Hapa bongo kuna watu wanaishi kama Ulaya

Wale masela kule masaki Chanika ndani huko yani niliwakuta kama wana serikali yao ,wako Poa tu hamna stress na kuna mama muuza anawahudumia na kuna mabinti kadhaa nao wanagonga vyombo gongo. Ndumu jamaa wanalivuta tu kama fegi.
aisee walinifikirisha sana,nikiwaza mi madeni niliyonayo jinsi kulipa,+kodi alafu jamaa wanakula bata kivyao porini huko bila mawazo nikawaonea wivu haswa.
Polisi kule hamna
 
"Kweli tupambane sana kuzisaka fedha, lakini tunapokuwa na nafasi ya kuinitiate maendeleo at macro level tusijisahau"

Tukumbuke huyu tajiri akitoka ndani ya nyumba yake, tunasimama naye kwenye foleni kama kawaida. Imagine kipindi kama hiki cha covid-19 ambacho kusafiri nje ni shida tunaingia nao katika hospitali zilezile. Mmoja kati ya uliyewataja hapo alikuwa Dodoma muda fulani, gari yake ya maana kabisa ilisumbua , hakukuwa na namna, ikaingizwa garage. Nilichoshuhudia namna ilivyoshughulikiwa na thamani ya ile gari, nadhani alivyofika Dar (kama alifika nayo) lazima ilitafutiwa mtaalamu tena....Pamoja na utajiri wao na kwamba wako na unafuu kuliko sisi, lakini kuna bughudha zetu nao zinawasumbua sana. raham eid ukifika level za hao jamaa, kero zako zitahama, zitakuwa hizihizi tunazolalamika sisi kajamba nani!! πŸ˜€
 
Nakuzingua tu mkuu ila unakula life kaka
Amini usiamini kuna watu kibao huku, hususan Wamarekani weusi, wanaondoka kimoja kuja kuhamia Bongo.

The grass is always greener on the other side.

Mcheki huyu Mnyamwezi anaifagilia sana Bongo huko Youtube https://www.youtube.com/channel/UCOhiR-6Y-MZtMERKRENrcRw

Nakumbuka tulikuwa tunakaa hiyo Oysterbay unayoisifia kuwa ushuani, basi kuna Bibi mzaa Baba alikuja kutoka Mwanza, kwa matibabu.

Sasa Bibi mwenyewe kashazoea maisha ya Mwanza kukaa na ndugu zake muda wote, ana nyumba yake, ingawa si Oysterbay lakini kwake.

Basi wee, kafika Oysterbay watu wote wanaondoka asubuhi kwenda makazini na mashuleni, kabaki mwenyewe na mfanyakazi na TV.

Bibi si akawa anasema anataka kurudishwa Mwanza. Hajazoea maisha yale ya Oysterbay yanamkinaisha, anamiss company yake Mwanza.Tukamwambia mbona una ratiba ndefu sana za matibabu bado bibi?

Ikawa anang'ang'ania kurudi Mwanza, mkimuachia peke yake anatoka getini anaanza kutembea anaanza kuuliza watu njia ya kwenda Mwanza wapi!

Wakati huo, huko Mwanza kuna vijana kibao hawajawahi kufika Dar wanatamani sana wangepata nafasi kufika Dar japo kwa wiki tu wasafishe macho.

Ni hulka ya watu tu.

The grass is always greener on the other side, mimi niliamua kujua nataka wapi nikajikita ninakotaka kimoja.
 
Kiranga wa ushuani Oysterbay to U.S, hongera sn mkuu
Mkuu mi nishakaa mpaka Tabata Ubaya Ubaya.Enzi hiyo Tabata Uswazi kwelikweli.

Usinichukulie poa wa Obay tu.

Unapajua Tabata Ubaya Ubaya wewe?

Kuna siku nilirudishwa na mshkaji wa Obay, kuna shimo barabarani lilitaka kuimeza Vitara nzimanzima.

Mshkaji akaapa huku harudi tena, enzi hiyo barabara haijatengenezwa.
 
Ndio maana pesa inatafutwa kwa njia yoyote, ili mtu asionekane anapataje, USHIRIKINA ni kila kitu. Ukiuwa mtu utatiwa hatiani ila ukiua kishirikina hakuna ushahidi. Yaaaani we acha tu!
 
Ujumbe mzuri
 
Ndio maana pesa inatafutwa kwa njia yoyote, ili mtu asionekane anapataje, USHIRIKINA ni kila kitu. Ukiuwa mtu utatiwa hatiani ila ukiua kishirikina hakuna ushahidi. Yaaaani we acha tu!

Unaambiwa at serikal haiamin uchawi je ukikutwa na msukule ndan sio noma hiyo
 

Uko vzr mkuu mawe yapo nyumban ya kutosha inaonekana
 

Ni kwel mkuu umasikin unakaraha zake na utajir unakaraha zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…