Hanspaul: Mshahara wa Laki 5 usikatwe Kodi

Hanspaul: Mshahara wa Laki 5 usikatwe Kodi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Group, Satbir Singh Hanspaul amependekeza mwananchi anayepokea mshahara wa laki tano kushuka chini asikatwe kodi.

Hanspaul ameyasema hayo siku ya Jumatano, Januari 08, 2025 katika Mkutano wa Wafanyabiashara na Wamiliki wa kampuni wa Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika katika Serena Hotel, Dar es Salaam.
 
Wakuu

Mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Group, Satbir Singh Hanspaul amependekeza mwananchi anayepokea mshahara wa laki tano kushuka chini asikatwe kodi.
View attachment 3195925
Ana maono MEMA shida wanaoshauriwa maana mara nyingi mwenye shibe huwa hamjui mwenye njaa !
 
Wakuu

Mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Group, Satbir Singh Hanspaul amependekeza mwananchi anayepokea mshahara wa laki tano kushuka chini asikatwe kodi.
Huyu mtu ambaye hana ubini wa mtu mweusi hajazaliwa kwenye shida na changamoto za kiuchumi lakini ana huruma na wananchi kuliko viongozi ambao tunashare nao ubini na mazingira ya ukuaji
 
Wakuu

Mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Hanspaul Group, Satbir Singh Hanspaul amependekeza mwananchi anayepokea mshahara wa laki tano kushuka chini asikatwe kodi.
View attachment 3195925
Kumbe kuna mshahara wa laki?
Tzs au $
 
Tatizo hao wanaolipwa laki tano na chini ninwengi sana kiasi wasipokatwa kodi serikaki itapunguza mapato sana.

Hivyo, hiyo kodi ama itafutwe kwa wanaoliowa zaidi, ama serikaki ipunguze matumizi.

Hapa panatakiwa uchakataji wa namba kuangalia quantitative analysis.
 
Hanspaul Group - Wanajihusisha na vitu mbalimbali ila huyu hapa ni Bosi wa workshop kubwa ya ku assemble magari pamoja na kujenga bodi za magari ikiwemo kurefusha magari kama yale yanayotumika kwa utalii
Huyo Tajiri anafaa kuwa Rais wa Tanzania. Kama mfanyabiashara Donald Trump kapewa urais USA hata Huyu tajiri anafaa.
 
Sio kwamba jamaa anajitetea yeye? Mfano alikuwa akikulipa 500,000 wewe unachukua 400,000 halafu 100,000 inakuwa kodi. Wakisema chini ya 500,000 haina kodi anaanza kuwalipa watu wake 400,000 tu.
Wewe unapata 400,000 yako ile ile na yeye anaokoa 100,000 akiwa na wafanyakazi 100 hio ni 10m kwa mwezi savings.
 
Back
Top Bottom