Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

nafikiri ni muhimu kwa serikali yetu kufikiria jinsi wanavyoweza kuimarisha reli ili kuondoa kabisa kutegemea hawa watu wa malori. usafirishaji kwa njia ya reli ni bora kuliko malori yanayoharibu tu barabara. kama wakigoma najua athari zitatokea lakini hata zikitokea, wataiamsha serikali kuimarisha reli ili kupunguza utegemezi kwa maloli.
huu ujinga ndio Nyerere aliukataa watu wakamuona mjamaa, hapendi maendeleo ya watu e.t.c kumbe ni kuzui nchi kuwa held hostage na wafanya biashara uchwara.
 
nafikiri ni muhimu kwa serikali yetu kufikiria jinsi wanavyoweza kuimarisha reli ili kuondoa kabisa kutegemea hawa watu wa malori. usafirishaji kwa njia ya reli ni bora kuliko malori yanayoharibu tu barabara. kama wakigoma najua athari zitatokea lakini hata zikitokea, wataiamsha serikali kuimarisha reli ili kupunguza utegemezi kwa maloli.

Nakuunga mkono,hawa ndio hawataki reli inaoonekana wamemonopolize sekta ya usafirishaji,Serikali iimarishe reli kukiwa na ushindani hawana wakumgomea.
 
Nakuunga mkono,hawa ndio hawataki reli inaoonekana wamemonopolize sekta ya usafirishaji,Serikali iimarishe reli kukiwa na ushindani hawana wakumgomea.

WAcha wagome tuwekewe reli .udhiya ukome wanaharibu barbar.
 
attachment.php

Kwa hiyo hawa watakosa pesa za kunywea?
 
attachment.php

Kwa hiyo hawa watakosa pesa za kunywea?
Hivi huyu ndie Kamanda Mpinga? ni sheria kweli kunywa na uniform za kijeshi?
And then hawa jamaa ndio maana hutengeneza foleni sana njia panda za Tazara,Kamata,Banda la Ngozi,Ubungo Mataa Mwenge n.k kwa nini wasiache taa zifanye kazi zenyewe maana zinawashnda akili
 
Katika maelezo yako hakuna tuhuma dhidi ya Magufuli, umezungumzia sheria mbaya na watendaji wabovu, hapo Pombe anahusika vipi? Hayo tuaache, hivi kwa mtu mwenye akili anaweza kulinganisha barabara za Botwana, Afrika Kusini na Australia na za hapa Tanzania? Hivi kweli mtu huyu yuko serious au ana chuki binafsi na Magufuli!

Kwa kifupi ni kwamba, huwezi kulinganisha nchi za wenye akili na ya kwetu kwenye nyanja yotote ile, iwe ni kwenye elimu, michezo, sayansi, miundombinu, uwajibikaji wa serikali, usafirishaji, fedha na uchumi. Sisi ni uzembe, rushwa ufisadi na ukandamizaji wa haki za raia ndo mwendo wetu. Magufuli anajitahidi sana kumbuka wizara hiyo walishapewa akina Chenge na Kawambwa lakini waliondoka hata barabara moja haikukamilika bali gharama za ujenzi wa Km moja ya Lami ili shoot...why?

Mkuu kwa uelewa wangu nafahamu kuwa magufuli ndiye kiongozi aliyeshika dhamana ya kuiongoza seckta hiyo, hivyo kama kuna mapungufu au maboresho tunategemea yeye ndiye mhusika mkuu, na kama ameshindwa kufanya jitihada ndani ya uwezo wake basi zigo la lawama limwangukie yeye ,hapa ndio viongozi wenye busara hujiuzulu pindi wanapoona uwezo wao umefikia mwisho,

Nia ya kutoa mfano wa barabara za botswana na rsa si kulinganisha cost za maflyover pamoja na undergroundround roads ambazo ni kweli Tanzania hatuwezi kuzimudu, bali ni kuonyesha jinsi sheria za huko zinavyotumika kutetea lifespan ya barabara zao. Mkuu ,si barabara zote huko ni world standard !! , nao wana barabara za kawaida sana baadhi ya maeneo, yet zinadumu. mfano bloemfonetein to port elizerbert , au portgesrust to botswana (kopfontein) naweza kusema hazina ubora ukilinganisha na barabara ya chalinze mpaka morogoro (n.b kama ukiondoa matuta yetu). Kwa taarifa tu, Zambia hawana barabara za gharama kama sisi, wanatumia mfumo wa axle kama botswana na rsa na bado barabara haziharibiwi na malori kama zetu, Australia nimekupa mfano wa jinsi the same tools zinazotuharibia barabara kwetu zinavyoweza kubeba mizigo mizito safely bila kuharibu barabara zao ,just because wenzetu wameruhusu idadi ya axle, nadhani mpaka axle 16 bado ni kawaida huko(normal haulage)

