Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Asante kwa taarifa. Hii huduma muhimu.

Wamejitahidi.

Nilivyokuja US na kuona karibu kila kimji na kijiji kina Fire Brigade nilisikitika sana kulinganisha na Dar.

Mkuu upo US pande gan
 
Wiki jana nilienda kwa aunt yangu Kijichi kuna mitaa fulani ya ushuani flani. Sasa nikasahau namba ya nyumba na jina la mtaa maana wana vimitaa vidogo vingi. Akawa hapatikani kwa simu, yeye alijua napakumbuka. Nilikuwa nakumbuka njia mbili, ya kutokea kwa Zombe yule askari au ya kutokea kwa Filikunjombe.

Kilichonichanganya katikati mitaani nilikutana na mbwa koko wengi kuliko watu. Yani Kijichi kuna mijibwa mingi njiani. Nikakumbuka hata kwetu pale sisi ndio wa kishua, mapaka hayakomi kuzalia kwetu ila sijawahi ona yanazaliana kwa majirani.
Conclusion niliyopata: hata mbwa koko na mapaka yanajua wapi kuna makombo yakushibisha. Wanapokula miguu ya kuku na kutafuna mifupa yote hawawezi tembelewa na mbwa koko hata siku moja.

Jamani tutafute hela hata wanyama watuheshimu.

Ushuani huwez kuta koko wala mapaka shume yasiyokuw na kwao hyo umeonge ukwel mtupu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu maisha ya huko oysterbay nimeishi sana tena ktk hiyo mijumba ya kifahari ila asikwambie mtu mkuu mambo yanayotokea usiku ni hatari sana yaani hao wenye hiyo mijumba wanafuga viumbe vyakutisha
Amini mkuu hao watu wanamaagano yakishirikina

[emoji817][emoji817]umenena kitu cha kwel utajiri wa mtu ni fumbo analolijua yeye na Muumba wake
 
Hivi unajua Bongo kuna baadhi ya watu (hususan hao unaosema wanaishi kama ulaya), lakini ukweli ni kwamba wanaishi zaidi ya watu majority waliopo huko ulaya.... Hata kama upo Ulaya na una pesa za kutosha Ukija Bongo utaishi kwa raha / matanuzi zaidi kuliko ukiwa huko ulaya...
 
Kuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.

Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.

Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.

Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.

Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.

Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.

Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.

Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.

Watoto wake wakakasirika sana.

Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?

Baba yao akasema ameshaamua.

Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.

Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.

Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.

Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.

Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.

Ukikipata unapata balaa.

Kwel mzee
 
Tena inazidi kukuuma ukijuwa hizo raha na maisha bora ya viongozi yanatokana na kodi unayolipa, au hela waliokwapuwa Kifisadi...

Wacha kabisa ukiwakuta walinz wa kule sijui wanajikuta km nan vile yan
 
Nipo mitaa ya osterbay kwa mbali naona mjengo wa Mo Dewji kwa mbali tena naona mjengo wa Paul Makonda kwa pemben yang naona mjengo wa makamu wa rais nikapita Bongoyo road nikakutana na mjengo anaoish mtoto wa Bakhresa kwa kwel nimesikitika sana hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya kweli haya maisha hayako fear wengin tunaish tu dunian ila kuna viumbe wengine wanaenjoy life imebidi kuingia hapa simply fresh kupata hata ka kinywaji kidogo.

PESA INAUMUHIMU MKUBWA SANA KATIKA MAISHA YETU TUTAFUTE PESA JAPO AJIRA NI KIKWAZO SANA
Kanywe supu ya pweza uongeze ukoo. Hilo unaliweza. Mijengo waachie wenye nazo.
 
Back
Top Bottom