Hans Pope, jeuri na kisiki

Hans Pope, jeuri na kisiki

Ok, lakini kumbuka reliability aliyonayo sasa baada ya msamaha wa Rais ambaye kikatiba ni holder of prerogative MERCY
Tupatie kiundani mkuu Kipindi anapanga Hayo mapinduzi alikuwa na wadhifa gani Jeshini mwaka gani?? na Akina nani walikuwa pa1 nae na alifungwa gerezan mwaka gani na Alisamehewa na kutoka Gerezani mwaka gani?? Na Je! Kesi ya uhaini INA msamaha???
 
Huyu Jamaa ninachomfaham n Kiongozi simba.. Zaidi mshua kamlinda sana maweni... Mshua kahamia Butimba nayeye wakamuhamisha BUTIMBA.. Huwa ni story za mshua kila akimsikia nikiwa nae Karibu..
Kwa nini Baba ako alipokuwa Maweni Na Zacharia Apelekwe Maweni je! Kulikuwa na connection yoyote au ilitokea kwa Bahati mbaya?? Na kwa nini Baba ako muda mfupi baada ya kuhamishiwa Butimba ZAKA nae akahamishiwa Butimba??ilikuwa ni kupangwa au ilitokea kwa Bahati mbaya?? Na kwa nini BABA ako amsaidie sana ZAKA gerezani je! Alikuwa na maslahi gani na ZAKA??Au alikuwa na maslahi gani ktk kesi ya uhaini ya ZAKA??? Ukitujibu haya maswali utakuwa umetusaidia sana
 
Yap mkuu huyo Jamaa kwa Mara ya kwanza Alikuwa Gereza Maweni ambapo ndipo mshua alianzia kazi 1986, 1989 mshua akahamia Gereza kuu Butimba na huyo Jamaa muda mchache nae wakamuhamishia Gereza Butimba-Mwanza...
Nimepewa stori zake alipo kua shimoni, zinasisimua.
 
Kwa nini Baba ako alipokuwa Maweni Na Zacharia Apelekwe Maweni je! Kulikuwa na connection yoyote au ilitokea kwa Bahati mbaya?? Na kwa nini Baba ako muda mfupi baada ya kuhamishiwa Butimba ZAKA nae akahamishiwa Butimba??ilikuwa ni kupangwa au ilitokea kwa Bahati mbaya?? Na kwa nini BABA ako amsaidie sana ZAKA gerezani je! Alikuwa na maslahi gani na ZAKA??Au alikuwa na maslahi gani ktk kesi ya uhaini ya ZAKA??? Ukitujibu haya maswali utakuwa umetusaidia sana
Hujanielewa mkuu Sio kwamba kamsaidia namaanisha kamlinda kama ambavyo askari jela wanalinda wahalifu tu.. Pia ilitokea tu kwa bahati kumbuka maweni ni Pa kawaida I mean hata ulinzi wa pale si mkali sana.. Asa wakamuhamisha pale kulingana na uzito wa kosa lake na Sababu za kiusalama zaidi MKUU...
 
Tupatie kiundani mkuu Kipindi anapanga Hayo mapinduzi alikuwa na wadhifa gani Jeshini mwaka gani?? na Akina nani walikuwa pa1 nae na alifungwa gerezan mwaka gani na Alisamehewa na kutoka Gerezani mwaka gani?? Na Je! Kesi ya uhaini INA msamaha???
Mzee Mwinyi aliamua kuwasamehe tu hata kama sheria hairuhusu msamaha kwa Mhaini. Alimsamehe hata Doris Liundi aliyetiwa hatiani kwa kesi ya mauaji. Huyo ndio Mzee Ruksa bwana yeye ni huruma na si sheria iliyomwongoza.

Hadithi kuhusu Pope kuhusika na mapinduzi ni ndefu na kwa kweli siijui kindani zaidi ya nilivyosoma makala za Gazeti la Rai kama miaka kumi iliyopita hivi. Kwa kifupi yeye alimkuwa JWTZ na alishiriki ktk mapinduzi ya serikali yaliyoshindwa mwanzoni mwa 1980s.
 
Asante kwa information mkuu.
Ila baba yake kwenye vita ya Uganda alisifika sana kwenye medani na aliitwa 'Black Mamba' ingawa yeye ni mweupe- nadhani alijipaka tope au masizi. Kwa hiyo ujeuri wake ni wa urithi. Kutoka hela mpaka kuwa tajiri siyo mchezo.
 
Jamaa anajiamini sana, ila ana historia kubwa katika nchi hii tangu enzi za nyerere, Wachache tunamfahamu.
Historia ipi hiyo zaidi ya uhaini uliompeleka jela na kutoka kwa msamaha wa Rais Mwinyi?
 
Hana historia yoyote ya maana kwa taifa hili. Labda kama siku hizi tumeanza kutukuza watu wanaopindua na kuondoa madarakani viongozi waliochaguliwa na wananchi kidemokrasia.

Hans Poppe amekuwa anafuatiliwa na usalama hadi enzi za Kikwete ndio wakaacha. Alikua katika kundi lilitoshutumiwa kutaka kumpindua Nyerere '82
 
2015 wakati wa kampeni chadema waliaandaa harambee ilirushwa live na tv kama sikosei alihudhuria harambee ile na pia aliichangia chadema ndio nikajua jamaa sio mwanaccm. na nilishasikia jamaa haipendi kabisa ccm
 
Zacharia Hans Pope,,,kapataje utajiri wa kutisha namna hii sabab jamaa ana mihela balaaa,malori kama daladala so unajiuliza kutoka mwanajeshi,then jela halafu bonge ya tajiri ha ha ha kweli hii ndio tanzania...

Yote kwa yote namkumbuka zaid kwa kauli yake kuhusu yanga baada ya kuwapumulia na kuwalowesha yanga bao 5 aliwaambia tumewapa SUPU YA MAWE NA PILIPILI YA MIIBA
Hans Pope ni chotara ndugu zake wengi wako Ujerumani mambo safi baada ya kutoka jela walimpa mtaji wa kutosha akafungua biashara
 
Story za vijiweni;Black Mamba ni Mayunga sio baba yake Hans!!Baba yake Hans alikua Polis na ni mmoja wa watu wa mwanzo kuuawa na mashambuliz ya Amin Kagera
Mayunga ndie alikuwa anaitwa black mamba ? Hebu jaribu kukumbuka tena
 
Back
Top Bottom