Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Ingawa ana mapungufu yake kama binaadamu,bado naamini katika utendaji wa Magufuli. Ukichunguza kwa sasa katika serikali,ni mawaziri wasiozidi watano ndio tunaona wanachofanya na ndio wanaoipa ccm proud japo kidogo.Kwa sababu wana uwezo wa ku call a spade a spade. Sasa mpotezeni Magufuli na hao wenzake wanne muone kama kutaonekana au kusikika utendaji wowote!
 
Huyu gaidi hans pope alitaka kumua nyerere mchana kweupe pale saint peter....tena kanisani. Anasumbuliwa na laana ya nyerere...kibaya zaidi nchi hii ina watu wasiotaka kuchambua mambo hayo eighteen wheeler sio kwa barabara nyepesi. Haya hebu turudi miaka ya themanini na tisini....mahufuli yuko kwa wananchi lakini wananchi hawaoni.
 
Hans poppe jiulize umelifanyia nini taifa hili kiasi cha kunshambulia Magufuli,kiongozi sisi wenye maono na nchi hii tunamuona kama mfano wa kuigwa?pili TATOA inawasaidia nini watanzania masikini aswa walioko vijijini ambao MAGUFULI anapambana na nyie mabepari ili kuwapelekea miundombinu barabara?
 
Nani kama Magufuli katika kuchapa kazi? kama hauamini nitafutia viongozi 10 wenye uwezo wa kusimamia sheria katika nchi hii kama Magufuli.Tuache wachache wazarendo wenye uwezo wa kusimamia sheria kama nguzo mama kwa taifa lolote lenye dira ya maendeleo watufundishe namna ya kuheshimu sheria.
 
Magufuli ni boot leaker tu. Amevurunda mara nyingi sana kuliko mawaziri wengi. Mara ngapi Pinda kapindua maamuzi mabovu ya Magufuli? Kama Magufuli asingekuwa mchumia tumbo tu angejiuzuru siku nyingi kwa kudhalilishwa mbele ya umma na kuvuliwa nguo hadharani kwanza na TATOA then na Waziri Mkuu Pinda.
Watu wengi wanadhani ukipiga kelele sana ndio ushahidi kuwa unajua kazi sana. Magufuli ni mweupe kabisa! Huwa najisikia vibaya sana nikimwona Magufuli akiramba viatu vya Kikwete mbele za watu bila hata tone la aibu! Mwanaume mzima! Baba mwenye watoto nyumbani! Mimi ningemkana kuwa baba yangu mtu kama Magufuli. Hakuna waziri yeyote anayemzidi Magufuli kwa kujikomba!
 
Hans Pope kichaa sana! Unataka uharibu barabara zetu kwa kubeba mizigo mikubwa!!!

Magufuri usirudi nyuma!!!
 
Linapokuja suala la reli vs barabara hapa ndio serikali hii huwa siielewi kabisaaaa bora wagome tena kwa muda mrefu ili tujifunze kwa njia ngumu
Nakuunga mkono. Nchi zilizoendelea mpaka na hata kesho wanathamini matumizi ya reli kwa ajili usafirishaji wa mizigo. Nimuomba Mungu mkuu Magufuli akomae wenye malori wagome zaidi, bandari ifurike, wateja wakimbilie Mombasa, labda mambo yakiharibika serikali itaweka vipaumbele vyake ktk mpangilio sahihi. Reli ndiyo mkombozi endelevu ktk sector ya usafirishaji mizigo. Reli ijengwe mpaka bandarini.

Serikali ifike mahali isifiwe kwa uboreshaji wa usafiri kwa njia ya reli. Kwa maoni yangu uwekezaja mkubwa kwenye mabarabara ni a "curse in disguise".

Komaa Magufuli, Komaa mwana wane!
 

Kuliko mawaziri wengine? Kama wepi hao?
 
Hatupaswi kuwatetea hawa jamaa wa malori, wameua barabara zetu zilizojengwa kwa kodi za wanyonge kwa kuzidisha uzito, wanatoka bandarini na tani 40 wakifika kimara wanaongeza tano sasa why wasipime mizani. Mabasi yakifika mizani yanaomba abiria kupungua au kusogea kati kuacha eneo la excel liwe jepesi au hilo nalo hatujui?. Magufuli kasimamia sheria ambayo mramba aliifuta kwa barua, kuna sheria inayofutwa kwa barua? Hili bunge nalo halijui wajibu wake
 
Ndie yeye, alitumikia adhabu yake kifungoni na aliachiwa huru mwaka 1995 kwa msamaha wa Mzee Rukhsa.

Ukitaka kujua Hans pope ni mhaini soma kitabu kinaitwa The Dark Side of Nyerere utajua kwanini aliitwa mhaini na wengine wengi
 


Umesikia kaka yake katoa go ahead!!!!!
 
Duuh jiwe tangu kitambo
 

Hizi zote zilikuwa ni alama za nyakati lakini hatukuziona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…