoeleza habari hizi watu walisisimka khasa Waislam.

Hali ilikuwa hivi nilipoeleza historia ya Said Chamwenyewe, Sheikh Suleiman
Takadir, Bi. Tatu biti Mzee
na majina mengine mengi kutoka katika majimbo
ambayo sasa si mageni tena kama Hamisi Kheri, Bi Sharifa biti Mzee nk. nk.

Historia hii iliwafurahisha wengi na iliwakera wengi na kila kundi lilifurahi na pia
kukereka kwa sababu zao.

Mengi yalipitika lakini mimi haya hayakunishughulisha muhimu kwangu ni kuwa
nilikuwa naihifadhi historia iliyokuwa imepotezwa kwa makusudi.

Huu nimekupa kama mkadama.
Yaani utangulizi.

Sasa ikiwa unazo taarifa ya mambo aliyofanya Cecil Matola itakuwa vizuri ukaandika
tutasoma kama tunavyowasoma hawa wengine.

Lakini ninachojua mimi Cecila Matola baada ya kuundwa kwa African Association
hakuishi sana akafariki nafasi yake ikachukuliwa na Mzee bin Sudi.

Mimi naijua historia ya wanachama waliokuwa African Association na mambo ambayo
walifanya katika kusukuma maslahi ya Tanganyika.

Alikuwapo Mwalimu Mdachi Shariff huyu alikuwa mwalimu na ndiye aliwasomesha
akina Abdul Sykes na baba yangu shule ya Kitchwele.

Alikuwapo Ramadhani Mashado Plantan yeye alianzisha gazeti, ''Zuhra,'' halikadhalika
alikuwapo Erika Fiah na yeye pia alikuwa na gazeti, ''Kwetu.''

Itahitaji darsa maalum mimi kueleza makubwa waliofanya wazalendo hawa katika magazeti
yao.

Baadhi ya magazeti haya yapo East Africana katika Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Nimeyasoma yote wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes.

Wazalendo hawa wawili waliniingiza katika dunia sikujua kuwa ilikuwapo.

Alikuwapo Mwalimu Thomas Saudtz Plantan mwalimu wa shule alisomesha Mpwapwa
na kwengineko akamalizia Shule ya Mchikichini kwa kueleza kwa uchache.

Babu yangu Salum Abdallah aliishi Dar es Salaam ya wakati huu na baba yangu hawa
wote niliokutajia akiwajua na nimejifunza mengi kutoka kwake.

Hapa ndipo ilipo tofauti kati yangu na wewe.
Mimi nimeishi ndani ya historia hii.

Mimi sikujui wewe wala utokako wala sijui wazee wako wana mchango gani katika TANU
na harakati za kudai uhuru.

Umezungumza mengi lakini naona sina haja ya kukujibu neno kwa neno ila nitagusa hili
la Mufti Sheikh Hassan bin Amir.

Sheikh Hassan bin Amir
hakufanya hayo wewe unayosema kafanya dhidi ya Nyerere.

Nimeandika historia ya Sheikh Hassan bin Amir na nimefanya mihadhara kadhaa mingine
iko youtube.

Ingia hapa:
https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm
 
Nnaona unabwabwaja na kuhororoja bila mpango na kutowa shutuma bila ya kuwa na yakini.

Jee, umekisoma kitabu cha Maisha na Nyakati za Abdul Wahid Sykes, kilichoandikwa na Alama Mohamed Said?
Faiza huyu jei jei hana anacho sema chenye ithibati ni mtu anaandika tu kwakuwa anajua kuandika.
Mbaya zaidi hajui na hajui kama hajui.
Mtu atoa mfano wa mesi na ronaldo hajui kama kuna neimer na shwares na hata gaucho.
Huyu atakupotezea muda wako mwingi sana ingawa si vyema kumuacha akiropokwa.
 
Sasa Kati yako na uliyemjibu nani anabwabwaja!? Hivi mbona una mtetea sana huyu mzee aliyeamua kuwapotosha!? Kwanini usijisimamie mwenyewe!? Huyu mzee sio kwamba hajafanya research, amefanya lakini anatumia research zake upside down kuwapotosha watu kama nyie. Kifupi anaandika historia kwa mtazamo wa kidini japo hamtaki kukubali. Mbona amekaza na kina Abdul Sykes wakati cabinet ilikuwa na watu wengi!? Kama hao kina Sykes walikuwa na uwezo walishindwa nini kupata uhuru miaka ya 1950 kabla ya ujio wa Nyerere. Barcelona inawachezaji wengi anayevuma ni Messi, Madrid inawachezaji wengi kinara wao ni Ronaldo, mtake msitake Nyerere is a hero, na hakuna washindi wa kwanza wawili hata wakilingana marks mwenye alfabert ya mwanzo ndio ataanza kutamkwa. Hakuna namna ya kuwatamka wote kwa sekunde moja hata maumbile yanakataa!!
Uncle...
Tatizo kubwa lililonifanya nikaandika historia ya Abdul Sykes ni kule
kuona kafutwa.

