Bado hujakutana na wachawi Mkuu, mwanadamu anao uwezo wa kupambana na ushirikina tu na sio uchawi.
Nimeuliza swali, kama uchawi una nguvu hio ilikuaje babu zetu wakashindwa kuwaroga wazungu kwenye ukoloni wakakimbia tukaendelea kujitawala?
Uchawi ungekuwa big deal mzee wangu kuna mambo katika hii dunia tunaishi yasingekuwa kuwa kama yalivyo kuanzia siasa, elimu, utajiiri, michezo n.k
Ndio maana nakuambia uchawi ni imani tu, ndio maana hata kwenye masuala ya sciende kuna mzee aliandika kitabu kinaitwa biology of belief anaitwa Bruce Lipton, huyo mzee ni professor mkubwa na anasema kuna mahusiano kati ya akili/mind na mwili anasema kuna muingiliano, uhusiano kati ya akili na maada.
Lipton anasema kwamba mawazo na imani zako zinaweza kuwa na athari kubwa kwa mwili wako, inaweza kuathiri kila kitu kutoka kwa mfumo wako wa kinga hadi homoni zako.
sasa hio ni sayansi, na wanasayansi wanakiri ni mapinduzi makubwa katika biology.
Hata uchawi ndicho nachosema hapa ni imani, kama wanasayansi wananyoosha mikono na kusema imani na akili ya mtu ni vitu powerful katika imani za kishirikina kwa nini upinge?