Same set ya sheria tunazotumia ukizifanya zitumike kwa wenzetu, muda mfupi tu nao watalalamikia malori kama tunavyolalamika sisi, kumbuka hata barabara imara unazozijua nazo zina kiwango cha kuvumilia (tolerance). sheria za barabara na mizani ambazo magufuli anasimamia anatumia ubabe na kuzitukuza kamwe hazitaziacha salama barabara zetu.

Ni kweli Magufuli amejitahidi kwa kujenga barabara za lami ,lakini je zinasimamiwa na sheria gani ndio alipochemka! binafsi sioni tofauti nawa ujenzi wa shule za kata ambazo hazina walimu,
 
In a nutshell magufuli anaonekana na watanzania kama mtu hodari na mchapakazi , kiuhalisia mimi naona kinyume chake.

Binafsi si msafiishaji wala sina uhusiano wowote na sekta hiyo , lakini ninasafiri sana kwa barabara nchi karibu zote za Sadc ,Suala la mizani na sheria zake zinazidi Kuwa tight hapa kwetu pengine kuliko nchi nyingine za sadc, na pengine ndo tunaongoza kwa rate ya uharibifu wa barabara kuliko wenzetu kwa sababu ya ubabe wa mtu mmoja tu, MAGUFULI !!!
Uharibifu wa barabara. Kwa kiasi kikubwa unatokana na sheria mbovu zilizowekwa na kusimamiwa na viongozi husika,kulalamkikia wasafirishaji ni sawa na kuficha ukweli wa tatizo, si kweli kuwa tunabeba mizigo mizito sana. Bali tuna utaratibu mbaya wa kubeba mizigo ndo maana barabara zetu hazidumu.

Kuna mawili huwa nafikiri dhidi ya wizara hii na watendaji wake, either wananufaika na rushwa kutoka kwa wasafirishaji hivyo wanaopt njia ambazo hazitatui tatizo bali kuiongezea.mzigo serikali na mtu wa kawaida au hawajui na hawako serious kuboresha pengne kuondoa kabisa sheria kandamizi zinazopelekea watu kutocomply.

Mfano Botswana idadi ya juu ya axle ni 9 urefu mwanzo hadi mwisho ni mita 22, hapa kwetu ni axle 7 na urefu hautakiwi kuzidi mita 17!!! put it simple unapokuwa na axle nyingi ndio unavyozidi kutetea barabara na the opposite is also true,
Ningekuwa mimi ndo magufuli nijuuliza swali moja kwa nini south africa wanabeba mizigo mizito yet road network zao zina lifespan kubwa kuliko zetu na pia hawana idadi kubwa ya mizani kama sisi . Na bado wakifika Tunduma wanaona ni afadhali kuoffload mizigo na kupakia kwenye malori yetu??

Hivi kuna hasara gani Tanroad ikiruhusu axle 9 na urefu ukawa 22 metre! !! Kwa nini Trailers za Inter link ambazo zinatuika karibu africa nzima hapa kwetu ni marufuku? remember Austalia wanabeba mpaka tani 80 kwa kuongeza idadi ya axle na kuto limit urefu! Na bado barabara zao zinadumu.

mkuu jibu ni kuwa barabara zetu ni za kisiasa!
 
Si ndio huyu alikuwa na kesi ya uhujumu uchumi enzi za mchonga, sasa na mbona maslahi gongana msafirishaji wakati huo huo ni mwenye mizigo. Yaani anasafirisha mizigo yake mwenyewe kwa nini asiongee na magufuri live.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mimi nasema hivi Magufuli akaze kamba kabiasaa haka ka ugomvi huenda kakatutoa watanzania. Mizigo yote siku zote inatakiwa isafiri kwa reli tu kupita barabarani iwe last resort huku kwetu ni kinyume reli imekua last resort matokeo yake gharama ya maisha inapanda na mbaya zaidi barabara zetu hazidumu kwa sababu ya kuelemewa. Kingine ajali zinakua nyingi ukizingati ni vijibarabara na wote tuna banana humo. Ni wakati mwafaka kwa Mwakyembe naye kuamka na kuimarisha reli zote ili zibebe mizigi hiyo. Kwa hili Magufuli namuunga mkono kwa sana!