Aliyepotosha historia si mimi.
Mimi nimekuja kuirekebisha.

Hayo mengine unayosema hayana maana yoyote.
 
duuh hostoria nzuri kweli kweli hakika Mzee Mohamedi Saidi unatudadavulia watu tusiyoyajua hongera sana Mzee
Wa ukae,
Ahsante sana.

Mungu ana mipango yake na njia zake sisi waja hatuwezi kuzijua.
Mimi nimezaliwa wakati ule na watu hawa.

Sikuingia darasani kusomeshwa historia ya TANU na siku niliposomeshwa
historia hii Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nilimwambia mwalimu wangu,
''Mwalimu mbona hii historia siyo?''

Nilipoanza kueleza hata yeye alipigwa na mshangao.
Akaniuliza mimi nimeyajuaje hayo yote?

Jibu langu lilikuwa, ''Wazee wangu ndiyo walioasisi TANU.''

Hebu sasa hebu wewe mwenyewe fikira nikawa natoa hata namba za kadi
zao za TANU.

Darasa lilkawa kama limemwagiwa maji baridi ya kuzizima.
 
Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.

All in all, you have a grudge against Nyerere.
Na unataka kuifanya chuki "yako dhidi ya Nyerere" iwe ni chuki ya "waislam dhidi ya Nyerere"

Wewe sio MTU mzuri.
 
Mimi sina chuki na Nyerere.

Hiyo chuki ya Waislam dhidi ya Nyerere kama ipo itakuwa
na sababu zake.

Wewe umemsingizia babu yangu uongo na nimekujibu basi
unashindwa hata kuniomba radhi baada ya kukueleza ukweli?
 
Huna chuki na Nyerere?
Mara ngapi hapa unaanzisha threads kwa titles tofauti ilhali ukilenga kumchafua Nyerere?
Na ni Mara Nyingi una-instigate chuki amongst innocent and unsuspecting Muslims.
Tukiendelea na thread hii, mwishowe watu watapata picha yenye uongo kuwa Muslims ndio walipigania Uhuru nchi hii, halafu Nyerere akawa-sideline kwenye maendeleo kwa maagizo ya kanisa katoliki. Mara zote unapoanzisha thread, lengo lako ndio hili: kuhamasisha chuki za kidini.
Utaanzisha threads za Kighoma Malima, waslam na NECTA, mapinduzi ya Zanzibar, n.k. lakini mwisho wa siku lengo ni kuhamasisha chuki tu.
 
Uncle...
Tatizo kubwa lililonifanya nikaandika historia ya Abdul Sykes ni kule
kuona kafutwa.

Aliyepotosha historia si mimi.
Mimi nimekuja kuirekebisha.

Hayo mengine unayosema hayana maana yoyote.

