Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Wiki jana nilienda kwa aunt yangu Kijichi kuna mitaa fulani ya ushuani fulani. Sasa nikasahau namba ya nyumba na jina la mtaa maana wana vimitaa vidogo vingi

Akawa hapatikani kwa simu, yeye alijua napakumbuka. Nilikuwa nakumbuka njia mbili, ya kutokea kwa Zombe yule askari au ya kutokea kwa Filikunjombe.

Kilichonichanganya katikati mitaani nilikutana na mbwa koko wengi kuliko watu. Yani Kijichi kuna mijibwa mingi njiani. Nikakumbuka hata kwetu pale sisi ndio wa kishua, mapaka hayakomi kuzalia kwetu ila sijawahi ona yanazaliana kwa majirani.

Conclusion niliyopata. Hata mbwa koko na mapaka yanajua wapi kuna makombo yakushibisha. Wanapokula miguu ya kuku na kutafuna mifupa yote hawawezi tembelewa na mbwa koko hata siku moja.

Jamani tutafute hela hata wanyama watuheshimu.
 
Mkuu maisha ya huko Oysterbay nimeishi sana tena ktk hiyo mijumba ya kifahari ila asikwambie mtu mkuu mambo yanayotokea usiku ni hatari sana yaani hao wenye hiyo mijumba wanafuga viumbe vyakutisha

Amini mkuu hao watu wanamaagano yakishirikina
 
Mkuu maisha ya huko oysterbay nimeishi sana tena ktk hiyo mijumba ya kifahari ila asikwambie mtu mkuu mambo yanayotokea usiku ni hatari sana yaani hao wenye hiyo mijumba wanafuga viumbe vyakutisha
Amini mkuu hao watu wanamaagano yakishirikina
Duh
 
Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.

Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.

Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.

Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.

Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.

Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.

Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.

Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.

Watoto wake wakakasirika sana.

Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?

Baba yao akasema ameshaamua.

Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.

Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.

Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.

Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.

Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.

Ukikipata unapata balaa.
 
OysterBay ya sasa si ile ya zamani Mkuu imeharibika sana. Nilipita mitaa hiyo hivi karibuni nilipigwa na mshangao wa hali ya juu. Miaka mingine 10 basi kunaweza kuwa Uswazi kabisa.
 
Tena inazidi kukuuma ukijuwa hizo raha na maisha bora ya viongozi yanatokana na kodi unayolipa, au hela waliokwapuwa Kifisadi...
 
Niliwahi kusikia kwamba ilikuwepo hata miaka ya karibuni inayofanywa na watu binafsi. Magari yao yako wazi kabisa kule nyuma ni Malori ya kawaida tu. Sasa kama kuna upepo uchafu wote hupeperushwa mitaani na kufanya uchafuzi mkubwa sana.
Hivi tunafananisha maisha ya Oysterbay na Ulaya.

Dar kuna huduma za umma za kuzoa taka?
 
Nikiwa zangu nakimbia jogging nikifika kwenye huu mjengo huwa nautazama sn..kijichi kuna watu Wana hela bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…