Mkuu asante kwa hoja nzuri na yenye kuchangamsha akili. Lakini kama kawaida yangu mimi nitakupa majibu kwa kutumia kitabu pendwa nikipendacho kuliko vyote, yaani "BIBLIA"; kitabu hichi kina majibu yote ya swali ulilouliza ingawa watu wengi wanakidharau.
Iko hivi utawala wa Rumi ni moja kati ya tawala tano kubwa zilizotabariwa au kuruhusiwa na MUNGU kuwepo hapa duniani, rejea kitabu cha DANIEL 2:36-44 ambapo utaona Danieli anamfafanulia Mfalme Nebukadreza ile ndoto yake ya sanamu kubwa. Katika ile ndoto, sehemu moja ya ile sanamu ilikuwa ni Ufalme wa Rumi, yaani ile miguu ya chuma.
Sasa basi kwa kuwa Ufalme wa Rumi ulikuwa umeshatabiliwa na MUNGU kuwa utatawala dunia yote kwa wakati ulioamuriwa, isengekuwa rahisi kwa General Hannibal pamoja na jeshi lake kuivamia Roma na kuuangusha Ufalme wa Rumi. Fahamu kwamba nyuma ya hizi falme kubwa huwa kuna nguvu ya ajabu inayoziongoza, nguvu hiyo inaweza ikawa imetoka kwa MUNGU au inaweza ikawa imetoka kwa yule Mwovu Lusifer Ibilisi.
Kwa Ufalme wa Rumi, hata kama ulitabiriwa na MUNGU, lakini nguvu yake ilikuwa inatokana na Lusifer Ibilisi; rejea kitabu cha UFUNUO 13:1-2 .........yule joka(Lusifer) akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi(Ufalme) na uwezo mwingi(Nguvu za kijeshi). Hivyo basi kutokana na nguvu alizopewa Rumi, isingekuwa rahisi kwa General Hanniba kuivamia Rumi na kuindoa kwenye utawala wa dunia.
Utaona kwamba hata baada ya kifo cha General Hannibal bado utawala wa Rumi uliendelea kuwepo kwa miaka zaidi ya elfu moja. Isitoshe Hannibal Barca yeye na utawala wake hawakutabiriwa kuitawala dunia hata kama walikuwa na nguvu kiasi gani.
Mkuu zitto junior kitabu hichi BIBLIA kina majibu yote, hata kama utaamini au hautaamini, lakini UKWELI ndiyo huo.
mkuu Bibilia pia inasehemu ya Jibu kwa nini Rumi haikushindwa.
Ilitabiliwa haitashindwa katika mfululizo wa tawala zile nne.
Pia nguvu ya rumi haitakwisha kabisa hadi Yesu anarudi.
Pia Hakutakuwa na Dola jingine kubwa zaidi ya Rumi ya wakati wake duniani, hata US ananguvu lkn zinamipaka sio kama zile na wenda nguvu yake inakuwa boosted na rumi hiyohiyo.
Note:
Msingi wa Ufafanuzi wa Unabii uliouweka wa Daniel 4, 7 na Ufunuo 13 ni Day/Year approach in interpretation of Biblical prophesies.
Msingi huo licha kuwa msimamo wa Wasabato, Waprotestant wa enzi za karne ya 16 waliamini (ukiacha hawa wa sasa ambao wengi ni product ya counter-reformation). Hata Commentaries za Mzee Jerome mkristo wa huko Uyahudi aliyecompile Bibilia ya awali kwa kilatini kibovu VULGATE alikuwepo siku Dola hilo linaanza kuanguka na commentary Yake alionyesha kabisa kinachotokea ni Utimilifu wa Unabii wa Daniel. Sio yeye tu na wengine wengi hadi wanasiasa wakina napoleon na wakina Hitler walielewa historia hizo.
