Haniulizi kwa lolote

Haniulizi kwa lolote

Umenikumbusha kuna kipindi fulani tulitofautiana na mtu.
Daima sipendi kulazimishwa...sasa yeye akawa ananilazimisha na mimi nikabaki na msomamo wangu.
Akanuna kama wiki 2...mimi kimyaaaa!
Mbona alinitafuta?
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Love is feelings, kama huna hisia nae ya nini kuwa nae, acheni unafiki.
 
Habari
Naomba nianzie mbali kidogo, mimi ni mwanaume wa miaka 43. Sijaoa ila niko mbioni kuoa. Wakati nilipomaliza kidato cha nne, nilijikuta katika mahusiano yaliyoniletea mtoto wa ujanani mapema sana. Mama wa mtoto huyu tuliachana nilipoingia chuo kikuu, hivyo nikawa kwenye mahusiano ya hapa na pale ambayo hayakudumu kwa kweli kiasi cha kufikia kuoana.

Mtoto wangu alipofikisha miaka 10 nilimchukua toka kwa mama yake na kuanza kuishi naye wakati huo nikiwa naishi kwa wazazi na hata nilipoanza kujitegemea niliondoka naye na niko naye hadi sasa na ni binti mkubwa tu. Kuna wakati tulikwaruzana sana na binti yangu. nadhani katika zile hatua za ukuaji. Akawa mtukutu sana na mwenye maendeleo mabaya shuleni.

Sasa katika kutafuta mahusiano nikajikuta katika mahusiano na mwanamke mmoja ambaye nimemzidi miaka 10. Mwanadada huyu tulikutana katika halfa fulani. Tukafahamiana na taratibu tukawa marafiki. Kiukweli nilivutiwa naye sana sio tu kwa mvuto alionao, bali pia namna alivyokuwa amejiweka. Msomi, mjasiriamali, muelewa na msikivu.

Nikawa nasita kidogo kumtokea nikihofia tofauti ya umri lakini siku moja akaamua mwenyewe kunieleza hisia zake. Nilishangaa sana mwanamke kunitokea.

Hivyo ndivyo tukajikuta katika mahusiano, Nakiri kwanza kuwa amenisaida mno kumnyoosha binti yangu kitabia na kitaaluma. Hivi ninavyoandika binti yangu anafanya vizuri darasani na ana nidhamu kwangu.

Ni miaka miwili tangu niwe na huyu dada inaelekea watatu lakini kinachonifanya niombe ushauri ni mambo madogo madogo ambayo nayaona kwa huyu dada na yananipa msongo kwa kiasi fulani, sielewi tatizo ni mimi au huyu dada.

Kwasasa tunaishi pamoja, ingawa ana kwake pia ila muda mwingi yuko nyumbani kwangu. Huyu dada hajui kubembelezana na mtu. yaani hana zile hulka za kike kike za mkikosana abembeleze au anune nune hivi. Huyu hana kabisa. Akikosea ataomba radhi hapo hapo na amemaliza. Ukimkaushia imekula kwako kwa kuwa akikutafuta mara mbili tatu ukamchunia ni mpaka utakapoamua wewe kumtafuta na utamkuta poa tu wala hakuulizi kwanini ulimkaushia.

Pili, Ukimkosea hana zile analia au kusema mpenzi wangu umeniumiza na vitu kama hivyo, yeye atakwambia abcd zake na amemaliza. Uombe radhi au upotezee hana habari. Hili jambo ndio huwa linaniacha hoi kabisa. Kuna wakati nilikuwa karibu na mwanamke fulani kazini. Akafuma meseji zenye utata kidogo. Alichofanya aliuliza na mimi nikajitetea kizembe sana ikawa basi, akaingia jikoni kupika na alipotoka uko akawa kama hakuona chochote.

Ni kama vile hana wivu ingawa pia akiona kitu tata anahoji kwa ukali kwelikweli na alishaniambia akichoka vituko atasepa kimoja, na mimi sitaki hilo litokee

Kuna wakati niliamua tu kumjaribu nikamkalia kimya, aliponitafuta nikamwambia nahitaji muda wa kuwa peke yangu. Nilijua labda atanibembeleza nimueleze tatizo. Aliitikia na kukubaliana nami. Huwezi amini alikaa wiki mbili kimya kabisa mpaka nilipoamua kumtafuta. Nikamuuliza kisa cha ukimya, akajibu ulisema unahitaji muda wa kuwa mwenyewe. Nilishangaa mno! Nikamwambia nimerudi. Akajibu karibu hakuuliza tatizo langu wala nini, Nilipomhoji kwanini haulizi hata kwanini nilikuwa kimya. Akanijibu we ni mtu mzima ukiamua utasema. Akaishia hapo.

Niliwahi kumkutanisha na dada yangu, masaa tu aliyokaa naye, aliniuliza huyu dada tutamuweza? Mbona hana bashasha za kiwifi wifi akimaanisha hazoeleki haraka. Marafiki zake ninaowajua ni watatu na sijawazoea kivile maana hata wao hawaelekei kunizoea.

Nikahisi labda anafanya hivi kwa kutafuta ndoa na angenionyesha makucha yake baadaye, nikamwambia mikakati ya ndoa tusitishe kwa sasa. Akajibu sawa wewe ndio muoaji, hakushtuka wala kukasirika. Baadae nikamwambia basi tuharakishe kufunga ndoa, akaniambia naonekana sijui nataka nini hivyo nitulize akili nijiulize kama kweli nataka kuoa na nataka kumuoa nani.

