Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

Hans Poppe wa TATOA amchambua Magufuli

nkosikazi

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2010
Posts
361
Reaction score
337
Mhazini wa TATOA ambacho ni chama cha wenye malori Tanzania amemwita Magufuli ni mtu asiyejua na ambaye ana chuki kubwa kwa transporters na angeweza angewaondoa wote nchini kwa tuhuma za kufikirika kuwa wanaharibu barabara.

Amekwenda mbali zaidi kwa kusema anafikiria kuwa Magufuli anafanya makusudi ili apate mgao wake wa rushwa. Hii ni kwa sababu amewaagiza wafanyakazi wa mizani ya Iringa wawatoze faini wenye malori na kuuliza kwanini faini zinapungua. Hans Poppe anasema faini zinapungua kwa sababu transporters wamekuwa compliant so hawatakiwi kutozwa faini ovyo.

Amesema Magufuli ndio Waziri wa ovyo kuliko wote kwa kuendesha uongozi wa vitisho na amri za ovyo na kwamba mainjia wote wanamwogopa sana na wanasema hivyo.

Anasema ingawa Magufuli si injinia lakini elimu yake inatosha kutoa mwongozo mzuri ila anafanya makusudi.

Amesema amri ya Magufuli kuondoa tolerance ya 5% katika uzito wa mizigo ni kinyume cha sheria kwani hiyo ni sheria au taratibu iliyowekwa tokea zamani wakati Magufuli bado anasoma.

Kwa hitimisho wameamua kusimamisha malori yote kutofanyakazi kuanzia kesho.

Hii imetoka katika mahojiano na ITV 5 minutes ago. Ipo kazi!
 
Magufuri mtu makini sana wanabeba mizigo mizito sana wanatuharibia barabara.
Lets see what happens wakigoma. Bandari itasimama na meli hazitashusha mzigo. So kutakuwa na msongamano wa meli bandari ya Dar na kuifanya isikubalike zaidi. Wateja watahamia Mombasa kwa wingi. This will cost Tanzania big time.
 
In a nutshell: Magufuli anaonekana na watanzania kama mtu hodari na mchapakazi, kiuhalisia mimi naona kinyume chake.

Binafsi si msafiishaji wala sina uhusiano wowote na sekta hiyo , lakini ninasafiri sana kwa barabara nchi karibu zote za SADC, Suala la mizani na sheria zake zinazidi Kuwa tight hapa kwetu pengine kuliko nchi nyingine za sadc, na pengine ndo tunaongoza kwa rate ya uharibifu wa barabara kuliko wenzetu kwa sababu ya ubabe wa mtu mmoja tu, MAGUFULI !!!

Uharibifu wa barabara kwa kiasi kikubwa unatokana na sheria mbovu zilizowekwa na kusimamiwa na viongozi husika, kulalamkikia wasafirishaji ni sawa na kuficha ukweli wa tatizo, si kweli kuwa tunabeba mizigo mizito sana. Bali tuna utaratibu mbaya wa kubeba mizigo ndo maana barabara zetu hazidumu.

Kuna mawili huwa nafikiri dhidi ya wizara hii na watendaji wake: Either wananufaika na rushwa kutoka kwa wasafirishaji hivyo wanaopt njia ambazo hazitatui tatizo bali kuiongezea mzigo serikali na mtu wa kawaida au hawajui na hawako serious kuboresha pengne kuondoa kabisa sheria kandamizi zinazopelekea watu kutocomply.

Mfano: Botswana idadi ya juu ya axle ni 9 urefu mwanzo hadi mwisho ni mita 22, hapa kwetu ni axle 7 na urefu hautakiwi kuzidi mita 17!!! Put it simple: napokuwa na axle nyingi ndio unavyozidi kutetea barabara na the opposite is also true,

Ningekuwa mimi ndo Magufuli ningejiuliza swali moja -kwanini South Africa wanabeba mizigo mizito yet road network zao zina lifespan kubwa kuliko zetu na pia hawana idadi kubwa ya mizani kama sisi. Na bado wakifika Tunduma wanaona ni afadhali ku-offload mizigo na kupakia kwenye malori yetu??

Hivi kuna hasara gani TANROADS ikiruhusu axle 9 na urefu ukawa 22 metre! !! Kwanini Trailers za Interlink ambazo zinatuika karibu Africa nzima hapa kwetu ni marufuku? Remember: Australia wanabeba mpaka tani 80 kwa kuongeza idadi ya axle na kuto limit urefu! Na bado barabara zao zinadumu.
 
Rushwa kwenye mizani kumechangia sana kuua barabara zilizojengwa kwa mkopo ambao wananchi tutadaiwa miaka nenda rudi. Na idadi ya malori yanayopita kwa siku ni zaidi ya yale yaliyokisiwa wakati wa kujenga barabara hizo.

Waziri lazima awe mkali sana kwani tutafika mahali barax2 zitakufa, reli hakuna na wakopaji hawatoi tena mikopo!
 
Yeye anasema Magufuli ana chuki binafsi na transporters, mimi nasema yeye ana chuki binafsi na Magufuli.

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akihojiwa na kipindi cha television (sikumbuki kituo gani), jamaa aliyaongea hayahaya, tena kwa dharau na kebehi kubwa kwa magufuli utafikiri anamuongelea mtoto wake. Nilijiuliza sana huyu jamaa anapata wapi kiburi hiki? Nikahisi kuna nguvu nyuma yake na si bure!

Inawezekana jamaa ana hoja, lakini jinsi anavyowakilisha hoja zake inaudhi.

