Mungu ametuwekea mambo ya kutupa raha machache sana yaani ukifikiria raha ni kunywa pombe, kula chakula, kufanya mapenzi na kulala usingizi.ila cheki majanga yalivyo mengi magonjwa, majanga ya asili, umaskini, ajali n.k
At least kidogo tungekuwaga na uwezo wa kupaa Kama ndege yaani unaruka angani ile ni raha kwa kweli.
Mkuu, kwa mujibu wa huu uzi; kila kitu ni STAREHE narudia tena kila kitu ni STAREHE. Hapo ninamaanisha kile ambacho kwako ni kero au hakikupi raha , basi kwa mwenzio ni starehe kubwa sana hadi moyo unasuuzika kabisa. Nitatoa mfano;- 1.
Wewe ukipata ajali
say ya gari na kuumia sana yupo atakayetoa comment "Yes, na akome, alizidi mno kuturingia na kigari chake" i.e. amefurahia kuumia kwako.
2. Wewe ukilala njaa, yupo atakayesema "nilijua tu- huyo hatoboi"
3. Mwanao au Jamaa yako akiugua halafu akafa, ukienda kwa muuza majeneza (yah. kwa wakristo) baada ya kununua usishangae akakuambia "..karibu tena ndugu yangu
😀
4. Ukiachika (kwa Ke) au ukitelekezwa (kwa Me) wapo watakaoshangilia kwa furaha sana.......
5. Yanapotokea mafuriko, hiyo ni fursa (furaha iliyojificha) kwa waokoaji n.k.
Wahenga walisemaga
"One man's meat is another man's poison"
Ndio maana utakuta wapo watu wanafurahia vita, wanaobaka, wauaji n.k. na ndipo likawepo neno la Husda, Wachawi n.k.......
Kwa kifupi Furaha yako ni Kero kwa wengine. Ni mtizamo wako tu ili kitu kiwe ni majanga.