Nimekuwa nikichunguza kama ana mahusiano mengine ya nje, kwa miezi mitatu nilimfuatilia sana na sikugundua kitu chochote zaidi ya kuwa ana ukaribu na watu wenye pesa zao na hadhi kubwa kubwa. nahisi kama ananicontrol bila kujua najikuta namfanyia visa na vituko vya kitoto kila mara mradi tu anipe attention yake hata kama ni kunionyesha hasira ila wapi.

Anaweza akaamua kutokupika, na ukimuuliza anakujibu straight mimi sio wife hapa kwako ni mpenzi tu, nina uhuru wa kuamua kupika au lah. Majibu kama hayo nachoka kabisa ukizingatia nimemzidi miaka 10!

Ana mtoto mmoja ambaye, anaishi kwake pamoja na mdogo wake. Mtoto wa huyu baba yake ni mtu wa nje na hawana hata mawasiliano kwa kuwa hilo nimechunguza pia. Kama ni kunipenda alinitamkia mwenyewe japo mimi pia nilishampenda lakini sielewi kwanini yuko hivi alivyo.

Nifanye nini anionee wivu hata kidogo tu, au awe na hulka za kike, au kama wanawake wengine wanaonyenyekea waume zao aache uandava alionao… nikisema nitumie pesa kumhandle hata yeye anazo kiasi chake na huwa haombi chochote kile na hajawahi kuomba hata senti na nilitegemea na umri wake huo angenipapatikia kidogo ili nimuoe matokeo ni tofauti. Ila nampenda sana huyu dada maana kwenye sekta zingine kama mwanamke sio mtu wa mchezo.
mkuu huyu mwanamke yuko vizuri muoe kabisa....wanawake wa kichaga wana hulka ya maendeleo..hawana muda kubemblezana kimapenzi (usiniulize nimejuaje kabila lake kwani tabia za wachaga hazifichiki). wachaga ndivyo walivyo mkuu....na huyo ndiye mwanamke maridhawa ambaye kila mwanaume angetamani kuwa nae...usithubutu kupoteza bahati hiyo.
 
huyo wa hivyo. no bashasha aisee simuwezi tafuta mwingine huyo kuna kitu amekitarget utaisoma namba
 
Mkuu wewe ndio tatizo your very cynical... Umekariri mwanamke.. Na kwa ushaur tu huyo ni bonge la mwanamke mzur.. Na Kama ni ishu za maendeleo they are very good na ni aina ya Wanawake ambao hata ukiwa mbali na akabaki na familia the family wil be safe.. Ni very understanding na wanaamuzi.
 
Daaah,,,aisee huyo dada kitaalamu tunamwita 'mashine' maana kawazidi ukauzu hata baadhi ya wanaume wanaopenda kulialia,,,,LAKINI mkuu, kama sekta zingine yuko vzuri na kupakua wapakua, wewe shida yako ni nini hasa????
 
Duuuh huyu Kaka ana umri wa mama yang mzazi ana 43 na ana watoto watatu na mim mkubwa nimemaliza chuo Lakin huyo Kaka bado anahangaika hatak kuoa ,, nakuonea huruma na umri unavyozidi kwenda
 
unafkiOTE="wigo, post: 18162409, member: 156965"]Love is feelings, kama huna hisia nae ya nini kuwa nae, acheni unafiki.[/QUOTE]
ni kujinunisha ili ubebembelezwe.
 
Alifaa kuwa na Mimi huyo hapendi kuudhi moyo wake kwa sababu ndog ndogo kama hizo.mapenzi humuumiza aside yajua.Hugo ni mkomavu kwenye game na usimbadili maana ukimbadili utateseka sana .
 
Mianaume mingine km viazi mbatata. Viwekwe jikoni viive viliwe tu basi. We Mungu amekupa dhahabu unaanza ih sijui shaba sijui bati iko km dhahabudhahabu vile! Mpewe nn mridhike nyie manunda wa aina hii? Akuoneewivu? Wivu wa nn sasa? Akiona wivu utasikia kazidi wivu huyu hana wivu ishakuwa kosa lol SHAMEUPON U BRO. JITATHMINI UPYA NA UHESHIMU EGO YA MWENZIO!!!
 
Jaman kumbe mmezoea kubembelezwa, naona mi naendana na huyo dada kidogo.. swala la kubembeleza mtu mzima linahitaji kipaji aisee....ila mzoee tu ndivyo alivyo, inawezekana anakuonea wivu sema hataki kabisa kukuonyesha usije ukatake advantage. Maana mtu akijua anapendwa always inakuwa shida
 
Mkuu ! Huyo demu anavuta bangi ! Kweli tena... ! Wavuta bangi ndivyo walivyo katika mahusiano.. ! Huwa wanakosa bashasha kabisaaa ! Hawanaga interests wala nini ! Mtu akuwa amelizika kwa kila kitu..!
Kuna ukweli hapa. Vp hatumii kilevi cha aina yoyote
 
Huyo dada nahisi ni FBI, yaani ana data zako zote hovyo anakusoma namba tu. Arobaini zako zikifika ataachansa na huo ushamba wako wa kukaa unamu-try kama gari!! Please, usi mu-drive atakuacha!!
 
Back
Top Bottom