Mkuu kuna mambo mengine huwezi ukabalance kwa simple equations!! , hata huko ulaya ,reli ina umuhimu wake na trucks zina umuhimu wake , ingekuwa ni simple kama unavyodhani probably kusingekuwa na manufacture anayetengeneza malori duniani coz ingekuwa proved ni useless kuyatumia.
 
Hata reli ikijengwa, bado tutahitaji malori, kwani reli haitaweza kufikisha mizigo hadi majumbani kwa watu au kwenye viwanda. Kuna mifano mingi ya nchi zenye mifumo mizuri ya reli lakini bado zina malori mengi. Nchi kama Uingereza hapa ni mfano mkubwa.

Nafikiri swala la kujiuliza hapa ni kuwa barabara zetu zina tofauti na barabara za Rwanda au Zambia ambako nako wana malori na haziharibiki?
 
Hizo barabara zimejengwa ili zikae urembo? wanaozidisha wanalipa faini na wasiozidisha wanapeta.

Kumbuka, barabara hata kama hukuitumia inaharibika.
Umenena FF. Magufuli na TANROADS wamezidi ubabe.
 
Hizo barabara zimejengwa ili zikae urembo? wanaozidisha wanalipa faini na wasiozidisha wanapeta.

Kumbuka, barabara hata kama hukuitumia inaharibika.

Inaharibikaje kama haitumiki? Umeniwacha njia panda.
 
Wakati Magufuli anaagiza magari yaliyozidi uzito yazuiwe, Mwakyembe aliendesha gari hadi kwenye mizani kwenda kuyakwamua mabasi mawili mapya mali ya raia wa Zambia, yaliyokuwa yamezuiwa (na Magufuli) eti hadi faini ya uzito ikalipwe Dar es Salaam, tena hadi Jumatatu kwani siku hiyo ilikuwa week-end! Nadhani hata Mwakyembe huwa anamshangaa sana Magufuli!

Mkuu hayo mabasi yalikamatwa kwa kuzidisha urefu unaoruhusiwa na si uzito!!

Ni hivi , watengenezaji wengi wa mabasi luxury marcopolo ,bus car ,irrizzar n.k wameopt kuongeza urefu ili kucompesate leg room na idadi ya abiria kwa basi , baada ya seat configuration ya 2x2 kuwa very popular, hapo zamani tulikuwa tunatumia configuration ya 2x3 ambayo kwa kweli ilikuwa very uncomfortable, ikumbukwe Zambia hawana length limit kwa mabasi na tayari wanatumia sana mabasi luxury marefu, kwa ilikuwa ni kituko kwao,

mabasi ya marcopolo 2010 model ambayo yalitumika kubebea mashabiki na wachezaji kwenye kombe la dunia mwaka 2010 na ambayo ni world standard ni kosa kuyatembeza hapa Tanzania kwa mujibu wa sheria za Tanroad.

Huwa najiuliza hivi hawa watendaji wetu kama kweli wako serious, unawezaje kusimamia na kutekeleza sheria za barabara ambazo karibu dunia nzima inaona zimepitwa na wakati!
 
Na yale ya Rizi nayo yatagoma!! Tusubiri tuone...

Usiwe na nongwa za kike ,kama ni kweli anamiliki magari kuna ubaya gani???,au wewe ulitaka wamiliki wawe watoto wa Waarabu, wahindi na wasomali tu.
 
TANZANIA na watendaji wake bure kabisa, mkuu yeyote akitaka tozo mwaka huu liwe kubwa, basi moja kwa moja watendaji hawafikiri mradi malengo waliyoambiwa yafike hata ukiwa compliant vipi , ili baadaye wasifiwe . nilimsifu manager mmoja wa TRA aliwahi kuwaambia watendaji wake msifukuzane na mlipa kodi mtafuteni muelimisheni then ataingia katika orodha ya mlipa kodi na kama anadaiwa mpeni mazingira ya nafuu ya ulipaji , lakini zamani TRA waligeuka mapolisi na ma defender yakawa yanabiringita kwa spidi kisa kukwepa kodi kumbe kwanza hata hajui aanzie wapi
 
Inaharibikaje kama haitumiki? Umeniwacha njia panda.

Ndio barabara huchakaa hata kama hazikutumika sana, baada ya miaka 15 lami upoteza uwezo wake wa kushikilia kokoto zile na ndio huanza kubomoka. Lakini uzito ukipita kipimo mara nyingi hata miaka 5 haifiki.
 
Back
Top Bottom