Na hata mwanahistoria wa Muda wate wa kiingereza Gibbon kaeleza hayo katika maandishi yake ambayo ulaya nzima wanaamini maandiahi yake ni source za kuaminika za kihistoria. Kaeleza kwa kina katika series za Volumes zake za RISE AND FALL OF ROMAN EMPIRE.
Maoni Kwa Nini Huyu Mwafrika Hakufika ROME na KUTAWALA Dunia ya wakati huo.
*Isingewezekana kwa sababu haikuwahi kutabiriwa hivyo katika unabii wa Muda mrefu hadi Dunia Inapota (sababu ya kiimani).
*Kwa Mujibu wa wananzuoni Marhabar alimwambia Hannibar, " You know how to gain a Victory, But Hannibal You know not how to use one''.
Kushinda Vita ni kitu kimoja, lkn kutakeadvantage ya huo ushindi ili kusukuma malengo makubwa ya kidola ni kitu kingine.
Wananzuoni wanamchambua Hannibal wakisema, Alikuwa amebobea kwenye MBINU ZA USHINDI, LAKINI HAKUWA NA MIKAKATI BAADA YA USHINDI.
Hata mipango yake mingi ilikuwa ya kimbinu zaidi (tactics) huku ikikoswa mikakati (Stratergies).
Mfano.
Alipigana vita mahususi na kupata ushindi ambao kama angekuwa na mikakati na maono ya mbele angeingia Roma na kutawala licha ya kuwa na jeshi dogo. Katika Ushindi wake pale CANNAE. Habari hizo za ushindi ule ziliwatetemwsha warumi wote, waliogopa sana na kama angeamua kusonga mbela akeiteka Rumi lkn hakuwa na mikakati na hakuona nje ya mbinu zake za kivita, akaamua kurudi Hispania alikotokea.
*Sababu nyingine Kulikuwa na mgawanyiko katika utawala wa Carthage. Wakati Barca anatafuta Ushindi mkubwa na kutawala njia zote za kiuchumi eneo hilo ambazo zilishikiliwa na Rumi, wakati huo akipambana kutokea Hispania alipokulia na kuandalia mikakati. Baadhi ya watu wa utawala huko Tunisia sehemu ya dola ya Carthage hakuunga mkono hilo wakiogopa vita kama vile vya kwanza enzi za baba yake Hannabal. hivyo hiki nacho kikawa ni kigezo. Ni sawa na kuwa na serikali yenye watu wenye maono makubwa huku wengine au baadhi ya watendaji kuyapinga.
*Sababu nyingine ni Mgawanyiko. Kikosi kilichoongozwa na kaka yake Hasdrubal Barca kilibaki Hispania. kulinda hiyo ngome yao huku Barca yuko huko italia anapambana na kikosi chake kidogo chenye mbinu za uhakika. Warumi walijua kumdhohofisha ni kwenda kushambulia na kupashohofisha maana wasingeweza kudhubutu kushambulia kutokea tunisia kwa sababu ufukweni hao carthage wangeshindwa. Hayo yalikuwa maono ya Cornelius na Scipio (mtoto wake alitimiza hayo maono), na hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kumtoa humo italia.
*Sababu nyingine Barca hakupata uungwaji mkono mkubwa na baadhi ya makabila huko italia kama alivyowashawishi wahispania kujiunga na jeshi lake. inasemekana wale jamaa hawakuonyesha ushirikiano wa kutosha hivyo kumfanya akose nguvu kiasi.
*Sababu nyingene Tofauti na waCarthage warumi wao walikuwa na umoja na maono yao waliyaunga mkono wote licha ya changamoto. Objective ya Taifa la warumi ilikuwa moja Tu, wao waendelee kuwepo kwa kutokuwepo kwa Hannibal Barca kwa gharama yoyote. Wakazi wa rumi wote hadi watumwa wao walikuwa nyuma ya serikali yao. Walijitolea hata kulipa kodi za ziada ili Jeshi lao lifanikiwe.
Umoja ni Nguvu
zitto junior
Malcom Lumumba
Red Giant
wakuu karibuni kwa kudadavua zaidi,