Simuungi mkono Magufuli, lakini si vema pia mtu kuwasilisha hoja kwa dharau kwa waziri mwenye dhamana!
 
Maroli yanaharibu barabara na ndio chanzo cha foleni mjini..hatuyataki wagome tuu
 
Yeye anasema magufuli anachuki binafsi na transporters, mimi nasema yeye ana chuki binafsi na magufuli. Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akihojiwa na kipindi cha television (sikumbuki kituo gani), jamaa aliyaongea hayahaya, tena kwa dharau na kebehi kubwa kwa magufuli utafikiri anamuongelea mtoto wake. Nilijiuliza sana huyu jamaa anapata wapi kiburi hiki? Nikahisi kuna nguvu nyuma yake na si bure!

Inawezekana jamaa ana hoja, lakini jinsi anavyowakilisha hoja zake inaudhi.

Simuungi mkono magufuli, lakini si vema pia mtu kuwasilisha hoja kwa dharau kwa waziri mwenye dhamana!

Mimi nasema hivi Magufuli akaze kamba kabiasaa haka ka ugomvi huenda kakatutoa watanzania. Mizigo yote siku zote inatakiwa isafiri kwa reli tu kupita barabarani iwe last resort huku kwetu ni kinyume reli imekua last resort matokeo yake gharama ya maisha inapanda na mbaya zaidi barabara zetu hazidumu kwa sababu ya kuelemewa. Kingine ajali zinakua nyingi ukizingati ni vijibarabara na wote tuna banana humo. Ni wakati mwafaka kwa Mwakyembe naye kuamka na kuimarisha reli zote ili zibebe mizigi hiyo. Kwa hili Magufuli namuunga mkono kwa sana!
 
Yeye anasema Magufuli ana chuki binafsi na transporters, mimi nasema yeye ana chuki binafsi na Magufuli.

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akihojiwa na kipindi cha television (sikumbuki kituo gani), jamaa aliyaongea hayahaya, tena kwa dharau na kebehi kubwa kwa magufuli utafikiri anamuongelea mtoto wake. Nilijiuliza sana huyu jamaa anapata wapi kiburi hiki? Nikahisi kuna nguvu nyuma yake na si bure!

Inawezekana jamaa ana hoja, lakini jinsi anavyowakilisha hoja zake inaudhi.

Simuungi mkono Magufuli, lakini si vema pia mtu kuwasilisha hoja kwa dharau kwa waziri mwenye dhamana!
Nakubaliana na wewe sana. Anaongea kwa kumdharau saba Magufuli. Na mimi pia nimejiuliza sana hii jeuri yake abaitoa wapi?

Ni kweli Magufuli kwa mtazamo wangu ni kionhozi wa wasi wasi ambaye kapata bahati ya kukubalika sana, lakini si rahisi kumdharau hivi mbele ya kadamnasi mtu kama yeye ambaye wengine wamefikia hadi kumpendekeza agombee urais
 
Zamani nilzani bonge la Waziri kumbe shipa tu, angalia alivyomwangusha Raila Odinga kule Kenya.

Mimi nawaambia bila Lowassa hakuna CCM hata mniloge habari ndio hiyo.
 
Magufuli anatakiwa aongeze faini. Watanzania walala hoi wanalipa madeni ya ujenzi wa hizi barabara, lakini watu kama wakina Hans Poppe wanaona ni sawa tu kupitisha magari yenye uzito juu ya kiwango kinachotakiwa.

Tofauti na huko nyuma sasa hivi hawa watu magari ya mizigo wamekuwa na kiburi sana wanapoambiwa wazingatie uzito, sijui wanatoa wapi hii jeuri? Kejeli za Hans Poppe ni kilelezo cha jinsi hawa watu wanajiona wao wana haki ya kubebesha mzigo watanzania wa kugharamia barabara ili mradi matumbo yao yajae.
 
Yeye anasema Magufuli ana chuki binafsi na transporters, mimi nasema yeye ana chuki binafsi na Magufuli.

Miezi kadhaa iliyopita alikuwa akihojiwa na kipindi cha television (sikumbuki kituo gani), jamaa aliyaongea hayahaya, tena kwa dharau na kebehi kubwa kwa magufuli utafikiri anamuongelea mtoto wake. Nilijiuliza sana huyu jamaa anapata wapi kiburi hiki? Nikahisi kuna nguvu nyuma yake na si bure!

Inawezekana jamaa ana hoja, lakini jinsi anavyowakilisha hoja zake inaudhi.

Simuungi mkono Magufuli, lakini si vema pia mtu kuwasilisha hoja kwa dharau kwa waziri mwenye dhamana!
Dawa ya moto ni moto, wamekutana hao, magufuli nae anakera sana kwa kauli zake
 
Mgari ya Ritz ni yeye anayasimamia!
 
Hivi hakuna sheria ya malori kupita kuanzia saa 7 usiku? Yanakera sana na kusababisha foleni hapa bongo...
 
Dawa ya moto ni moto, wamekutana hao, magufuli nae anakera sana kwa kauli zake
​Magufuli anachoweza sana ni kujikomba kwa JK kwa kumtaja kila baada ya dakika moja katika hotuba zake!
 
Nimemuona leo ITV asubuhi. Ana hoja za msingi ila kamponda sana mzee wa sifa, Magufuli.

Transporters wakigoma itakuwa balaa hapa. Mizigo itarundikana bandarini, meli hazitashusha mizigo, serikali italipa meli fees nyingi za kuziweka meli hapa, nchi jirani zitahama na kutumia mombasa na majanga mengine lukuki
 
Back
Top Bottom