zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Habari za asbuhi wana jukwaa bila kupoteza muda embu twende moja kwa moja kwenye mada
MWANZO
Hannibal barca alizaliwa mnamo mwaka 247 BC... alikua jenerali wa jeshi la CARTHAGE yaani Tunisia ya leo na alipata umaarufu hasa kwenye vita vyake dhidi ya dola ya kirumi na mataifa mengine makubwa ya ulaya kwa wakati huo zilizofahamika kama PUNIC WARS
Jenerali huyu Alitoka afrika na kuweza kuvamia bara la ulaya kupitia Iberia yaani ureno na spain akiwatandika wote waliomzuia njiani kwa kutumia mbinu za kimedani bora zaidi kuwahi kushuhudiwa wakati ule.... Na umaarufu ulipanda zaidi alipovamia ITALIA kwenye moyo kabisa wa dola la kirumi na kushinda vita tatu muhimu dhidi ya dola hiyo kwenye miji ya trebia,trasimene na cannae. Nguvu zake ziliweza kuitia hofu dola hii kiasi walikuwa wakisikia jina lake wanatetemeka!!!
Katika moja ya vita kubwa kabisa ni vita ya cannae ambayo kihistoria ndio vita ambavyo Dola ya kirumi ilipoteza wanajeshi wengi zaidi kati historia ambapo wanajeshi elfu 80 walifia hapo huku masenator 80 wakichinjwa.... Kibaya zaidi alilizunguka jeshi zima la Rumi hivyo hakuna masalia waliopona na tokea hapo jeshi la Rumi liliogopa kupigana vita ya uso kwa uso na Hannibal Barca
Hannibal Barca Aliendelea kuitawala italia kwa miaka 15 lakini jambo ambalo mimi najiuliza mpaka leo na nimekosa majibu ni kwanini General Hannibal Barca aliyeogopeka dunia nzima ya kale aliwatandika warumi kwenye vita zote alizokutana nao ila alisita kuvamia Rome?? Je nini kilimzuia asivamie?? Aliogopa nini??
MBINU ZAKE VITANI
Hannibal anafahamika zaidi kwa kutumia tembo kwenye uwanja wa vita.... Alikuwa anatumia tembo mkubwa wa jamii ya syria ambao kwa sasa wametoweka hivyo ukubwa wake ulikuwa ni kama vifaru vya kijeshi vya sasa..... Aliwatanguliza mbele tembo kama 80 kiasi kwamba mpaka mnamalizana na tembo mnakuta mshazingirwa na kupewa kipigo cha mbwa mwizi
MWISHO WAKE
Baada ya kupata taarifa kuwa nchini mwake wamevamiwa ikabidi arudi kuokoa jahazi na kufikia muda huo mbinu zake za medani zilikwisha somwa vizuri na jenerali scipio Africanus wa dola ya Rumi ambaye alitaka kulipa kisasi baada ya Hannibal kumjeruhi vibaya baba yake kwenye ile vita ya trebia hivyo akampiga hannibal huko mjini ZAMA nchini Carthage (Tunisia) na baada ya hapo Hannibal Barca aliranda randa sana ulaya na mwishowe alisalitiwa na kurudishwa kwa warumi ila aliamua kujiua kwa kunywa sumu ili kuepuka dhahama ya kuangukia mikononi mwa maadui zake.
HITIMISHO
Jenerali huyu anatazamiwa kuwa mwanajeshi bora kuwahi tokea katika historia za kijeshi hapa duniani ila swali nalotaka mnisaidie great thinkers je ni kwanini General Hannibal pamoja na kuwatandika dola ya rumi huko italia aliogopa kuvamia roma ambayo ingeifuta rasmi dola ya kirumi kwenye uso wa dunia????
Naomba kuwasilisha