Shing Yui
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 15,168
- 38,049
Aisee! Umesikitika kwa kuona mambo mazuri? 😬😬😬kwel nimesikitika sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee! Umesikitika kwa kuona mambo mazuri? 😬😬😬kwel nimesikitika sana
Hapana mkuuKijichi ni Mbagara iliyochangamka.
Kipato chako hakizuii mwanamke kukuacha juzijuz bill gate inasemekana katarakiana na mke wakeNataman kuwa na nyumba kali.
Demu wangu asingeniacha kirahisi vile.
OysterBay ya sasa si ile ya zamani Mkuu imeharibika sana. Nilipita mitaa hiyo hivi karibuni nilipigwa na mshangao wa hali ya juu. Miaka mingine 10 basi kunaweza kuwa Uswazi kabisa.
Oysterbay ya msasani bonde la mpunga,maandazi road ,macho tirdo hahaaaaani uswahilini matola,mama ntilie kibao!!
Amini usiamini kuna watu kibao huku, hususan Wamarekani weusi, wanaondoka kimoja kuja kuhamia Bongo.Nakuzingua tu mkuu ila unakula life kaka
Mkuu mi nishakaa mpaka Tabata Ubaya Ubaya.Enzi hiyo Tabata Uswazi kwelikweli.Kiranga wa ushuani Oysterbay to U.S, hongera sn mkuu
Ziko wapi turushiemo wakulungwa tuzioneMkuu nimepiga pc ya nyumba ya mtoto wa bakhresa ila kwa kuibia sana kwamaan ni msalama macctv camera na walinzi juu na chin
Ujumbe mzuriKuna Mzee mmoja alikuwa anafanya kazi serikalini. Alikuwa mtu mkubwa kicheo.
Akawa kapandishwa cheo kikubwa kabisa kazini kwake.
Akapewa nyumba nzuri sana Oysterbay.
Karibu kabisa na ubalozi wa Marekani.
Watoto wake wakafurahi sana. Wakaona wanaenda kuhamia Oysterbay, tena karibu kabisa na Ubalozi wa Marekani.
Lakini, yule Mzee hakuwa mtu wa kupenda makuu.
Alisema anapapenda pale alipokuwa anaishi, maana pana sehemu kubwa, tena amezoeana sana na majirani. Wanaishi vizuri.
Zaidi, hakuona sababu za kuhamahama nyumba za serikali kwani alikuwa anakaribia kustaafu.
Watoto wake wakakasirika sana.
Wakasema Baba unaacha nafasi ya kuhamia Oysterbay, tena mtaa wa Laibon ukae jirani na rais Mwinyi na ubalozi wa Marekani?
Baba yao akasema ameshaamua.
Basi muda kidogo tu, ubalozi wa Marekani ukapigwa bomu. Ile nyumba ikapasukapasuka vibaya sana kwa sababu ilikuwa karibu sana na ubalozi wa Marekani.
Kama yule Mzee angehamia pale, familia yake ingeweza kuumia vibaya sana.
Watoto wale wakamuona yule mzee kama alikuwa na uwezo wa kuona yajayo.
Unaweza kutamani kitu kizuri, ukasononeka kukikosa.
Kumbe, usalama wako unakuja unapokikosa hicho kitu.
Ukikipata unapata balaa.
Ndio maana pesa inatafutwa kwa njia yoyote, ili mtu asionekane anapataje, USHIRIKINA ni kila kitu. Ukiuwa mtu utatiwa hatiani ila ukiua kishirikina hakuna ushahidi. Yaaaani we acha tu!
Ziko wapi turushiemo wakulungwa tuzione
Amini usiamini kuna watu kibao huku, hususan Wamarekani weusi, wanaondoka kimoja kuja kuhamia Bongo.
The grass is always greener on the other side.
Mcheki huyu Mnyamwezi anaifagilia sana Bongo huko Youtube https://www.youtube.com/channel/UCOhiR-6Y-MZtMERKRENrcRw
Nakumbuka tulikuwa tunakaa hiyo Oysterbay unayoisifia kuwa ushuani, basi kuna Bibi mzaa Baba alikuja kutoka Mwanza, kwa matibabu.
Sasa Bibi mwenyewe kashazoea maisha ya Mwanza kukaa na ndugu zake muda wote, ana nyumba yake, ingawa si Oysterbay lakini kwake.
Basi wee, kafika Oysterbay watu wote wanaondoka asubuhi kwenda makazini na mashuleni, kabaki mwenyewe na mfanyakazi na TV.
Bibi si akawa anasema anataka kurudishwa Mwanza. Hajazoea maisha yale ya Oysterbay yanamkinaisha, anamiss company yake Mwanza.Tukamwambia mbona una ratiba ndefu sana za matibabu bado bibi?
Ikawa anang'ang'ania kurudi Mwanza, mkimuachia peke yake anatoka getini anaanza kutembea anaanza kuuliza watu njia ya kwenda Mwanza wapi!
Wakati huo, huko Mwanza kuna vijana kibao hawajawahi kufika Dar wanatamani sana wangepata nafasi kufika Dar japo kwa wiki tu wasafishe macho.
Ni hulka ya watu tu.
The grass is always greener on the other side, mimi niliamua kujua nataka wapi nikajikita ninakotaka kimoja.
"Kweli tupambane sana kuzisaka fedha, lakini tunapokuwa na nafasi ya kuinitiate maendeleo at macro level tusijisahau"
Tukumbuke huyu tajiri akitoka ndani ya nyumba yake, tunasimama naye kwenye foleni kama kawaida. Imagine kipindi kama hiki cha covid-19 ambacho kusafiri nje ni shida tunaingia nao katika hospitali zilezile. Mmoja kati ya uliyewataja hapo alikuwa Dodoma muda fulani, gari yake ya maana kabisa ilisumbua , hakukuwa na namna, ikaingizwa garage. Nilichoshuhudia namna ilivyoshughulikiwa na thamani ya ile gari, nadhani alivyofika Dar (kama alifika nayo) lazima ilitafutiwa mtaalamu tena....Pamoja na utajiri wao na kwamba wako na unafuu kuliko sisi, lakini kuna bughudha zetu nao zinawasumbua sana. raham eid ukifika level za hao jamaa, kero zako zitahama, zitakuwa hizihizi tunazolalamika sisi kajamba nani!! 😀
umewahi kufika ulaya mkuu ?Ni zaidi ya Ulaya ukiwa na pesa
Aisee! Umesikitika kwa kuona mambo mazuri? [emoji51][emoji51][emoji51]