Hans Pope, jeuri na kisiki

Tupeni historia kamili ya zacharia Hans pope, kidogo inavutia kuijua
 
Hana historia yoyote ya maana kwa taifa hili. Labda kama siku hizi tumeanza kutukuza watu wanaopindua na kuondoa madarakani viongozi waliochaguliwa na wananchi kidemokrasia.
Mbali na harakati za uhaini, Zacharia Hans Pope ni mfanyabiashara maarufu aliyeajiri makumi kama sio mamia ya watanzania ktk makampuni yake aliyowekeza ktk logistics nk . Zacharia Hans Pop amekuwa Rais wa wawekezaji wa logistics Taifa kwa muda kadhaa sasa hivyo ni mdau muhimu sana ktk uchumi wa Nchi hii. Kama hayo hayatoshi huwezi kuzungumzia maendeleo ya soka la TZ bila kuuhusisha mchango wa Hans Pope ndani ya klabu ya Simba na soka kwa ujumla wake sasa sijui unataka sifa gani ili mtu awe VIP?
 
Kitendo cha yeye kushiriki katka jaribio la kumpindua rais aliyechaguliwa kidemokrasia kinamfanya kuwa mtu wa kawaida katika taifa hili mpaka atakapoingia kaburini. Ndio maana hivyo vyeo atavipata huko huko private sector. Hawezi kugombea ubunge wala urais wa nchi hii kwa sababu moja kubwa kwamba ana historia chafu ambayo haiwezi kufutika kwa kuifadhili Simba au kuwa na malori mengi.
 
Ila baba yake kwenye vita ya Uganda alisifika sana kwenye medani na aliitwa 'Black Mamba' ingawa yeye ni mweupe- nadhani alijipaka tope au masizi. Kwa hiyo ujeuri wake ni wa urithi. Kutoka hela mpaka kuwa tajiri siyo mchezo.
Huyo black mamba unayemsema wewe sio baba yake mzazi na Cpt Zacharia Hans Pope bali black mamba (a.k.a) alikuwa Major General Walden ( marehemu) mmoja kati ya technical commenders aliyeongoza kwa ufanisi mkubwa vikosi vya JWTZ vilivyojulikana kama Amphibians troops ktk vita vya Kagera. Sasa baba yake Cpt Zacharia aliitwa Hans Pope (marehemu) huyu mpaka anauawa alikuwa RPC.
 
Jamaa anajiamini sana, ila ana historia kubwa katika nchi hii tangu enzi za nyerere, Wachache tunamfahamu.
Nakumbuka makeke yake mitaa ya magomeni na angekuwa na busara hii leo asingeitunishia serikali misuli maana historia yake siyo safi
 
Mbona story yako haileti maana haiwezekani gari lipite likiwa empty halafu liwelimezidisha uzito, hizo ni porojo...!!
 
Alifanya hivyo sababu alikwa Raisi wa umoja wa wawekezaji wa logistics Taifa.
 
Hapo kama ndiyo hali ipo hivyo namshauri awe mpole maana atasahaulika ktk dunia ya wafanya biashara
 
Asante sana mkuu
 
Ok, lakini kumbuka reliability aliyonayo sasa baada ya msamaha wa Rais ambaye kikatiba ni holder of prerogative MERCY
 
Jamaa anajiamini sana, ila ana historia kubwa katika nchi hii tangu enzi za nyerere, Wachache tunamfahamu.
Nakumbuka walitaka kupindua nchi Mwl.Nyerere ana huruma sana waliwekwa ndani tu na baada e wakatoka.
Actually the man he is a soldier,you can imagine
 
Zacharia Hans Pope,,,kapataje utajiri wa kutisha namna hii sabab jamaa ana mihela balaaa,malori kama daladala so unajiuliza kutoka mwanajeshi,then jela halafu bonge ya tajiri ha ha ha kweli hii ndio tanzania...

Yote kwa yote namkumbuka zaid kwa kauli yake kuhusu yanga baada ya kuwapumulia na kuwalowesha yanga bao 5 aliwaambia tumewapa SUPU YA MAWE NA PILIPILI YA MIIBA
 
Huyu Hans Pope nakumbuka aliwahi kujibizana na waziri mmoja kwenye serikali iliyopita kama sikosei, sijui ni waziri gani kuhusu mizani na magari yake kuzidi alimjibu vibaya sana aisee yaani mpaka niliona aibu mimi mwenyewe!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…