Amini usiamini kuna watu kibao huku, hususan Wamarekani weusi, wanaondoka kimoja kuja kuhamia Bongo.
The grass is always greener on the other side.
Mcheki huyu Mnyamwezi anaifagilia sana Bongo huko Youtube
https://www.youtube.com/channel/UCOhiR-6Y-MZtMERKRENrcRw
Nakumbuka tulikuwa tunakaa hiyo Oysterbay unayoisifia kuwa ushuani, basi kuna Bibi mzaa Baba alikuja kutoka Mwanza, kwa matibabu.
Sasa Bibi mwenyewe kashazoea maisha ya Mwanza kukaa na ndugu zake muda wote, ana nyumba yake, ingawa si Oysterbay lakini kwake.
Basi wee, kafika Oysterbay watu wote wanaondoka asubuhi kwenda makazini na mashuleni, kabaki mwenyewe na mfanyakazi na TV.
Bibi si akawa anasema anataka kurudishwa Mwanza. Hajazoea maisha yale ya Oysterbay yanamkinaisha, anamiss company yake Mwanza.Tukamwambia mbona una ratiba ndefu sana za matibabu bado bibi?
Ikawa anang'ang'ania kurudi Mwanza, mkimuachia peke yake anatoka getini anaanza kutembea anaanza kuuliza watu njia ya kwenda Mwanza wapi!
Wakati huo, huko Mwanza kuna vijana kibao hawajawahi kufika Dar wanatamani sana wangepata nafasi kufika Dar japo kwa wiki tu wasafishe macho.
Ni hulka ya watu tu.
The grass is always greener on the other side, mimi niliamua kujua nataka wapi nikajikita ninakotaka kimoja.