Super, nakubaliana nawe kwamba Wachina wa zamani sio wa sasa hivi, ndio maana hata Serikali yao ikipata taharifa kwamba kuna rushwa imetembea kwenye major projects zao, basi wahusika wanahukumiwa fasta na kupigwa risasi ya kisogoni bila simile. Nchi za Kiafrica zinazo shirikiana na Wachina kwa karibu kasi yao ya maendeleo ni kubwa sana, ndiyo maana Kenya inafanya kila liwekenalo kuwa nao sambamba, Uganda nayo imewapa Wachina major projects, DRC nk - ndio maana wakina M7, Kenyatta na PK wamewapa Wachina project ya ku-modernise Reli ya kutoka Mombasa mpaka Kigali - ninavyo wajua wachina reli hii inaweza kukamilika ndani ya miaka mitatu/minne kama watafanya kazi usiku na mchana, wafanyakazi wa kichina hawahitaji kukaa kwenye a five star Hotel au kutuletea a tall order zisizo na mshiko! Taifa letu kama liko serious ku-modernise i.e kutandika reli yetu in standard gauge basi Wachina ndio wanaweza kutandika reli hii kwa kasi, kwanza kiwanda cha kutengeneza sleepers kipo Mbeya, ballast zinapatikana huko Mbeya na Dodoma/Morogoro kama sikosei - kitu ambacho Wachina wata-import kutoka kwao ni reli na machine za kumwaga ballast na kutandika reli basi, sasa Mungu akupe nini? Tukifanya makosa na kutegemea nchi za magharibi ambazo wakati mwingine hazieleweki vizuri/vigeugeu tutakwama.