Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 11,936
- 15,196
Habari za mapumziko,
Inasemekana walioiba Silaha kwenye ofisi za TAKUKURU huko Handeni ni maafisa TAKUKURU wenyewe.
Chanzo chetu kutoka Handeni kinasema maafisa hao wakishirikiana na watu wa ishu/Majambazi walisuka njama za kuziiba silaha hizo huku wakiahidiwa kupewa donge nono.
Inasemekana siku ya tukio washukiwa walikuwa wote kwenye baa moja maarufu wilayani hapo wakikamilisha mpango huo.
Mnyetishaji wetu anasema hakukuwa na uvunjifu wowote na kutupwa kwa funguo ni geresha iliyopangwa na maafisa hao ili kuonesha kwamba walikuwa ni majambazi.
silaha hizo zilisafirishwa usiku na kupelekwa mkoa mmoja huko kaskazini mwa nchi ambako kuna ujambazi mwingi.
Tunazishauri mamlaka zinazohusika ziwabane MAAFISA TAKUKURU Ili wakaoneshe silaha zilipo kwani wao ndiyo wahusika kwenye mpango huu.
Nawasilisha