Huenda wewe umeona kafutwa, huo ni mtazamo wako. Lakini si lazima uwe sahihi. Unatakiwa kuelewa kuwa historia inakawaida ya kumbeba mtu kulingana na wakati na umuhimu wake kwa wakati husika. Sykes na familia yake wanamchango mkubwa kabisa katika harakati za uhuru wa Tanganyika hakuna anayebisha. Lakini hata yeye angekuwa hai angetusaidia kukuelezea umuhimu wa Nyerere baada ya kuingia rasmi mwaka 1952 kwenye mapambano hayo. Labda nikukumbushe maandiko yako mwenyewe ya Tar. 25 may, 2013 siku ya Jumamosi kwenye gazeti la Mwananchi uliyoandika baada ya kifo cha Ally Sykes kule Kenya. Uliandika hivi,... "inajulikana na wengi kuwa Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Julius Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952." Unaendelea kuandika "Nyerere alifika nyumbani kwa kina Sykes kwa utambulisho na hii ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa na udugu mkubwa..." Hapa unakiri familia ya Sykes kuwa na urafiki na "udugu" na familia ya Nyerere. Kisha unaandika hivi:... "wakati huo Abdulwahid ndiye alikuwa Rais wa TAA na harakati za kuanzisha TANU zimepamba moto"... Halafu angalia hapa uliyoandika,..." ndiyo maana TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 Aly Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba 2, Nyerere namba 1, Abdulwahid Sykes kadi yake namba 3..." Hoja yangu hapa ni moja tu, wewe unasema "historia ya Nyerere katika TANU haina umuhimu tena ", lakini hao unaotaka wao ndo wawe na umuhimu kuliko Nyerere wanapingana na wewe kwa kumpa Nyerere aliyekuwa mgeni kwao tena wa kutambulishwa kadi namba moja ya CHAMA! Hivi unataka useme wao walikuwa ni wapuuzi kiasi hicho!? Kwa kadiri ya maandishi yako mwenyewe, Nyerere alikuwa amejuana na kina Sykes kwa takribani miaka miwili tu lakini bado walimpa kadi namba moja!?! Wao walikosa nini ambacho Nyerere alikuwa nacho hadi kupewa namba Moja!? Je, hicho walichokosa wao na Nyerere kuwa nacho leo kwako kimekuwa si lolote!? Wazee wako walikiheshimu na walikithamini hicho walichokosa ambacho alikuwa nacho Nyerere. Kwanini wewe upingane na Wazee wako!?
 
Huna chuki na Nyerere?
Mara ngapi hapa unaanzisha threads kwa titles tofauti ilhali ukilenga kumchafua Nyerere?
Na ni Mara Nyingi una-instigate chuki amongst innocent and unsuspecting Muslims.
Tukiendelea na thread hii, mwishowe watu watapata picha yenye uongo kuwa Muslims ndio walipigania Uhuru nchi hii, halafu Nyerere akawa-sideline kwenye maendeleo kwa maagizo ya kanisa katoliki. Mara zote unapoanzisha thread, lengo lako ndio hili: kuhamasisha chuki za kidini.
Utaanzisha threads za Kighoma Malima, waslam na NECTA, mapinduzi ya Zanzibar, n.k. lakini mwisho wa siku lengo ni kuhamasisha chuki tu.
Nanren,
Nimekuuliza huna uungwana wa kunitaka radhi kwa kumsingizia
kuwa aliwekwa ndani kwa chokochoko wakati si kweli?
 
Tangawizi,
In deed kaka hamna kitu.
Ni bahati tu hata kujua kuandika.

Mwenyewe ''ambition,'' yangu nilipokuwa nakua
mitaa ta Gerezani nicheze mpira Sunderland
(sasa Simba) kisha timu ya taifa.

Sikufanikiwa.

Mzee safi sana kumbe hata kwenye kabumbu ulikuwepo asante
 
Huenda wewe umeona kafutwa, huo ni mtazamo wako. Lakini si lazima uwe sahihi. Unatakiwa kuelewa kuwa historia inakawaida ya kumbeba mtu kulingana na wakati na umuhimu wake kwa wakati husika. Sykes na familia yake wanamchango mkubwa kabisa katika harakati za uhuru wa Tanganyika hakuna anayebisha. Lakini hata yeye angekuwa hai angetusaidia kukuelezea umuhimu wa Nyerere baada ya kuingia rasmi mwaka 1952 kwenye mapambano hayo. Labda nikukumbushe maandiko yako mwenyewe ya Tar. 25 may, 2013 siku ya Jumamosi kwenye gazeti la Mwananchi uliyoandika baada ya kifo cha Ally Sykes kule Kenya. Uliandika hivi,... "inajulikana na wengi kuwa Ally Sykes na kaka yake Abdulwahid Sykes ndio watu wa mwanzo kumpokea Julius Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka 1952." Unaendelea kuandika "Nyerere alifika nyumbani kwa kina Sykes kwa utambulisho na hii ilijenga urafiki ambao ulipitiliza na kuwa na udugu mkubwa..." Hapa unakiri familia ya Sykes kuwa na urafiki na "udugu" na familia ya Nyerere. Kisha unaandika hivi:... "wakati huo Abdulwahid ndiye alikuwa Rais wa TAA na harakati za kuanzisha TANU zimepamba moto"... Halafu angalia hapa uliyoandika,..." ndiyo maana TANU ilipokuja asisiwa mwaka 1954 Aly Sykes kadi yake ya TANU ikawa namba 2, Nyerere namba 1, Abdulwahid Sykes kadi yake namba 3..." Hoja yangu hapa ni moja tu, wewe unasema "historia ya Nyerere katika TANU haina umuhimu tena ", lakini hao unaotaka wao ndo wawe na umuhimu kuliko Nyerere wanapingana na wewe kwa kumpa Nyerere aliyekuwa mgeni kwao tena wa kutambulishwa kadi namba moja ya CHAMA! Hivi unataka useme wao walikuwa ni wapuuzi kiasi hicho!? Kwa kadiri ya maandishi yako mwenyewe, Nyerere alikuwa amejuana na kina Sykes kwa takribani miaka miwili tu lakini bado walimpa kadi namba moja!?! Wao walikosa nini ambacho Nyerere alikuwa nacho hadi kupewa namba Moja!? Je, hicho walichokosa wao na Nyerere kuwa nacho leo kwako kimekuwa si lolote!? Wazee wako walikiheshimu na walikithamini hicho walichokosa ambacho alikuwa nacho Nyerere. Kwanini wewe upingane na Wazee wako!?
Uncle...
Sina tattizo na yote uliyoandika na khasa kuwa huenda historia hii
haikufutwa.

