Well said mkuu, jamaa hawa hawamtaki Magufuli kutokana msimamo wake na anaelewa ubaya wa magari ya mizigo kuzidisha uzito - barabara zinagharimu fedha nyingi sana kuzijenga na kuzikarabati, unlike permanet way ya reli ambayo haigharimu sana kui-maintain unless kukitokea derailment kubwa ya kuharibu mataruma, nayo ni nadra sana. Mambo ya kudai eti Magufulini sio injinia hayana mshiko wowote - Magufulini ni mwana sayansi yuko well versed na nyanja zote za Sayansi including Engineering sio mbumbumbu kama wafanya biashara wanavyo mfikiria, wala siwezi kushangaa kama baadhi ya Wafanya kazi wizarani mwake nao wanachangia kutaka kumkatisha tamaa Mzalendo Magufuli wakishirikiana na Wafanya biashara wakubwa wa malori ili aondolewe wizarani, kuna kamkakati ka aina fulani hapa si bure. Hakuna Serikali ambayo inaweza kuruhusu watu wenye nguvu za fedha kufanya wapendalo bila ya kufuata sheria, tukilaza damu tukakosa kuwa wangalifu katika utunzaji wa barabara zetu kwa kuogopa lawama za uongo na kweli, basi effort zote za utawala wa JK katika nyaja za miundo mbinu za babaraba zitakwenda na maji - tukumbuke matajiri wa malori wanacho jali ni kusafirisha mizingo bila kujali uzidishaji wa uzito wa mizigo inapo bidi. Mimi nashindwa kuelewa kwa nini Serikali yetu inaonekana kusua sua katika suala la kukarabati/kujenga upya reli yetu ya kati, kwa nini hachangamkii suala hili? - 'am sorry kusema sioni kama kuna dalili zozote za kipa umbele katika suala hili!! Jana ndio niliona gazetini tenda ya kujenda/karabati reli ya kuzunguka Dar na siyo ya kwenda Bara. Swali ni, lini Serikali itahanza kutandika reli mpya yenye standard gauge kwenda Bara, kwa nini project hii amuwapi Wachina ambao wengechukua muda mfupi kuikamirisha badala yake tunakimbilia kwa Wajapan ambao hatuna uhakika kama watatujenga reli kweli au la, wenzetu wa Kenya na Uganda watatuzidi kete baada ya kuomba msaada kutoka kwa Wachina ili wa modernise reli yao 2 standard gauge, narudia kuhoji tena hapa kwetu kuna nini lakini? Au cartel ya wasafirishaji wa barabara ndio wanaweka spana katika utandikaji wa reli mpya kwenda bara - I might be wrong, lakini lolote linawezekana katika Taifa letu - ucheleweshaji wa utandikaji wa reli mpya kwenda bara siwa kawaida hata kidogo! Hata kama wenzetu usema "there's no hurry in Africa" binafsi katika hilo naona Tanzania tumezidi kuwa dead slow kuanzisha Project ya ku-modernise reli ya KATI ambayo ni lifeline ya TAIFA letu kusema ukweli.