Haniulizi kwa lolote

Haniulizi kwa lolote

Hahahaha eti kununiana hahahaha hyu itakua aliruka stage @43 unawaza kununiana wkt we dd that @18-20
Kugombana kupo na kupotezeana ila sasa mwenzangu analazimisha anuniwe hahahhaha kweli dunia ina mambo
 
Habari
Naomba nianzie mbali kidogo, mimi ni mwanaume wa miaka 43. Sijaoa ila niko mbioni kuoa. Wakati nilipomaliza kidato cha nne, nilijikuta katika mahusiano yaliyoniletea mtoto wa ujanani mapema sana. Mama wa mtoto huyu tuliachana nilipoingia chuo kikuu, hivyo nikawa kwenye mahusiano ya hapa na pale ambayo hayakudumu kwa kweli kiasi cha kufikia kuoana.

Mtoto wangu alipofikisha miaka 10 nilimchukua toka kwa mama yake na kuanza kuishi naye wakati huo nikiwa naishi kwa wazazi na hata nilipoanza kujitegemea niliondoka naye na niko naye hadi sasa na ni binti mkubwa tu. Kuna wakati tulikwaruzana sana na binti yangu. nadhani katika zile hatua za ukuaji. Akawa mtukutu sana na mwenye maendeleo mabaya shuleni.

Sasa katika kutafuta mahusiano nikajikuta katika mahusiano na mwanamke mmoja ambaye nimemzidi miaka 10. Mwanadada huyu tulikutana katika halfa fulani. Tukafahamiana na taratibu tukawa marafiki. Kiukweli nilivutiwa naye sana sio tu kwa mvuto alionao, bali pia namna alivyokuwa amejiweka. Msomi, mjasiriamali, muelewa na msikivu.

Nikawa nasita kidogo kumtokea nikihofia tofauti ya umri lakini siku moja akaamua mwenyewe kunieleza hisia zake. Nilishangaa sana mwanamke kunitokea.

Hivyo ndivyo tukajikuta katika mahusiano, Nakiri kwanza kuwa amenisaida mno kumnyoosha binti yangu kitabia na kitaaluma. Hivi ninavyoandika binti yangu anafanya vizuri darasani na ana nidhamu kwangu.

Ni miaka miwili tangu niwe na huyu dada inaelekea watatu lakini kinachonifanya niombe ushauri ni mambo madogo madogo ambayo nayaona kwa huyu dada na yananipa msongo kwa kiasi fulani, sielewi tatizo ni mimi au huyu dada.

Kwasasa tunaishi pamoja, ingawa ana kwake pia ila muda mwingi yuko nyumbani kwangu. Huyu dada hajui kubembelezana na mtu. yaani hana zile hulka za kike kike za mkikosana abembeleze au anune nune hivi. Huyu hana kabisa. Akikosea ataomba radhi hapo hapo na amemaliza. Ukimkaushia imekula kwako kwa kuwa akikutafuta mara mbili tatu ukamchunia ni mpaka utakapoamua wewe kumtafuta na utamkuta poa tu wala hakuulizi kwanini ulimkaushia.

Pili, Ukimkosea hana zile analia au kusema mpenzi wangu umeniumiza na vitu kama hivyo, yeye atakwambia abcd zake na amemaliza. Uombe radhi au upotezee hana habari. Hili jambo ndio huwa linaniacha hoi kabisa. Kuna wakati nilikuwa karibu na mwanamke fulani kazini. Akafuma meseji zenye utata kidogo. Alichofanya aliuliza na mimi nikajitetea kizembe sana ikawa basi, akaingia jikoni kupika na alipotoka uko akawa kama hakuona chochote.

Ni kama vile hana wivu ingawa pia akiona kitu tata anahoji kwa ukali kwelikweli na alishaniambia akichoka vituko atasepa kimoja, na mimi sitaki hilo litokee

Kuna wakati niliamua tu kumjaribu nikamkalia kimya, aliponitafuta nikamwambia nahitaji muda wa kuwa peke yangu. Nilijua labda atanibembeleza nimueleze tatizo. Aliitikia na kukubaliana nami. Huwezi amini alikaa wiki mbili kimya kabisa mpaka nilipoamua kumtafuta. Nikamuuliza kisa cha ukimya, akajibu ulisema unahitaji muda wa kuwa mwenyewe. Nilishangaa mno! Nikamwambia nimerudi. Akajibu karibu hakuuliza tatizo langu wala nini, Nilipomhoji kwanini haulizi hata kwanini nilikuwa kimya. Akanijibu we ni mtu mzima ukiamua utasema. Akaishia hapo.

Niliwahi kumkutanisha na dada yangu, masaa tu aliyokaa naye, aliniuliza huyu dada tutamuweza? Mbona hana bashasha za kiwifi wifi akimaanisha hazoeleki haraka. Marafiki zake ninaowajua ni watatu na sijawazoea kivile maana hata wao hawaelekei kunizoea.