Sawa haikufutwa lakini haikuhifadhiwa na waliokuja kushika madaraka
katika TANU na serikali yake.

Nina ushahidi na ukipenda nitakuwekea hapa kuwa walikuwa wakikereka
na historia hiyo.

Mimi nimeona imefutwa na ndiyo maana nikaiandika na kuhitimisha
historia ya TANU.

Baada ya hili kukamilka ndiyo basi kwangu umuhimu wake umekwisha.
Wanaopata shida ni wewe na watu mfano wa wewe.

Hayo mengine unayasema huna ujuzinayo wala huyajui.

Mambo baada ya uhuru kupatikana yalibadilika pakubwa na ndiyo sababu
Abdul na Ally Sykes pamoja na wazalendo wengine michango yao ikafutwa.

Abdul na Ally walipewa medali za kuwaenzi kama wazalendo waliopigania
uhuru wa Tanganyika baada ya miaka 50 uhuru kupatikana.

Ikulu ilikuwa haijui Abdul na Ally walikuwa na mchango gani katika uhuru wa
Tanganyika.

Ikabidi waende ofisini kwa Ally Sykes kumuomba awaandikie mchango wake
na wa marehemu kaka yake.

Unafahamu ni nani aliyeandika ''profile,'' ile iliyosomwa Viwanja wa Ikulu katika
sheria ya kuwatunuku medali Abdul na Ally Sykes?

Je, unakijua kilichowafanya wakawie kwa miaka yote hiyo kuwaenzi hawa ndugu
wawili waliokuwa na kadi za TANU no. 2 na 3?
 
Mzee safi sana kumbe hata kwenye kabumbu ulikuwepo asante
Remote,
Tatizo kipaji nilikuwa sina sikuweza kufikia viwango.
Lakini wenzangu wengi walifika hadi kileleni kabisa.

Ikawa wao wakitoka timu ya taifa na Adidas mpya
mie wananitupia za zamani na bukta zao.

Wengi wa rafiki zangu hawa wametangulia mbele
ya haki.

XYMqEZSvBNSeDI8mZr7OhmACjYvF4WT99rs2LcaiqXMCMS6x_hLORu5seB5leFdlssXArDeKke2by_QNcO1dPyQnN8Zb8C0zI_jIg71u8-UvNTiLw5v52TYhQ5sFIQ58nFhNO-WZS9VzjRCjNMexWZlXxYTq5mw66eNIG0LqE-5aUwDt8rHl2uv_egLqWlyEmfOS5SK4eQeUakfA0L6G1YQdQWTf7tMlVbRSeiO73gSQmlaLhok0A-dAuR0aiCMdU2N6MT7VfNF9BT3P-UO9GsAb_fy7rsnROpJooTHHPNeD72hcer6iIE-T4yRaSxpunWv5U7d4lNntWPDvZUt2zrS_tcm4HjGl4E3ELI-pDbiWIeMeTBESVpoeSrcegPIwrPNwvcX6tIT4r4laIIOrDXEX-G0DMnzoL0C-807aitYLU3-zThSvaeYhHcLbml8i5RwlwDgEfNJ4PB891wJmlr1BT61KGFBRS4OC3mJXsV02-FJrmFBoNMYQogUwY3RiOjsipFztKJTD6CF-cwWnmGBzvZ6xqpWW-AZMBZX7YGY7AW73BTkEA7L_hwfIHl61GIWqb-hOTwjHuzIFd6CpS3GKj8iyyfr5=w596-h657-no
 
Back
Top Bottom