Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,581
Mkuu hili jambo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi. Hakuna nchi duniani ambayo imnatembeza malori mabarabarani kwa km 1000 yakiwa yamesheheni mizigo. Tunaambiwa gharama ya kutengeneza km 1 ya barabara hapa Tanzania ni zaidi ya Tshs. 1 billion lakini barabara hizo zinaharibika mapema sana kwa sababu ya mamizigo ya malori.
Mizigo inatakiwa ipite kwenye reli. Mfano toka Dar hadi mwanza unakutana na malori zaidi ya elfu kwa siku yote yamejaa mizigo, kwa nini mizigo isibebwe kwa reli? Tukiangalia bandari tu bila kuangalia barabara basi tutaishia kukusanya mapato ya bandari na kuendelea kujenga na kukarabati barabara kila kukicha.
Nampa Big Up Dr. John Pombe Magufuli kwa jitihada anazofanya katika kujenga barabara na kuhakikisha barabara zinadumu. Dr. Magufuli wafanyabiashara wanachokijua ni faida tu hawaelewe kuwa barabara zinaharibika mapema na wahandisi wako kuambiwa wamechakachua kumbe ni uzito wa malori. Endeleza mapambana kwa faida ya watanzania wote.
tatizo ni kwamba hata hao wanasiasa nao wanahusika sana na umiliki wa malori,,,,hao wamilik wa malori ndio wafadhili wa siasa na ndo wanasiasa,,,,na mi nahis wanasiasa wanaihujumu reli ili tu waneemeke,,,,,