Nikahisi labda anafanya hivi kwa kutafuta ndoa na angenionyesha makucha yake baadaye, nikamwambia mikakati ya ndoa tusitishe kwa sasa. Akajibu sawa wewe ndio muoaji, hakushtuka wala kukasirika. Baadae nikamwambia basi tuharakishe kufunga ndoa, akaniambia naonekana sijui nataka nini hivyo nitulize akili nijiulize kama kweli nataka kuoa na nataka kumuoa nani.

Nimekuwa nikichunguza kama ana mahusiano mengine ya nje, kwa miezi mitatu nilimfuatilia sana na sikugundua kitu chochote zaidi ya kuwa ana ukaribu na watu wenye pesa zao na hadhi kubwa kubwa. nahisi kama ananicontrol bila kujua najikuta namfanyia visa na vituko vya kitoto kila mara mradi tu anipe attention yake hata kama ni kunionyesha hasira ila wapi.

Anaweza akaamua kutokupika, na ukimuuliza anakujibu straight mimi sio wife hapa kwako ni mpenzi tu, nina uhuru wa kuamua kupika au lah. Majibu kama hayo nachoka kabisa ukizingatia nimemzidi miaka 10!

Ana mtoto mmoja ambaye, anaishi kwake pamoja na mdogo wake. Mtoto wa huyu baba yake ni mtu wa nje na hawana hata mawasiliano kwa kuwa hilo nimechunguza pia. Kama ni kunipenda alinitamkia mwenyewe japo mimi pia nilishampenda lakini sielewi kwanini yuko hivi alivyo.

Nifanye nini anionee wivu hata kidogo tu, au awe na hulka za kike, au kama wanawake wengine wanaonyenyekea waume zao aache uandava alionao… nikisema nitumie pesa kumhandle hata yeye anazo kiasi chake na huwa haombi chochote kile na hajawahi kuomba hata senti na nilitegemea na umri wake huo angenipapatikia kidogo ili nimuoe matokeo ni tofauti. Ila nampenda sana huyu dada maana kwenye sekta zingine kama mwanamke sio mtu wa mchezo.





duuuuuuuuu huyo kwa mimi ndo anafaa coz napenda tu mtu ajue nafasi yake na sio kuchimbana
 
Pole mkuu Huyo alishawah kupenda kupitiliza na alikuwa na wivu usiopimika na alifanyiw kitu mbaya katk mahusiano so alishaona hivyo vitu kwa sasa havina ulazima katk maisha yak kwa kifup kaathirik kisaikilojia kwa kias kikubwa ongea naye polepolw
 
yupo poa sana mademu kama hao ndo wazuri hawana unafki.. binafsi nimempenda sana
 
Huyo manzi kama hajalelewa na wazungu basi anatokea kanda ya ziwa mkoa fulani hivi yaani wenyewe hawana swaga sijui kukuita majina ambayo si yako, sijui kubembeleza wenyewe nyeupe ni nyeupe ila wana mapenzi ya kweli aisee.
 
Kuna watu wanamsifia huyo dada but ukweli ni kwamba jiongeze. Kwake ukiwepo usipokuwepo hupungukiwi chochote.

Na hiyo ni hatari.
Mdada hana feelings nae, ndio maana akiwepo na asipokuwepo hapungukiwi kitu.
 
Huyo ndo mzuri kama hutaki subiri wakukunyenyekea! Na kama unahitaji unyenyekevu nenda kanisani kiongozi au msikitini ila namba utaisoma! Binafsi nashukuru nimeshaoa vinginevyo ningemtafuta kwani napenda mwanamke aliye straight forward na si vinginevyo!
 
nakupa makavu live bila chenga...

1, umetongozwa ukakubali.. tukitongozwa maana yake me ni dereva.
2. jinga wewe unaact kama demu unamletea vituko vituko mambo ya kike.
3, haupo kama mwanaume umelegea legea hata uandishi wako unaonyesha kitu cha paragraph mbili umeandika kumi.

that woman she is controlling frick chukua au acha.

NB: KUWA MWANAUME
Miss chagga, mbona story ya mkubwa haina tatizo...! Mwache mamii, aseme ya moyoni,
 
Umesema huyo dada anamtoto mmoja yawezekana alishawah umia kwa kuendekeza kupenda Sana, sasa saikologia yake kashaijenga kujidefence peke yake na pamoja na kukupenda ila anamamuz yake binafsi nikusih umwoe huyo mdada ila kwa kua umedhamsoma tabia zake, hayo ndio mazaifu yake na uyabebe kama yalivyo
 
nakupa makavu live bila chenga...

1, umetongozwa ukakubali.. tukitongozwa maana yake me ni dereva.
2. jinga wewe unaact kama demu unamletea vituko vituko mambo ya kike.
3, haupo kama mwanaume umelegea legea hata uandishi wako unaonyesha kitu cha paragraph mbili umeandika kumi.

that woman she is controlling frick chukua au acha.

NB: KUWA MWANAUME

yaani umenisaidia kumpa kitu live....... huyu ni bwege bwegezo.....huyo dem ndie anaongoza maisha yako..... mwanaume gani hujielewi wewe???? mpaka siku akuguse senta back ndo utajitambua......kweli una 43yrs wewe??? ndo nyie mnafika 45 mnaanza kuvaa kata "K".....pambafu sana wewe......
 
Back
Top Bottom