Hapa Bongo, ukimkabidhi mama mali zako zote akulindie kama Hakimi, hakikisha kwanza umeandika wosia! 😂😂😭

Hapa Bongo, ukimkabidhi mama mali zako zote akulindie kama Hakimi, hakikisha kwanza umeandika wosia! 😂😂😭

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
Linaanzia kwenye mfumo wetu wa familia za Kiafrika, yaani EXTENDED FAMILY! Hapa ndugu si ndugu tu, ni ndugu pamoja na matawi yake yote! Unampa mama yako mali zako, kesho yake wajomba, shangazi, binamu mpaka watoto wa binamu wanajua dada yao ana ukwasi!

Mama akisema, “Hizi mali mwanangu ameniachia nizisimamie,” ghafla familia nzima inakuwa na mikakati ya maendeleo! Mmoja anataka mtaji, mwingine ada ya mtoto, mwingine anatunga uongo anaumwa apelekwe ulaya Mwisho wa siku unarudi nyumbani unakuta mali zimepigwa kata funua

Kwa walokole ndiyo balaa linafika level nyingine! Mama anaenda kanisani, mchungaji anahubiri kuhusu mbegu ya imani, mama anatazama akaunti yako anasema, “Bwana amenibariki kupitia mwanangu, ngoja nipande mbegu ili mavuno yaongezeke!”

Anatoa sadaka ya kupanda mbegu kwa imani kwamba Mchungaji atakuzidishia utajiri, kumbe wewe unatazamia statement ya benki unaona mali zako zinashuka kwa kasi ya lifti iliyokatika kamba!

Na sasa fikiria unampa pesa mama ambaye matapeli wakimpigia simu tu na kusema, “Mama, tuma hela kwenye hii namba, kuna tatizo la dharura!” Mama anakuwa tayari kutuma kabla hata hawajamaliza salamu!

Huyu ukimkabidhi mali zako halafu akakutana na matapeli waliobobea, wewe na yeye mtakutana kwenye kikao cha familia mkiwa wote ni wahanga! Utamuuliza, “Mama, hela ziko wapi?” Atakujibu, “Mwanangu, nimekubeba miezi tisa acha haya yapite tugange yajayo!”
 
Nimecheka hapo Pa kutuma hela kwa matapeli kabla hata hawajamaliza salamu.

Nimekumbuka mama angu alitapeliwa 170k, ilikua amtumie dogo, sijui wale walijuaje, wakatuma text , "hiyo hela tuma kwenye namba hii......."
Nayeye mda huo huo ni kutuma, 😂😂😂
 
Umenikumbusha dada mmoja ivi Znz enz izo alipigiwa simu na hawa jamaa , wakamwambia aende kwa wakala awatumie pesa yeye atachukua iliyo ingia kwenye sm .
Dada haraka haraka kaenda kwa wakala anamlazimisha atume maana walimuambia hela iliyo ingia abakishe na asante kama 50k .
Kwavile wakala alikua anamjua yule dada akatuma 400k aisee hela imeishaingia anaangalia muamala wake aloambiwa imeingia hewa nilimuonea huruma kweli.
 
Duuh hii mbaya sana.
 
kwa kweli sisi zetu ni dua tu. ilisikika sauti ya bwana mmoja alievaa msuri na barakashia
 
Ni tabia ya uoga na kuigana. Kwanini mali zako uandike jina la mama?. Mama yako anaweza kuolewa na hizo mali zake au urithi wake ukawa wa yeye na mume wake. Kama unampenda sana mama yako, mpe fungu lake kisheria na mali zingine gawa kwa jinsi utakavyo ona inafaa.
 
Kuna siku bibi yangu alinipigia simu Jane embu Fanya laki moja Hapo nadaiwa mjukuu Wangu Fanya haraka Sana
Nikajikakamua nikatuma

Sasa siku nimeenda nasema ngoja niangalie miamala niliyomtumia mwezi huu ni kiasi gani
KatIka pekua pekua nakuta Ile ela aliyoomba kwangu kaifowadi kwa mwanawe wakiume last born (itabidi niulize machawa what happened naambiwa mjomba alitoka na gari akagonga so ilitakiwa ela) imagine

Ndo wazazi WA Africa unaweza muandikisha vzr kwa mapenzi ila mwishowe ndugu zangu Ndo wanafaidi

Ila kama wewe ni WA kikeuandikishe Tu Baba yako zitakuwa salama
Dad's wetu wapo vzr Sana kulinda vya mabinti zao
 
Nimecheka hapo Pa kutuma hela kwa matapeli kabla hata hawajamaliza salamu.

Nimekumbuka mama angu alitapeliwa 170k, ilikua amtumie dogo, sijui wale walijuaje, wakatuma text , "hiyo hela tuma kwenye namba hii......."
Nayeye mda huo huo ni kutuma, 😂😂😂
Hao matapeli ndio ilikuwa mbinu yao, mkielewana na mtu mwengine utume pesa, meseji yao wakibahatisha kuifikisha kipindi upo kwenye hatua, unaweza kutapeliwa kirahisi sana
 
Kwa walokole ndiyo balaa linafika level nyingine! Mama anaenda kanisani, mchungaji anahubiri kuhusu mbegu ya imani, mama anatazama akaunti yako anasema, “Bwana amenibariki kupitia mwanangu, ngoja nipande mbegu ili mavuno yaongezeke!”
Hahaha
 
Hao matapeli ndio ilikuwa mbinu yao, mkielewana na mtu mwengine utume pesa, meseji yao wakibahatisha kuifikisha kipindi upo kwenye hatua, unaweza kutapeliwa kirahisi sana
Haswaa
 
Ni tabia ya uoga na kuigana. Kwanini mali zako uandike jina la mama?. Mama yako anaweza kuolewa na hizo mali zake au urithi wake ukawa wa yeye na mume wake. Kama unampenda sana mama yako, mpe fungu lake kisheria na mali zingine gawa kwa jinsi utakavyo ona inafaa.
Au akahonga kibenten zote

Ova
 
Mali zangu watarithi wanangu kwa majina yangu.... Kwann niandke la mzazi sjui ndg ?? Upumbavuu mtupu
 
Naona watu mnalishana matango pori, kuandika jina la mama yako ni salama zaidi. Mama akifa mali zinabaki kwa wanawe au mtoto wake, hakuna atakayejua mali zaidi ya wewe na marehemu, watagombania urithi ambao hawana ushahidi nao au hawajui ni wapi ulipo?

Kuweka mali ktk majina ya mama yako mzazi ni salama, labda uwe ktk familia isiyoeleweka na isiyojitambua.
 
Back
Top Bottom